Let take the argument a notch higher. Tanzania imetia sahihi na kutambua Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Haki za Binadamu (rejea hotuba ya Mwalimu kwenye Umoja wa Mataifa). Azimio hilo kwa kiasi kikubwa ni msingi wa Haki za Msingi (Bill of Rights) za Katiba nyingi za nchi mbalimbali. Natambua kuwa baadhi ya yaliyomo kwenye Azimio hilo yameanishwa kabla katika Katiba mbalimbali na Maandishi mbalimbali kabla yake.
Kwa ajili ya hoja zetu tuangalia Ibara ya 20 kwanza:
Inasema Msisitizo wangu.
Article 20.
- (1) Everyone has the right to freedom of peaceful assembly and association.
- (2) No one may be compelled to belong to an association.
Katiba ya Tanzania inamlazimisha mtu kujiunga na jumuiya au chama fulani. Kwa kusema kwamba mtu hawezi kugombea nafasi ya uongozi isipokuwa awe mwanachama wa chama cha siasa (siyo ya dini, shirika n.k) Katiba yetu inavunja moja kwa moja ibara hiyo.
Nayo Ibara 21 sehemu yake inasema:
Article 21.
- (1) Everyone has the right to take part in the government of his country, directly or through freely chosen representatives.
Kama "Kila mtu" anayo haki ya kushiriki katika utawala wa nchi yake moja kwa moja (kama kiongozi) au kuchagua kwa uhuru wawakilishi wake basi Katiba yetu inatunyima haki ya kuchagua kwa uhuru kwani tunaambiwa NI LAZIMA tuchague mtu aliye kwenye chama cha siasa.
Sasa inakuwaje kama yupo Mtanzania ambaye ana uwezo na ana nia ya kushiriki katika uongozi wa taifa lake (per article 20) na wananchi wanataka awaongoze (iwe udiwani, ubunge au Urais) lakini Katiba inasema hawezi kwa sababu japo ana sifa nyingine zote lakini hana ya uanachama je kwa hili siyo uvunjaji wa Azimio hilo kwa kuwanyima watu uhuru wa kumchagua?
Je, kama tunaambiwa mnaweza kuwachagua x,y, z, d, a lakini hamuwezi kumchagua m kwa sababu hajajiunga na kikundi cha siasa, je kama tunamtaka "m" kutuongoza (no pun intended here) si kwamba tumenyimwa uhuru huo kwa kuweka kipengele cha kulazimisha chama cha siasa? Mahakama zimeshaamua huko nyuma jibu ni ndiyo.
Lakini naweza pia kutoa hoja nyingine kutoka kwenye azimio hilo; nayo ni ajira.
Article 23.
- (1) Everyone has the right to work, to free choice of employment, to just and favourable conditions of work and to protection against unemployment.
Kama mimi nataka kuwa diwani na kwamba hiyo ndiyo iwe kazi yangu ya kunipa ujira lakini sitaki kuwa mwanachama wa chama cha siasa, kwa kunilazimisha nijiunge na chama hicho kunaninyima uhuru wa kuchagua ajira niitakayo?