Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini?

Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini?

Godwine,
Kuruhusu mgombea binafsi itawezesha watu wenye uwezo kupata nafasi ya kuongoza nchi hii ikumbukwe mara nyingi kwenye vyama hasa CCM wagombea wao huwa sio wale wenye uwezo ila wale wenye mtandao uwe wa ufisadi au la!

pindi watakaporuhusu mgombea binafsi basi tutakuwa na demokrasia ya kweli maana wale wanaenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha ugombeaji wa tiketi ya chama husika wanakuwa na nafasi ya kugombea kama binafsi! Haswa watakapokuwa na uhakika na msukumo wa umma kama chaguo la wananchi. Mfano Dr Salim A. Salim, Prof.

Mwandosya wangeweza kugombea 2000 au Kikwete 1995. Kwa hiyo ufisadi utapungua kwa kiasi kikubwa sana!
 
Tumewahi kuwa na mfumo wa mgombea binafsi kipindi cha nyuma yaani 1960s na matokeo yake yalionekana kwa mgombea binafsi (Sarwat )kule mbulu kushinda ubunge dhidi ya TANU.

Hakuna mfumo usiokuwa na madhara yake ila la msingi ni mechanism imara ya kukabiliana na changamoto kuuimarishaaa..

Naunga mkono hoja ya mgombea binafsi kama chachu ya kupanua DEMOKRASIA zaidi nchini.
 
Luteni,

Ibara 30(5) kinasema hivi..............

(5) Where in any proceedings it is alleged that any law enacted or any

action taken by the Government or any other authority abrogates or abridges any of the basic rights, freedoms and duties set out in Articles 12 to 29 of this Constitution, and the High Court is satisfied that the law or action concerned, to the extent that it conflicts with this Constitution, is void, or is inconsistent with this Constitution, then the High Court, if it deems fit, or if the circumstances or public interest so requires, instead of declaring that such law or action is void, shall have power to decide to afford the Government or other authority concerned an opportunity to rectify the defect found in the law or action concerned within such a period and in such manner as the High Court shall determine, and such law or action shall be deemed to be valid until such time the defect is rectified or the period determined by the High Court lapses, whichever is the earlier.


na Ibara 13 (2) kinasema hivi..............

13.-(2) No law enacted by any authority in the United Republic shall make any provision that is discriminatory either of itself or in its effect.

Je Ibara ya 98 inaondoa uhalali huo hapo juu....hebu tuione inasemaje hapa chini............

98.-(1) Parliament may enact law for altering any provision of this Constitution in accordance with the following principles:

(a) a Bill for an Act to alter any provisions of this Constitution, other
than those relating to paragraph (b) of this subarticle or any provisions of any law specified in List One of the Second Schedule to this Constitution shall be supported by the votes of not less than two thirds of all the Members of Parliament; and

(b) a Bill for an Act to alter any provisions of this Constitution or any
provisions of any law relating to any of the matters specified in List

Two of the Second Schedule to this Constitution shall be passed
only if it is supported by the votes of not less than two-thirds of all
Members of Parliament from Mainland Tanzania and not less than
two-thirds of all Members of Parliament from Tanzania Zanzibar.

(2) For the purpose of construing the provisions of subarticle (1), alteration of provisions of this Constitution or the provisions of a law shall be understood to include modification, or correction of those provisions or repeal and replacement of those provisions or the re-enactment or modification of the application of the provisions.
 
nyauba

kipindi cha nyerere ni tofauti kwani hakuna fisadi ambaye angejitokeza kusaidia mtu kwani mfumo wa usalama ulikuwa mkubwa mno wangeweza kumfuatilia na kumweka pabaya lakini sasa hivi ata ukiwa fisadi lakini ukitoa msaada kwa wananchi wanaokupenda basi unapata uongozi, wananchi wamekuwa wauza madaraka wakubwa sana, lazima tuliangalia swala hili kwa pande mbili ili tuweza kupunguza madhara na mwanya utaoletwa na sheria hii kwa waharifu,ili uwe mfumo wenye mazuri mengi kuliko mabaya ,
 
ELNIN0,
Mkuu serikali ilipoambiwa kuwa katiba inatoa haki kwa private candidate na kutakiwa ku-amend katiba accordingly, contrary, CCM mijambazi ya demokrasia ikakimbilia bungeni kuongezea kifungu kinachosema ..."ni lazima uwe mwanachama wa chama cha siasa ili uweze kugombea nafasi za uongozi"...

BS
 
Mkuu.......serikali ilipoambiwa kuwa katiba inatoa haki kwa private candidate..........majambazi wa demokrasia wakakimbilia bungeni kuongezea kifungu kinachosema ......."ni lazima uwe mwanachama wa chama cha siasa ili uweze kugombea nafasi za uongozi"........BS

Nakubaliana na wewe. Hivi hii serikali ya CCM inaogopa nini hasa kuhusu wagombea binafsi?
 
Nadhani maeneo ya mijini ni rahisi sana mgombea binafsi kushinda! Kule vijijini wamezoea kuona wagombea wenye mabendera yakiambatana sambamba na Khanga, Kofia na Pilau itakuwa kazi sana kuwashawishi wachague Mgombea binafsi. Ni mawazo yangu haya
 
Nadhani maeneo ya mijini ni rahisi sana mgombea binafsi kushinda! Kule vijijini wamezoea kuona wagombea wenye mabendera yakiambatana sambamba na Khanga, Kofia na Pilau itakuwa kazi sana kuwashawishi wachague Mgombea binafsi. Ni mawazo yangu haya

umesahau tarumbeta za kapteni Komba!!
 
umesahau tarumbeta za kapteni Komba!!

There we are! Tuna safari ndefu sana ndugu yangu.......sisi wepesi sana wa kusahau. Uende bila bendera, bila pilau, kofia, Tshirt, Khanga, na tarumbeta hutaeleweka jamaa wa CCM hata wakiweka TOY wapiga kura watachagua hilo.
 
Nadhani maeneo ya mijini ni rahisi sana mgombea binafsi kushinda! Kule vijijini wamezoea kuona wagombea wenye mabendera yakiambatana sambamba na Khanga, Kofia na Pilau itakuwa kazi sana kuwashawishi wachague Mgombea binafsi. Ni mawazo yangu haya

Masanilo ndugu yangu, nilibahatika kuwa kijijini kwetu wakati wa uchaguzi wa 2005, sasa wakati wa kampeni - gari za CCM ziliingia pale kijijini kwa bwembwe - watu wanaacha watoto majumbani - jikoni kina mama wanaunguza kwenda kwenye magari ya CCM,

kina baba wakaacha kazi zao wote kukimbilia kuona Magari ya CCM, baadaye next day wakaja CUF, hakuna mtu alienda talk of the village ikawa jamaa wana gari mbili tu - hawafai - tukiwapa uongozi hadi wale kwanzaa washibe ndiyo watujali sisi - bora tuwape walioshiba kabisa.

hii ni kweli na nakuhakikishia mkuu, kwa hiyo na support point yako.
 
Nimesoma kwenye baadhi ya magazeti (Majira la jana 9/2/10) na mijadala mingine huru ya mitandaoni na nimesikiliza mijadala kwenye "vibanda vya gahawa" inaonekana watu wanaongea bila kufikiria au hawaelewi.

Watu wanasema eti kitendo cha serikali kukata rufaa dhidi ya hukumu ya kesi ya mgombe binafsi lengo lao icheleweshwe hadi uchaguzi ufike so kitendo cha mahakama ya rufani kutamka kuwa maamuzi ya mahakama kuu yataendelea kuheshimiwa ni sawa na kuiumiza serikali.

Mimi naomba niulize..Kuna sababu gani za msingi za serikali kuogopa mgombea binafsi wakati iko wazi kabisa kuwa mgombea huyo hawezi kushinda urais na hata kwenye ubunge itakuwa ni idadi ndoooooooooooooooooooogo na inawezekana wasiwepo?

Au serikali inaogopa vipi mgombea binafsi wakati wao ndo wenye dola na wna kila aina ya mbinu ya kihuni kushinda?

Naombeni mawazo yenu wakuu. Tusijidanganye, soni sababu ya serikali kuogopa mgombea binafsi
 
Serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi - Ofisi ya Rais (Bunge na Uratibu) Philip Marmo amesema hakutakuwa na mgombea binafsi kwa mwaka huu 2010.

Akiwa Bungeni ambako anaendelea kunguruma, alisema kuwa mchakato wa kubadili katiba ya nchi ni mkubwa, hivyo hata mahakama itakuwa tayari imeridhia kuwepo kwa mgombea binafsi, muda hautatosha kuibadili.

Bado demokrasia inaminywa Tanzania? tujadili
 
hilo mbona liko obvious kabisa? hata marmo naona kahangaika tu kusema kitu ambacho sie tulijua kitambo sana.

pia siamini kama ni kuminyaa demokrasia. jiulize kwa uelewa wa waTZ mgombea binafsi anafaa kwa sasa? angalia JK anavyokosolewa, angekuwa ni rais "binafsi" hali ingekuwaje?

Hamuoni kuwa rais wa chama fulani inasaidia angalau kuna vikao vya kikatiba kuwekana sawa inapotokea rabsha serikalini na kati ya serikali na mihimili mingine ya dola?
 
Hata mimi nimemsikia Marmo, sababu pekee aliyotoa ni muda.

Hukumu ya mahakama kuu olitamka wazi kuwa mgombea binafsi 2010.

Kama Zanzibar itafanya mabadiliko ya katiba pamoja na kura ya maoni kabla ya uchaguzi mwezi October, sembuse badiliko la katiba tuu bila hata referendum!.

Serikali ina dharau, imelidharau bunge, na imeidharau ile hukumu ya mahakama kuhusu mgombea binafsi, amini nawaambieni, mahakama kuu ya rufaa, itatoa hukumu ya kukazia utekelezaji wa hukumu ya kuruhusu mgombea binafsi. Hii ndio the only legacy Jaji Agustino Ramadhani, atawapa Watanzania zawadi kabla ya kustaafu rasmi Dec, 31, 2010.
 
we marmo kwanini unaidharau mahakama, unajua hiyo ni sawa na kusigina katiba? kwani hukumu ilitolewa lini mpaka mkashindwa kubadili katiba?
 
Akili Kichwani,
Unadhani JK anakosolewa kwanini? Angekuwa anawajibika na kuutmikia umma kwa uadilifu angelalamikiwa kwanini?

Inaelekea kwa uelewa wako ni kwamba mgombea binafsi ataiendesha nchi kama familia yake.Kumbuka taasisi zote za utawala zitaendelea kuwepo (serikali, mahakama, bunge, nk) na rais hataendesha nchi kwa matakwa yake bali kwa mujibu wa sheria.

Tofautisha ugombea binafsi na "katiba binafsi" (if there were such a thing)!
 
we marmo kwanini unaidharau mahakama, unajua hiyo ni sawa na kusigina katiba? kwani hukumu ilitolewa lini mpaka mkashindwa kubadili katiba?

Wakuu... kweli demokrasia ni nzuri sana..... lakini haya mambo hayatabadilishwa kwa kutumia keyboard za computer. Inatakiwa tamko la kizembe namna hiyo liamshe hasira zetu tuingie mitaani ili kuwakumbusha kuwa hii nchi ni yetu.... wote
 
Mimi nilitarajia kabisa hili kutokea.. Marmo ametamka bila hata ya chembe ya soni..hakuna dhamira ya dhati ya kukuza demokrasia katika nchi hii.
 
Chama Cha Majambazi hawawezi kukubali mgombea binafsi kwa sababu wakifanya hivyo wanafahamu tonge limeshatoka kinywani.
 
Chama Cha Majambazi hawawezi kukubali mgombea binafsi kwa sababu wakifanya hivyo wanafahamu tonge limeshatoka kinywani.

jamani msijifariji? nani anaweza kuwa mgombea binafsi na kushinda Tanzania? hizi sio zile wanazoita ndoto za mchana? wananchi wa tanzania uelewa wao ni mdogo sana hatujafikia level hiyo wakuu, angalia tu kamati ya mwakyembe na kuchonga koooooote kule kumbe hakuna kitu! tuendelee kujenga demokrasia taratibu, tutafika tu.
 
Back
Top Bottom