Gangi Longa
JF-Expert Member
- Feb 5, 2010
- 275
- 135
Godwine,
Kuruhusu mgombea binafsi itawezesha watu wenye uwezo kupata nafasi ya kuongoza nchi hii ikumbukwe mara nyingi kwenye vyama hasa CCM wagombea wao huwa sio wale wenye uwezo ila wale wenye mtandao uwe wa ufisadi au la!
pindi watakaporuhusu mgombea binafsi basi tutakuwa na demokrasia ya kweli maana wale wanaenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha ugombeaji wa tiketi ya chama husika wanakuwa na nafasi ya kugombea kama binafsi! Haswa watakapokuwa na uhakika na msukumo wa umma kama chaguo la wananchi. Mfano Dr Salim A. Salim, Prof.
Mwandosya wangeweza kugombea 2000 au Kikwete 1995. Kwa hiyo ufisadi utapungua kwa kiasi kikubwa sana!