Uchaguzi 2020 Mgombea kupitia CHADEMA, Tundu Lissu achukua fomu za Kugombea Urais wa Tanzania ofisi za NEC Dodoma

Tunaweza kweli kukosa, ila sio kwa njia ya kura, bali kwa maagizo ya rais. Rais anaahidi uchaguzi huru kama nani wakati na yeye ni mshindani?
Hili la mhe rais kuahidi uchaguzi huru na wa haki lakini kivionya vyombo vya ulinzi na usalama visitumie nguvu katika uchaguzi,limekua ni pigo kubwa sana kwa cdm.
 


😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂
 
KUB ameshindwa kutumia ata zila 8B kuhonga vijanna wa boda boda angalau 2000 wampe msafara wa maaana ona izi aibu
 
Tunaweza kweli kukosa, ila sio kwa njia ya kura, bali kwa maagizo ya rais. Rais anaahidi uchaguzi huru kama nani wakati na yeye ni mshindani?
Yeye ni mkuu wa nchi na ana dhamana ya kuhakikisha nchi inabaki kuwa na amani hata kama yeye naye ni mgombea. Uchaguzi utakuwa huru na haki ila nyinyi Chadema mnatengeneza mazingira ili mkishindwa mseme haukuwa huru na haki.

Chadem huwa mnapenda kudanganya ila kwa ujanja. Nikupe mifano mitatu:
Wakati wa kumuaga Marehemu Rais mstaafu uwanja wa taifa mliongopa mmezuiwa kuingia, laki mwenzenu Mr Sugu akasema kuwa mlichelewa uwanjani. Kama Sugu asingetoboa ukweli huo watanzania wangapi wangeamini uongo wenu?

Lijualikali wakati alipokasirika kwa kufukuzwa bila kupewa fursa ya kusikulizwa alitoboa siri jinsi mlivyoiba kura kule Kilombero, na mtu anapokuwa na hasira huwa anachosema mara nyingi kinareflect ukweli.

Tatu, m/kiti wenu alipoumia kwa bahati mbaya nyumbani kwake Dodoma mlidanganya kuwa kashambuliwa lakini uchunguzi wa polisi na maelezo yaliyotolewa yalionyesha dhahiri pasina shaka kuwa tukio lile lilitokana na yeye kuteleza na sio kushambuliwa.

Ingieni katika uchaguzi lakini eleweni kuna kushinda na kushindwa. Uungwana ni kukubaliana na maamuzi ya wapiga kura. Nchi hii ina wapiga kura milioni 29 hivi katika vijiji elfu 12 na miji yote ya Tz, wanaoshabikia humu mitandaoni hawafiki hata milioni 3. Mtapata baadhi ya kura lakini hamtafikisha hata robo ya viti vya ubunge na urais hamshindi.
 
Anapoteza muda huyu,bora angeenda kuomba ubunge huenda angeambulia kitu,urais kwake itakuwa ni ndoto na kamwe haitatimia

Kwanza kwenye ushindani lazima kuna wakwanza mpaka wa mwisho. Toka nchi hizi imeanza, waliowahi kuutaka urais ni zaidi ya 200, lakini watano tu ndio wamefanikiwa mpaka sasa. Hakuna ajabu haya yeye asipokuwa rais. Maana kuwa rais nchi hizi, uwezo sio kigezo pekee, bali kigezo namba moja ni mbeleko ya vyombo vya dola. Haymta hivyo kushinda sio sifa pekee ya urais, bali hata idadi ya kura zako huchangia idadi ya viti maalum. Huenda unadhani kugombea ushindi ndio matokeo pekee ya kugombea urais.

Anayepaswa kuona aibu iwapo atashindwa, ni aliyekuwa mzima bila kuguswa na risasi hata moja mwilini, kufanya siasa peke yake kwa miaka mitano, kumiliki kundi la watu wasiojulikana, kufanya lolote atakalo bila kuhojiwa. Sio huyo aliyekuwa kitandani kwa miaka mitatu bila kufanya siasa.
 
Huyu mgombea wenu msaliti wa Tanzania ataendelea kuongoza kwa kura mitandaoni. Hakuna mtanzania makini anayeijua vyema Tanzania anaweza kupoteza muda hata kufikiria kwamba Lissu atakuwa Rais wa Tanzania.

Kwa watu makini wanaoijua dunia vizuri na ambao wanajua hila na njama za nchi za magharibi kwa nchi za Africa wanamuona Lissu kama nyoka,huyu ni mtu ambaye anataka kuitumbukiza Tanzania kwenye mikono ya MABEBERU.

Wenzetu LIBYA,Congo DRC ,Angola na nchi nyingine zenye rasilimali walishapitia hali kama ambayo wengi mnaojiita wasomi mlioko kwenye social media mnaitaka kwa kushabikia vibaraka mbwa mwitu wa wazungu.

Ni bahati mbaya sana kwenu hili mnalolitaka halitafanikiwa kamwe maana nchi ipo mikononi mwa Mwenyezi Mungu na kwa maajabu ya Mungu amemponya Lissu baada ya kushambuliwa na Chadema ili kuichafua serikali ya Mh Rais Magufuli yupo hai ili aone Magufuli anavyosimamia transformation ya Tanzania.

Kuna maisha ya mitandaoni na maisha halisi,kuna siasa za mitandaoni na siasa za huko site.
Tukutane Oct 28 na msisite kuipongeza CCM na Rais Magufuli japo mmejiegesha kwa wazungu wafadhiri wenu.

Mapovu ruksa.
 
Yeye ni mkuu wa nchi na ana dhamana ya kuhakikisha nchi inabaki kuwa na amani hata kama yeye naye ni mgombea. Uchaguzi utakuwa huru na haki ila nyinyi CDM mnatengeneza mazingira ili mkishindwa mseme haukuwa huru na haki...

Uchaguzi hausimamiwi na rais bali tume ya uchaguzi, anaahidi yeye kama nani wakati tunajua fika kuwa yeye ndio huwa anaagiza box la kura linajisiwe?

Hakuna uwezekano wowote wa ccm kushinda hata kama itashinda kwa zaidi ya 60%. Na hata hizo 60% ccm itafikisha kwa sababu tume sio huru, na kila taasisi ya nchi hii inadhani ina wajibu wa kuibeba ccm itangazwe washindi fullstop.
 
Jana tuliambiwa jiji la Dodoma litatikiswa hatari, mara wanafunzi wa UD, CBE kumbe ilikuwa propaganda utopolo.
 
Huyu mgombea wenu msaliti wa Tanzania ataendelea kuongoza kwa kura mitandaoni. Hakuna mtanzania makini anayeijua vyema Tanzania anaweza kupoteza muda hata kufikiria kwamba Lissu atakuwa Rais wa Tanzania...

Hizi ni propaganda za kizee, na sehemu kubwa ni za wazee au vijana wa ccm wasioweza kujitegemea nje ya mbeleko za madaraka, hivyo unaogopa ikitokea serikali na chama unachokitetea kikatoka madarakani, itabidi ukaolewe kwa ugumu wa maisha.
 
Niko area D watu wabugujika machozi ya furaha kwa kutaka kumuona Mh, Lissu ..aaah Magufuli yuko ICU hawezi kutoboa hata mshindi wa tatu hataingia ,nadhani hii coalition yake na Tlp ndo itamsaidia kuingia top 5
Hahahahahaaaaaa aaaah!!
 
Hili la mhe rais kuahidi uchaguzi huru na wa haki lakini kivionya vyombo vya ulinzi na usalama visitumie nguvu katika uchaguzi,limekua ni pigo kubwa sana kwa cdm.

Pigo la nini, au yeye ndio huwa anaviagiza hivyo vyombo kutumia nguvu? Na lile kundi la watu wasiojulikana nalo kalipeleka likizo?
 
Hizi ni propaganda za kizee, na sehemu kubwa ni za wazee au vijana wa ccm wasioweza kujitegemea nje ya mbeleko za madaraka, hivyo unaogopa ikitokea serikali na chama unachokitetea kikatoka madarakani, itabidi ukaolewe kwa ugumu wa maisha.
Hizi hoja ni za hovyo sana kwa level zako aisee, au ni hasira?
 
Niko area D watu wabugujika machozi ya furaha kwa kutaka kumuona Mh, Lissu ..aaah Magufuli yuko ICU hawezi kutoboa hata mshindi wa tatu hataingia ,nadhani hii coalition yake na Tlp ndo itamsaidia kuingia top 5
Naona nyomi limejaa barabara hazipitiki
 
Huyu mgombea wenu msaliti wa Tanzania ataendelea kuongoza kwa kura mitandaoni. Hakuna mtanzania makini anayeijua vyema Tanzania anaweza kupoteza muda hata kufikiria kwamba Lissu atakuwa Rais wa Tanzania...
Ni ajabu sana kwamba unaweza kumtaja Mwenyenzi Mungu na kuwaita MABEBERU (kwa herufi kubwa) watu ambao wameumbwa kwa sura na mfano wa huyo Mwenyenzi Mungu!!

Watu hao unaowaita MABEBERU wanachangia asilimia kubwa ya budget yetu ya kuendesha serikali na miradi ya maendeleo, na siku hizi wakitua KIA, mawaziri wanatupa takwimu!!😂 lakini kuweza kumtaja Mungu na kuita wanadamu wenzako MABEBERU, Wewe ni genious!!😂
 
Awajaenda ata na Mnyika wangenyimwa form sijui wangesemaje ndio wajue hakuna mtu mwenye shida ya kuwazuia haki yao demokrasia.

Vyama vingine vyote vimetii utaratibu uliowekwa wa kwenda na makatibu wao wa vyama isipokuwa CDM tu, hawa watu inabidi wabadilike wafuate vitabu kama wengine na kuacha kujiona wao ni special breed.

Lingetokea la kutokea huko wangeanza kulalama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…