Uchaguzi 2020 Mgombea kupitia CHADEMA, Tundu Lissu achukua fomu za Kugombea Urais wa Tanzania ofisi za NEC Dodoma

Uchaguzi 2020 Mgombea kupitia CHADEMA, Tundu Lissu achukua fomu za Kugombea Urais wa Tanzania ofisi za NEC Dodoma

Hadi hapo NEC itakapokuwa huru, huru kabisa isifungamane na chama chochote. Hadi hapo raisi wa nchi atakapopunguziwa madaraka ya kuteua na kuchafua vile anajisikia, hadi hapo ndio hizi porojo zitakuwa na uhalisia, otherwise CCM itaongoza hadi vizazi.
 
Aisee nieamini makamanda wa hapa JF ni bendera fuata upepo, hakuna hata mmoja mwanachama halisi wa Chadema, pereree tu

Mpaka sasa jamaa ameshachukua fomu hakuna hata picha moja

Chadema ni mitandaoni tu, tena kwa watu wachache wenye ID's nyingi
SH.
tapatalk_1496084922915-1.jpg
 
Anapoteza muda huyu,bora angeenda kuomba ubunge huenda angeambulia kitu,urais kwake itakuwa ni ndoto na kamwe haitatimia
 
Mwaka huu CCM hawashindi. Tutafanya kampeni ya kufa na kupona kuwaelimisha wananchi kuwa CCM haifai na tutawaeleza vizuri wachague Chama sahihi na chenye Sera sahihi na watu sahihi Chadema ili waweze pata maendeleo ya kweli.
Nikikuona wewe mwenyewe ukifanya hizo Kampeni za nyumba Kwa nyumba, utakuwa umasaidia Sana kumwangusha mgombea aisee
 
Hata sisi mnatushangaza sana. Magu alisema anataka kuifanya TZ iwe kama ulaya lkn miaka 5 ameshindwa kuifanya iwe kama Rwanda tuu.

Alisema hatanhuko ulaya kuna sehe ziko TZ tuu hawana kila kitu sasa je ni ulaya gani.iyo anayotufananishia?
Ninyi sera yenu ni kuonyesha majeraha ya risasi na kumshambulia Magufuli. Habari ya kuwafurahisha chadema ni mashambulizi na matusi kwa mhe rais. Lakini kumbukeni sanduku la kura linakawaida ya kusaliti. Huu umaarufu wenu jamiiforums usiwalevye.
 
Ni Tanzania tu kwa ukanda EAC ndo kuna usawa wa kidemokrasi.
Lakini uvunjaji wa sheria mkubwa mnaofanya ni sababu tosha ya kuwatoa ama kuwafuta kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi.
Sheria ipi imevunjwa ?
 
Aisee nieamini makamanda wa hapa JF ni bendera fuata upepo, hakuna hata mmoja mwanachama halisi wa Chadema, pereree tu

Mpaka sasa jamaa ameshachukua fomu hakuna hata picha moja

Chadema ni mitandaoni tu, tena kwa watu wachache wenye ID's nyingi
IMG_20200808_114937.jpg
 
Haaaaaa nimeona hofu kubwa kwa wale jamaa wa NeC cdm noma wamehakikisha pale pale ndani ya begi kuna nn
Subirini mtanange uanze ndiyo mtaamini kama mgombea wenu ana ubavu wa kuzunguka nchi nzima bila kurudi tena ubeligili kwa check up.Tanzania ni square km 945,000.Inahitaji msuli kuizungukia
 
Ninyi sera yenu ni kuonyesha majeraha ya risasi na kumshambulia Magufuli. Habari ya kuwafurahisha chadema ni mashambulizi na matusi kwa mhe rais. Lakini kumbukeni sanduku la kura linakawaida ya kusaliti. Huu umaarufu wenu jamiiforums usiwalevye.
Hahah kwa hio hamtaki aonyeshe majeraha yake?

Tena ningeshauri Lissu apige kampeni akiwa amevaa bukta kabisa kila mtu ajionee wakombozi wa wanyonge walichomfanya Lissu.
 
Kutoka maeneo mbalimbali kwenye viunga vya mji wa Dodoma, Tundu Lissu leo anachukua Fomu ya Urais.

===

Tundu Lissu leo kwa Mara ya kwanza anarejea katika mji wa Dodoma akienda kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea Urais. Ikumbukwe Tundu Lissu mara ya mwisho kuondoka katika mkoa huu ni baada ya kupigwa risasi.

Fuatilia baadhi ya matukio na picha mbalimbali za tukio hilo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA Tundu Lissu akiwa amewasili katika Ofisi za Chadema Kanda ya Kati zilizopo jijini Dodoma na kupokelewa na viongozi mbalinbali wa Chama, wanachama, wapenzi na mashabiki wa Chadema, kabla ya kuelekea Ofisi za Tume ya Uchaguzi kuchukua fomu, leo Jumamosi 08/08/2020.

====

TUNDU LISSU AFIKA OFISI ZA NEC KUCHUKUA FOMU YA UTEUZI

Mgombea Urais Tanzania kupitia Chama cha CHADEMA, Tundu Lissu amefika katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuchukua fomu ya Uteuzi ya kugombea Urais

Lissu amefika katika Ofisi hizo na Mgombea Mwenza Salum Mwalim huku wakiwa wamesindikizwa na Wanachama wengine. Wamekabidhiwa fomu hizo na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage

Uchukuaji fomu za kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 umeanza Agosti 5 hadi 25,2020.

Lissu amechukua fomu, wamezihakiki na kujiridhisha kisha wameondoka katika Ofis za NEC ili kuendelea na taratibu nyingine za kichama.

#JamiiForums #Siasa #JFSiasa #Uchaguzi2020
Mungu ibariki Tanzania, amani na upendo vitawale ktk kipindi hiki Cha Uchaguzi mkuu
 
Ni Tanzania tu kwa ukanda EAC ndo kuna usawa wa kidemokrasi.
Lakini uvunjaji wa sheria mkubwa mnaofanya ni sababu tosha ya kuwatoa ama kuwafuta kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi.

Ni kweli, maana hizi ndio mbinu za ushindi za Magufuli toka akiwa mbunge.
 
Kuna vijibwa vya mboga mboga vilikuwa vinabweka toka asubuhi kuwa Chadema wameingia chaka kupanga tarehe ya leo kwenda kuchukua form, yaani CCM wamechanganyikiwa wanavizia tu kumuengua Lissu ili wapate mteremko. Safari hii tutabanana hadi kipenga cha mwisho.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
1596877761537.png

kila mtu yuko na ishue zake bana 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂
 
Back
Top Bottom