Mgombea Umeya Arusha alalamika wapiga kura kutekwa

Mgombea Umeya Arusha alalamika wapiga kura kutekwa

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Diwani wa kata ya Daraja Mbili kupitia CCM, Prosper Msofe ambaye aligombea Umeya wa jiji la Arusha na kupata kura 9 amelalamikia yaliyotendeka katika uchaguzi huo.

Msofe amelalamikia wapiga kura kutekwa na kuwekwa kwenye ‘bar’ ambao pia walikatiwa mawasiliano naye. Amesema viongozi kuingilia uchaguzi unanyima haki za msingi za wananchi.

Ametoa rai kwa CCM na Serikali kuwa Uchaguzi uachwe kuwa huru, na wagombea wasibebwe.

Katika uchaguzi huo Maximilian Ilangye, diwani wa kata ya Kaloleni alichaguliwa kwa kura 24 na kuibuka kuwa Meya wa jiji hilo. Aidha Isaya Doita diwani wa Kata ya Ngarenaro kupitia CHADEMA alipata kura mbili.

​
 
Hajielewi nn huyu? Ajue tupo kwny enzi ya one man show; aliyepita Nina limetoka juu; aamini km anavyomwamini yesu au mtume.
 
Back
Top Bottom