Uchaguzi 2020 Mgombea Urais CCM kuhutubia kwa kisukuma huko Mwanza. Huu ni ukabila. NEC tunasubiri kuona hatua kali dhidi yake

Kila siku mnatukana wasukuma washamba mara magu msukuma anapendelea kanda ya ziwa haya kaja kuwaonyesha usukuma mnalalamika aiseee
 
Magufuli 5 tena.

Wamkaya
Mwalimu Nyerere alipata kusema ”namchagua huyu kwa sababu ni kabila langu". Akaendelea kueleza kuwa hii si sawa kwani hatuendi kwenye uchaguzi kuchagua kabila. Kadhalika watu waliofirisika kisela hujinasibu kwa kabila, rangi au dini. Na hivi ndivyo inavyoonekana katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi.
 
Yaani hyo mwaka huu ataongea lugha zote ,lakini hawexi kufikisha 52% alizopata mwaka 2015
 
Nani.alikwambia watanzania wote wanajua kiswahili?,lengo ujumbe uwafikie walengo kwa mtindo wowote ule,hakuna ubaya wowote
 
Nani.alikwambia watanzania wote wanajua kiswahili?,lengo ujumbe uwafikie walengo kwa mtindo wowote ule,hakuna ubaya wowote
Njoo na takwimu ya watanzania wangapi hawajui kiswahili
 
Sio Kisukuma tu mheshiwa Rais amekuwa akitumia vilugha mbalimbali kusalimia audience, Halafu pamoja na kuwa Rais wa Nchi huyo pia ana kwao ambako ni Usukumani sioni shida kufanya ivo
 
Inasikitisha kabisa tumerudi nyuma miaka 80. Viongozi wa aina hii ni hatari kwa mshikamano wetu tusiwachague.
 
Safari hii hata aongee kihutu lazima tumchape
 
NEC tunasubiri kuona hatua kali dhidi yake
 

Hapa ndio tutaona Tune ikichukua hatua kama kweli iko huru. Tena tunataka itangaze hatua hizo hadharani.
 
Kwa kifungu kipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…