Uchaguzi 2020 Mgombea Urais CCM kuhutubia kwa kisukuma huko Mwanza. Huu ni ukabila. NEC tunasubiri kuona hatua kali dhidi yake

Wasukuma pekee ni Milioni ngapi Chief? Kama umeenda shule njoo na jibu halafu nikulipue
Tabora, Simiyu, Mwanza, Shinyanga na Geita ni mikoa mitano ambayo yote ni ya kabila mmoja la wasukuma.

Ndio kabila kubwa kuliko makabila yote Tanzania kama ulikuwa hufahamu.

Rais kuongea kisukuma sio kosa kumbuka anaongea na kundi kubwa la watu na havunji sheria.
 
Mgombea wa ccm alipokuwa Magu amehutubia kwa kisukuma mwanzo mwisho. Ninakushauri kaeni naye na mumwambie asiiharibu nchi yetu kwa kupanda mbegu ya ukabila.

Wasukuma kwa wingi wao wangeamua kuwa wakabila huyo Nyerere angepata taabu tangu miaka ile ya sitini mwanzoni. Na asingeongoza kwa amani.

Huwa inashangaza kuona makabila madogo yakijitutumua na kutaka kusikika na kutawala makabila makubwa.
 
Nec ipi Mkuu? Hii hii au kuna ingine?
 
Wala sio ukabila!!!
 
Wasukuma kwa wingi wao wangeamua kuwa wakabila huyo Nyerere angepata taabu tangu miaka ile ya sitini mwanzoni. Na asingeongoza kwa amani.

Huwa inashangaza kuona makabila madogo yakijitutumua na kutaka kusikika na kutawala makabila makubwa.
Kwa hiyo sasa ni wakati wa makabila makubwa kutawala!!!??
 
Mtatapatapa kutafuta visingizio mpaka BASI! Nasubiri Lissu naye alivalie njuga hili ingawa naye nilimsikia akiongea kilugha cha kwake pale kwao. Msisumbuke na vitu vidogo vidogo au ndiyo dalili za mfa maji au uhaba wa SERA!?
 
Hujanielewa nilichomaanisha.
Tutaelewana tu. Yawezekana nimekuelewa vile usivyotaka nikuelewe na si lazima nikuelewe utakavyo.
Ndio maana tuna utashi na uwezo wa kutafakari kila mmoja anao wake.
Sentensi moja inatosha kufikisha ujumbe husika
 

Kama hawaelewi kiswahili, kwa hiyo ataongea kote aendako? naona kaanzia Mkoa wa Simiyu, Shinyanga, Mara, Geita na ataendelea kufanya hivyo Tabora, Katavi na Rukwa haya yote ni mikoa yenye idadi ya kutosha ya Wasukuma?
 
Mh. raise anaboa sana kwa hii tabia yake.
kiswahi yenyewe hajui msimlaumu ,hawezi kuongea sentensi moja iliyonyooka kwa kiswahili ,english hajui na kiswahili hajui lia ameamua kuja na kisukuma
 
Yeye anafikiri mwanza wanaishi wasukuma peke yao? Wengi hapo kwenye mkutano hawamwelewi, Tanzania ina makabila zaidi ya 120 na wanaishi mikoa mbalimbali bila kujali kabila gani.
Ina maana jamaa anaomba kura kutoka Kabila lake tu?
 
Tutaelewana tu. Yawezekana nimekuelewa vile usivyotaka nikuelewe na si lazima nikuelewe utakavyo.
Ndio maana tuna utashi na uwezo wa kutafakari kila mmoja anao wake.
Sentensi moja inatosha kufikisha ujumbe husika
Hakuna wakati wa kabila kubwa wala dogo kutawala, ujumbe ni kwamba tuwashukuru kina Nyerere kwani kama wangekuwa hawana maono basi kabila kubwa kama wasukuma wangesumbua tangu miaka ile ya sitini mwanzoni baada tu ya uhuru.

Nigeria na mataifa mengine makubwa yalishindwa kuwadhibiti “wasukuma” wao na mpaka kesho wanasumbuka.
 
Kwa hiyo ni lugha ipi inapaswa kutumika katika kampeni zinazoendelea?
Si vibaya baada ya kuona ushahidi huo ambao umetengenezwa na wanaouvunja kujitoa ufahamu kisha kujibaraguza...
Yasipokemewa sasa basi yaachwe ili kila mwenye kutafuta kura kwa kunena kwa lugha na azitafute ili mwisho wa siku tuvune matunda tunayofurahia sasa!!
 
Rais Duni kama huyu hivi aliwahi kuwepo nchi gani nyingine ?
 
Asilimia kubwa ya wanaokuwepo katika hiyo mikutano wanaelewa kisukuma na sio kwamba kwa kuongea kisukuma kuna kifungu cha katiba kinavunjwa.

Hili ni jambo dogo sana kulinganisha na yaliyoandikwa kwenye ilani ya kurasa 303 yenye kutakiwa kutekelezwa ndani ya miaka mitano.

Nyerere alikuwa anaongea kizanaki mpaka katika mikutano ya CCM miaka ile na hakuna aliyewahi kumkosoa.

Tuachane na hizi nongwa za kitoto.
 
Endelea kupamba kaburi lkn ndani mwake ni uvundo mtupu. Swali: Kutumia kilugha kwenye kampeni ni kuendeleza ubaguzi na ukabila. Kweli si Kweli??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…