Ukweli ni kwamba Rais Magufuli yupo kwenye msongo mkubwa wa mawazo, alijiaminisha kila mtu anamuabudu kisa fix zake za kujenga uchumi bila kujua kuwa watu wana hali mbaya.
Rais Magufuli anataka kuwaaminisha watu wavumilie shida ambazo yeye haziishi, huyu mtu haishi kwenye shida ya njaa, afya na kufunga biashara. Yeye anapewa kila kitu na wanaompa wanamuaminisha kuwa hali ni nzuri sana ili walinde vibarua vyao.
Sasa anapita huko akiona watu kibao anajua anapendwa sana, kesho yake anamshuhudia Lisu akiwa na umati ule ule bila uwepo wa Diamond, Kiba, Harmonize na mazombie wengine, hapa Magufuli kama binadamu mwenye akili zake anaona hali sio nzuri huenda napakwa mafuta kwa mgongo wa chupa ila huenda hali ni ngumu na nikisema niende kichwakichwa nikaibe bila mipango yanaweza nikuta kama yalivyowakuta wenzake huko duniani baada ya kuiba kura kijinga na anajua siku watu wakiamua CCM wenzake watamkimbia asubuh na mapema abaki mwenyewe.
Mimi binafsi sina tatizo na Magufuli kuwa Rais ila nina tatizo na hili dhehebu lake jipya aliloanzisha la kusifia na kutukuza.