Uchaguzi 2020 Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu afanyiwa mahojiano kwenye kipindi cha ITV dakika 45

Nilipenda alivyojibu maswali alitulia sana. Hoja zilipangaliwa kwa ufundi ukubwa. Alieleza sera zake huku akionesha mapungufu yaliyopo katika awamu hii.

Kama viongozi wa taifa hili wangekuwa wanapatikana kwa ubora wa ilani na hoja walizonazo basi tayari huu jamaa alimaliza kazi jana.
 


..TL ni mwanazuoni wa sheria, utawala, siasa, na katiba.

..alinishangaza alivyosema kauli mbiu ya kupambana na Ujinga, Umasikini, na Maradhi, ni ya uchaguzi wa mwaka 1958.

..waTz wengi wamekuwa wakiamini kauli mbiu hiyo ni ya baada ya Uhuru, kumbe ni ya kabla ya Uhuru wa Tanganyika.

..kwenye suala la Katiba, wakati wasomi wengi wanataja katiba ya mwaka 1977, TL amezama mpaka katiba ya 1962, na akazama zaidi mpaka katiba ya 1926.

..kuna kipindi ulikuwa unaona jinsi reaction ya mtangazaji inavyobadilika kutokana na elimu aliyokuwa akiipata toka kwa TL.
 
Yes....nilimuona yule mtangazaji alikuwa anatabsamu namna hoja zinavyojengwa. Huyu jamaa ni msomi na anaijua historia ya nchi.
 
Namchukia Lissu,namchukia Lissu kuliko mtu yoyote Tanzania na Duniani.
Namchukia Lissu kwasababu anawazindua WaTanzania ambao walikuwa hawajui Katiba ya JMT ina mapungufu mengi ambayo kwayo imesababisha kukwama kwa maendeleo ya nchi.

Namchukia Lissu kwasababu anahubiri habari ya Uhuru na Kazi, Uhuru na Umoja, Uhuru na Maendeleo. Hivi huyu Lissu nani kamtuma ebo atuachia nchi yetu sisi hatutaki haki,hatutaki uhuru na maendeleo tunataka madaraja,flyover,mabwawa ya umeme,mandege mengi na maviwanja ya ndege na barabara.

Namchukia Lissu nani alimwambia tunataka tume huru,bunge huru,mahakama huru sijui TRA inayomsikiliza mfanyabiashara.Tume watuletee yoyote kadri watakavyo,TRA watoze kodi kubwa kubwa hata kama biashara zitakufa zife sisi tunataka madaraja,Mahakama ziamue zitakavyo sisi hatuna shida na mshindi na mshindwaji.Nasema tena na tena Lissu funga domo lako sisi na madaraja madaraja na sisi.
 
one of the best interview!..congole H.E . Lissu
 
Yes....nilimuona yule mtangazaji alikuwa anatabsamu namna hoja zinavyojengwa. Huyu jamaa ni msomi na anaijua historia ya nchi.

..Nasema ana uwezo wa kukaa pamoja na viongozi wengine wa Afrika na akawafunika.

..Na huyu ndiye kiongozi ambaye Tanzania inamhitaji.

..Maraisi wa Tanzania wamekuwa ni viongozi wa Maraisi wengine wa Afrika.
 
Watumishi wa lissu nawaona mupo kazini kudanganya watanzania. Nawatakia kazi njema.
 
Maswali yalikuwa ya kawaida Sana Tena nahisi CDM ndio waliyatunga. Hakukuwa na critic qn hata moja
 
Huyu jamaa ni world class leader, anaweza akajenga hoja na dunia ikafata anachosema.
Mungu mkubwa aliepusha mkono wa binadamu usimuondoe.
 

Morogoro, Tanzania
Uhuru na Haki ya Kujiletea Maendeleo ya Watu binafsi

Mwekezaji alalamika serikali kutompatia mazingira ya uhuru na haki ili aendelee kuleta Maendeleo ya Watu.

Prof. Martin Shem anayemilika ardhi kwa ajili ya ufugaji mkubwa wa kisasa anasema serikali hailindi Haki na Uhuru wa wawekezaji kuendesha shughuli za maendeleo.

Source : ITV Tanzania
 
Tanzania ni nchi mtu anaamka asubuhi anaenda kushinda kijiweni na ardhi ipo,Tanzania ni nchi mtu anaona kituko hata kama ni bomu limeripuka wanakimbilia kuona,Tanzania ni nchi ambayo watu wanatukana vijiweni na mitandaoni bila kuulizwa chochote isipokua wachache sana

Halafu mtu anasema watu hawapo huru??

Huyu jamaa anaitwa Tundu Lisu ni muhuni tu anatengeneza namna ya kusukuma maisha yake kiuchumi na kutafuta heshima
 
Huyu Lissu ni zaidi ya Genius!
 

Wewe ni MJINGA tu kama walivyo WAJINGA wengine wa aina yako...

Hujachelewa, unahitaji KUELIMISHWA ili UJINGA ukutoke...!

Niwie radhi kama nitakuwa nimeku - offend kwa kukupa sifa ya "UJINGA"...

Lakini sina namna nyingine ya Kuku - describe kwa namna unavyofikiri na kutoa fikra zako katika maandishi yako....
 
✳️TUNDU LISSU AJIBU HOJA YA YEYE KUTUMIKA NA MABEBERU KATIKA UCHAGUZI MKUU 2020

Mgombea Urais kwa Tiketi ya Chadema,Tundu Lissu alijibu swali aliloulizwa na wandishi wa habari waliokusanyika nyumbani kwake Jumatano 9/9/2020 , "JE TUNDU LISSU INASEMEKANA UNATUMIKA NA MABEBERUU, NA UNAWEZA KUIUZA NCHI KWA MABEBERU IKIWA UTAKUWA RAIS?"


Mheshimiwa Tundu Lissu alianza kulijibu swali hilo kwa kuuliza swali " JE HAO MABEBERU NI AKINA NANI?

MAJIBU YAKE YALIKUWA HIVI!!

LISU : Hao mabeberu ni akina nani? Mkinipa jibu la hao ni akina nani, basi the rest is easy,

Je ni wamerakani?, Kama marekani ni mabeberu, basi kumbuka wanatufundishia Polisi wetu na wanajeshi wetu wanapofanya military exercise na majeshi mengine ya east africa, anayelipa ni Wamarekani, Africa command iliyocko based Germany ndio wanao cordinate na kufundisha hao wanajeshi wetu!! Je hao wamarekani ndio mabeberu? Kama hao ndio mabeberu basi tuambie nani anayetumiwa kati ya serikali yenu(CCM) Au mimi? wakati polisi wenu na usalama wenu mnafundishiwa na hao mnaowaita Mabeberu

Hao ambao wana fund, wanatoa misaada ya madawa tunazotumia, Are they mabeberu?Hawa ambao wamekuwa wanatupa misaada tangu uhuru ambao nyerere alienda kuomba chakula cha njaa mwaka 1962, hao ndio mabeberu? Hao ambao kipindi cha kikwete ndio walitoa uniform za wanajeshi wetu wote , je hao ndio mabeberu?

Hii hoja ya mabeberu ni hoja ya KIJINGA NA KIPUMBAVU kabisa!!.Hizi nchi ni nchi Rafiki za Tanzania , zilikuwa rafiki wakati Nyerere, wakati wa Mwinyi, Mkapa na hata Kikwete lakini Rais Magufuli ndio amevuruga marafiki zetu wote

Mimi(Lissu) nasema, tuta repair this damage to our international diplomacy, lazima tutawarudia marafiki zetu wote wamarekani, Waingereza, wachina,Warusi na kila mmoja ambaye amekuwa rafiki yetu miaka yote hii ambaye amevurugwa na kuitwa beberu na Rais magufuli wakati bado wanaenda kuwaomba misaada, ila sisi(Serikali ya Chadema) tutatengeneza upya huo uhusiano wetu wa kidiplomasia wa kimataifa ulioharibiwa na Rais Magufuli

Sasa kama sisi Chadema, tukifanya hivyo ni kuwa tunatumika na mabeberu, Sasa niambieni kwanini mnatumia madawa yao mbalimbali kama ya ukimwi,Malaria n.k Hata swala la kusomesha watoto, ule mradi wa kuboresha elimu, mmelipiwa na nani? mmeenda kukopa hao mabeberu! Hii ni nchi ambayo ni omba omba kwa miaka yote alafu tuna ujasiri wa kusimama na kuwaita watu mabeberu? Huku tunawaomba misaada? Huu ni ujinga kabisa!

Nani anayesaini mikataba ya madini na makampuni ya nje ya hao tunaowaita mabeberu?Nani anayemiliki madini yetu,by the way?.Miaka 5 ya magufuli , ni nani anayemiliki mgodi wa geita?ambao ndio mgodi mkubwa kuliko yote katika nchi hii Nani anayemiliki mgodi wa nyamwungu na Bulyanhulu na Buzwagi? utaona ni hao hao ambao mnawaita mabeberu ila miki nikizungumza mnasema Lissu anatumiwa na mabeberu ila akija mzungu wanazungumza nae wanasema Mwanaume amekuja yaani wakiwapa hela mnawaita wanaume ! Huu ni ujinga kabisa

Fikirieni, Nyinyi amshangai kwamba wale waliodai wametuibia kwamba hawajalipa kodi ya dola bilioni 495 hiyo kesi imeishia wapi?wakawakamata wakina deo mwanyika na kuwafungulia makosa makubwa lakini leo hiyo Deo mwanyika ndio mgombea wa ccm , Sasa hapo nani anatumia ufisadi, nani anatumika na mabeberu?Hivyo tuachane na haya maneno ya kupeana ujinga ujinga yasiyo na maana

Kwahiyo Mimi we will build our international diplomacy, maana bila kuwa na diplomasia huru basi nchi yetu tumekwisha.Magufuli anafikiri na sisi Tanzania ni Donar country? Are we donar country?Tanzania hii isiyoweza kulipa mishahara ya wafanyakazi wake, sisi ndio donar country?

Lazima tufahamu sisi(Tanzania) ndio tunaihitajo dunia kwani dinia inaweza kuendelea bila kununua pamba ya Tanzania au corosho ya Tanzania, au kahawa ya Tz au almas ya tanzania au dhahabu ya tanzania, dunia inaweza ikaendelea bila kununua chochote cha Tanzania, ila Je sisi Tanzania tunaweza kuka survive au kuendelea bila kununua vitu vya dunia? Can we survive?Kwahiyo hapa donar country ni nani?

Hayo ndio majibu ya Mhe tundu lissu aliyojibu alipoulizwa kuhusu kutumiwa na Mabeberu.....

Usikose kuendelea kujua maswali mengine mengi ya mtego aliyoulizwa Mhe Tundu lissu na kuyajibu kwa ufasaha wa hali ya juu..# Ni YEYE- 2020
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…