Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Kampeni za uchaguzi zishaanza.
Wagombea wanakatiza nyika sehemu mbalimbali za nchi kuzinadi sera zao. Wanatoa kila aina ya ahadi. ‘Mimi nitafanya hivi, nitafanya vile, nitafanya haya, nitafanya yale’.
Sasa mimi ni mmoja wa watu ambao huwa sitegemei mwanasiasa au mtu mwingine kuniboreshea maisha yangu. Naamini hilo jukumu linaanzia na kuishia kwangu mimi mwenyewe. Nimemsikia mgombea wa CHADEMA akitoa ahadi tele. Ahadi zinazowapagawisha misukule wake.
Moja ya ahadi anazotoa ni ile ya bima ya afya kwa wote. Yaani kila mtu, kila raia, eti awe na bima ya afya. Mimi si mtaalamu wa mambo ya bima wala mambo ya afya. Na wala sina ‘usomi’ wowote ule. Nimeishia kidato cha nne tu 🤣😉. Hivyo, huenda nikawa na uwezo mdogo wa kuelewa na kuchanganua mambo.
Katika ahadi zake hizo, sijasikia namna ambayo mgombea huyo wa CHADEMA ataweza kumpatia kila raia hiyo bima.
Hizo hela atazitoa wapi? Ataenda kuziomba kwa nchi hisani? Ataongeza viwango vya kodi ili kuongeza mapato yatayotumika kuileta hiyo bima? Au ataomba kwa Mungu atudondoshee hizo hela toka mbinguni?
Ahadi ni tele. Namna ya kuzifanikisha ahadi hizo, mpaka sasa ni sufuri!
Oh, na jingine ambalo sijamsikia kabisa akilizungumzia ni hili suala la Corona.
Kulikoni wewe mbeba maono wa CHADEMA? Ushakubali sasa kuwa Corona haipo? Au ushakubali kuwa ipo, lakini si hatari kama tulivyolishwa matango pori na Wazungu?
Manake we mwenyewe tokea urudi, zaidi ya mwezi sasa, huvai cha barakoa na wala hujitengi na jamii!
Unajichanganya kama ilivyo ada na sijakuona hata mara moja ukipiga chafya wala kukohoa.
Kwenye suala la Corona, hata kama huwezi kukiri kwa sauti, nahisi kimoyomoyo unakubaliana na jinsi Ngosha alivyoamua kukabiliana nalo😉.
Sisi akina Ngosha hatukutishika. Mfano mimi, hakuna hata siku moja niliyojifungia ndani. Sijawahi kuvaa barakoa. Na bado nipo nadunda nikibeba maboksi tena yale mazito kwelikweli ilhali kuna watu eti mpaka leo hii wamejifungia ndani kama mwali.
Mangosha wa ukweli hawawezi kujifungia ndani wakiogopa mafua na kikohozi💪🏿💪🏿.