Uchaguzi 2020 Mgombea Urais wa CHADEMA, Lissu kaahidi Bima ya Afya kwa wote

Uchaguzi 2020 Mgombea Urais wa CHADEMA, Lissu kaahidi Bima ya Afya kwa wote

Watu wenye upeompana wa ufahamu wa mambo wanataka Lissu afafanue fedha za mambo yote anayoahidi anazitoa wapi kama ni kodi basi aseme.
kama JPM kashindwa kuongeza ajira yeye Lissu ataongeza ajira atazitoa wapi?.sio kupayuka tu kama anakula ugali na mrenda.
Exactly!

Ahadi kila mtu anaweza kuzitoa. Si ni maneno tu....
 
We ushasikia hizo ahadi atazifanikishaje? Hela za bima ya afya kwa watu wote atazitoa wapi? Atazichapisha labda?
Itakua una uwezo mdogo wa kufikiri.
Kwani wanaofungiwa umeme wa elfu 27 hizo hela zinatoka wapi?

Huoni ni sisi ndio tunaowalipia kwa kununua luku wanakata percentya REA??
 
Selikali ya CCM inadhurumu watanzania.
Bima ya Afya ninayo nakatwa kwenye mshara wangu. Lakini nikienda hospital Hakuna Dawa, hakuna vifaa tiba, hakuna Madaktari, glaves ni aibu sana kwa kweli. Unaelekezwa duka unalopaswa kwenda kununua hivyo fifaa na dawa.

Bila matibabu Bima ya Afya ni mzigo.
*Inadhulumu* siyo ‘inadhurumu’.

*Gloves* siyo ‘glaves’.

*Vifaa* siyo ‘fifaa’.
 
Msukule ni baba ako na mama ako walioshindwa kukutunza ukakimbilia marekani kwenda kubeba box.

Wewe mbeba box utawashauri Nini watanzania.? Maisha yako tu mtihani.

Elimu bure ndio nyie wapumbavu mlisema haiwezekani? Leo ni bilion 22 tu kwa mwezi kwa nchi inayokusanya trion 1 kwa mwezi..

Bima wapi Lissu amesema atatoa bima bure? Lissu alisema ataleta bima na atahakikisha zinakuwa zenye ufanisi sio za Sasa za kulipa laki 190


Halafu unaambiwa dawa hakuna upumbavu mtupu kweli ukiwa CCM unakuwa mpumbabu Sana .

Swala gani halitekelezeki la TRA kufumuliwa? Na kuanzisha Kodi moja bandalini ambayo Ni 10% ya mzigo unaoagizwa..

Maana ya kupunguza Kodi Ni kuuza Sana kama tulikuwa tunatoza Kodi 50% ya bidhaa zinazoingia nchini ikashushwa mpaka 10% it means tutahakikisha tunaongeza uingizwaji wa mizigo kwa 40% ili kuendana na mapato Yale Yale bila kuwaumiza wafanyabiashara.

Ccm mnaona kwamba vitu havitekelezeki kwa sababu mliishi kwa uongo na upumbavu na ndio nyie mnaowafanya watanzania misukule .


Muache kuwa wapumbavu na kuita watu misukule wakati nyie ndio misukule.
Kamanda mbona povu jingi? Umekunywa Omo kwani?
 
Kampeni za uchaguzi zishaanza.

Wagombea wanakatiza nyika sehemu mbalimbali za nchi kuzinadi sera zao.

Wanatoa kila aina ya ahadi. ‘Mimi nitafanya hivi, nitafanya vile, nitafanya haya, nitafanya yale...’.

Sasa mimi ni mmoja wa watu ambao huwa sitegemei mwanasiasa au mtu mwingine kuniboreshea maisha yangu.

Naamini hilo jukumu linaanzia na kuishia kwangu mimi mwenyewe.

Nimemsikia mgombea wa CHADEMA akitoa ahadi tele. Ahadi zinazowapagawisha misukule wake.

Moja ya ahadi anazotoa ni ile ya bima ya afya kwa wote. Yaani kila mtu, kila raia, eti awe na bima ya afya.

Mimi si mtaalamu wa mambo ya bima wala mambo ya afya. Na wala sina ‘usomi’ wowote ule. Nimeishia kidato cha nne tu 🤣😉. Hivyo, huenda nikawa na uwezo mdogo wa kuelewa na kuchanganua mambo.

Katika ahadi zake hizo, sijasikia namna ambayo mgombea huyo wa CHADEMA ataweza kumpatia kila raia hiyo bima.

Hizo hela atazitoa wapi? Ataenda kuziomba kwa nchi hisani? Ataongeza viwango vya kodi ili kuongeza mapato yatayotumika kuileta hiyo bima? Au ataomba kwa Mungu atudondoshee hizo hela toka mbinguni?

Ahadi ni tele. Namna ya kuzifanikisha ahadi hizo, mpaka sasa ni sufuri!

Oh, na jingine ambalo sijamsikia kabisa akilizungumzia ni hili suala la Corona.

Kulikoni wewe mbeba maono wa CHADEMA? Ushakubali sasa kuwa Corona haipo? Au ushakubali kuwa ipo, lakini si hatari kama tulivyolishwa matango pori na Wazungu?

Manake we mwenyewe tokea urudi, zaidi ya mwezi sasa, huvai cha barakoa na wala hujitengi na jamii!

Unajichanganya kama ilivyo ada na sijakuona hata mara moja ukipiga chafya wala kukohoa.

Kwenye suala la Corona, hata kama huwezi kukiri kwa sauti, nahisi kimoyomoyo unakubaliana na jinsi Ngosha alivyoamua kukabiliana nalo😉.

Sisi akina Ngosha hatukutishika. Mfano mimi, hakuna hata siku moja niliyojifungia ndani. Sijawahi kuvaa barakoa. Na bado nipo nadunda nikibeba maboksi tena yale mazito kwelikweli ilhali kuna watu eti mpaka leo hii wamejifungia ndani kama mwali.

Mangosha wa ukweli hawawezi kujifungia ndani wakiogopa mafua na kikohozi💪🏿💪🏿.
Pumbafu
 
..Magufuli anasema tuzae elimu ni bure.

..What about afya?

..ana mpango gani ktk huduma za afya?



Rwanda: the beacon of Universal Health Coverage in Africa
Ya Magufuli siyajui. Si ajabu naye anaongea tu.

Ndo maana pale mwanzo nikasema mimi sitegemei mwanasiasa kuniboreshea maisha yangu....
 
Wamechagua garasa mara hii watazoa aibu, akili zao fupi wanafikiri mtu kukariri vifungu vya sheria ndio usomi.
 
Selikali ya CCM inadhurumu watanzania.
Bima ya Afya ninayo nakatwa kwenye mshara wangu. Lakini nikienda hospital Hakuna Dawa, hakuna vifaa tiba, hakuna Madaktari, glaves ni aibu sana kwa kweli. Unaelekezwa duka unalopaswa kwenda kununua hivyo fifaa na dawa.

Bila matibabu Bima ya Afya ni mzigo.

Tupatie ushuhuda ulikwenda hospitali ipi na ukaambiwa dawa hakuna wakati umelipia bima ya afya?

Mbona mimi napata huduma safi kabisa ya afya nikiumwa kwa kulipia bima ya afya kule NSSF?
 
Tupatie ushuhuda ulikwenda hospitali ipi na ukaambiwa dawa hakuna wakati umelipia bima ya afya?

Mbona mimi napata huduma safi kabisa ya afya nikiumwa kwa kulipia bima ya afya kule NSSF?


Rwanda: the beacon of Universal Health Coverage in Africa
 
Back
Top Bottom