Uchaguzi 2020 Mgombea Urais wa chama kimoja aweza muunga mkono mgombea urais wa chama kingine tofauti bila ridhaa ya Mkutano Mkuu wa chama chake?

Uchaguzi 2020 Mgombea Urais wa chama kimoja aweza muunga mkono mgombea urais wa chama kingine tofauti bila ridhaa ya Mkutano Mkuu wa chama chake?

Screenshot_20200922-063119.jpg

[/QUOTE]
 
Kachero ameachwa anamangamanga tu pasi zinapigwa juu kwa juu hana athari kama tule tupicha kwenye ganda la bazoka.

Kawepo kasiwepo,hakaathiri utamu wa peremende.😁!
 
Ukisikia udikteta ndio huu sasa.

Kwa mujibu wa katiba za Chadema na ACT - Wazalendo maamuzi yote makubwa na muhimu yanatolewa na vikao halali vya chama kama kamati kuu, halmashauri kuu, mkutano mkuu nk...
Dr. Bashiru hakukosea kusema. Mpaka uchaguzi uishe tutaona mengi.
 
Kwa sasa Africa iba dikteta mmoja tuu naye ni John
VIONGOZI wa vyama kuunga mkono wagombea wa vyama vingine bila ridhaa ya mkutano wa kamati kuu au mkutano mkuu sio udikteta?

Membe komaa ili uwaonyeshe kuwa demokrasia haaiimbwi tu komaa endelea na kampeni
na mgombea uraisi Zanzibar kupitia chadema komaa endelea na kampeni muwashikishe adabu kuwa demokrasia sio ya kuchezea

Askari wapeni ulizi wakiendelea na kazi zao ZA KUJINADI
 
Kuna maajabu yanayovunja katiba za vyama kwenye uchaguzi huu mkuu.

Tumeona Lisu Makamu mwenyekiti taifa wa CHADEMA na mgombea uraisi kupitia Chadema akitoa tamko kuwa anamuunga mkono Mgombea uraisi wa Zanzibar Maalim Seif wa Act wazalendo...
Saccos kubwa inaungana na saccos ndogo ndogo.
 
Hao watu wajanja, wamekwepa mitego ya msajili, najua unataka kuona anavifuta hivyo vyama, pole mtego wenu umeteguliwa.
Wewe si ndio ulikuwa unamuona Membe ni snitch na hafai kuungana na Lisu? Leo tena umebadili gia angani?

Sijui tindo anasemaje juu ya hili
 
VIONGOZI wa vyama kuunga mkono wagombea wa vyama vingine bila ridhaa ya mkutano wa kamati kuu au mkutano mkuu sio udikteta?....
Kwa sasa mnampenda tena Membe?
Lissu akili kubwa na kwa kulitambua hilo ndo maana mlitaka kumuua.
Kama mlidhani "kachero" atawakachero cdm na act, basi imebuma na badala yake ana "wakachero" nyie nyie maccm.

Lissu anawanyoosha sawa sawa, hata kama "kachero" atalazimisha kubaki jukwaani kugombea, halafu Zitto na Maalim kwa maana ya chama wasiwe upande wake, ataonekana kituko tu.
Kifupi ni kwamba "kachero" kujitoa na kumwachia Lissu siyo ombi bali ni amri ya chama chake. Hutaki unaacha.

Sent from my Infinix X606B using JamiiForums mobile app
 
Kuna maajabu yanayovunja katiba za vyama kwenye uchaguzi huu mkuu.

Tumeona Lisu Makamu mwenyekiti taifa wa CHADEMA na mgombea uraisi kupitia Chadema akitoa tamko kuwa anamuunga mkono Mgombea uraisi wa Zanzibar Maalim Seif wa Act wazalendo...
Mkuu kwanini unaona ya Act na Chadema tu,wakati Kuna ya CCM na TLP, UDP? au hivyo sio vyama vyasiasa?Umesahau kua 2015 mrema alienda adi kwenye jukwaa laCcm kule vunjo kumnadi na magufuli ili hali Chama chake kilisimamisha mgombea......;Msipaniki ndugu zangu pambaneni tu kwasera sio vioja Kama iv ni Aibu sana
 
Kuna maajabu yanayovunja katiba za vyama kwenye uchaguzi huu mkuu.

Tumeona Lisu Makamu mwenyekiti taifa wa CHADEMA na mgombea uraisi kupitia Chadema akitoa tamko kuwa anamuunga mkono Mgombea uraisi wa Zanzibar Maalim Seif wa Act wazalendo....
Ningekuona wa maana sana kama ungesema walau kifungu cha sheria kinachozuia hilo
 
M
Mkuu kwanini unaona ya Act na Chadema tu,wakati Kuna ya CCM na TLP,Udp?au hivyo sio vyama vyasiasa?Umesahau kua 2015 mrema alienda adi kwenye jukwaa laCcm kule vunjo kumnadi na magufuli ili hali Chama chake kilisimamisha mgombea......;Msipaniki ndugu zangu pambaneni tu kwasera sio vioja Kama iv ni Aibu sana
Ile ilikuwa Ni makosa mwaka huu TLP walikaa vikao vya kamati kuu na mkutano mkuu ukapitisha kuwa wamuunge mkono mgombea Uraisi wa CCM
 
Ningekuona wa maana sana kama ungesema walau kifungu cha sheria kinachozuia hilo
Kasome katiba za Chadema na ACT wazalendo kuhusu uteuzi wa wagombea Uraisi
 
Ukisikia udikteta ndio huu sasa.

Kwa mujibu wa katiba za Chadema na ACT - Wazalendo maamuzi yote makubwa na muhimu yanatolewa na vikao halali vya chama kama kamati kuu, halmashauri kuu, mkutano mkuu nk....
Bwashee, nyie katiba yenu inafuatwa? Mbona ya nchi hamuifuati? Kwanza mnajuaje hawana ridhaa ya wanachama? Au ndio mateke ya mwisho mnapiga kabla ya roho kuacha mwili?

Mtaumia sana mwaka huu. Mwambieni mgombea wenu atembee na picha za vielelezo vyenu: reli, ndege, flyover nk., akawaoneshe na watu wa Ngara na Karagwe.
 
Ile ilikuwa Ni makosa mwaka huu TLP walikaa vikao vya kamati kuu na mkutano mkuu ukapitisha kuwa wamuunge mkono mgombea Uraisi wa CCM
Asante kwajibu zuri....mbona hamkupga kelele wachukuliwe hatua?Vpi kuhusu Udp maendeleo maana juzi John Cheyo kampgia kampeni mgombea uraisi waCcm nawakati wao nao wamesimamisha mgombea
 
Ukisikia udikteta ndio huu sasa.

Kwa mujibu wa katiba za Chadema na ACT - Wazalendo maamuzi yote makubwa na muhimu yanatolewa na vikao halali vya chama kama kamati kuu, halmashauri kuu, mkutano mkuu nk...
Lyatonga Mrema aliwahi kumpigia kampeni mgombea wa mboga mboga huku chama chake kikiwa na mgombea lakini wewe takataka hukuona tatizo.

Si hivyo tu hata NEC ya mboga mboga nayo ikawa kimya bila kuona tatizo. Hakika wewe unafaa kupewa nishani kwa unafiki na ujinga usio na mfano. Hongera sana.
 
Waache wasalitiane CCM inapasua kati inasonga,mbona akuna jipya,washaungana mara nyingi tu lakini wanatoka patupu.
 
Back
Top Bottom