Sisi wakinga hatuogopi moto,Kwenye hizi biashara tuna maamuzi magumu sana ambayo wewe huwezi kuyafanya na hata ukiyafanya utakosa furaha maisha yako yote na unaweza ukaishia kuona maluwe luweMadhara ya kufanya hivyo ni nini?
Kwanini hawapo tayari? Mjadala wa nini? Madhara ya kuorodhesha maghala yenu ni yapi?
Mnaogopa moto?
TRA ni mamlaka inayokubali kutumika kifisadi kwaajiri ya kuwaridhisha na kuwapa hawa ma'CCM pesa za kirahisi rahisi.Hivi kweli hatuwezi kuja na mfumo mmoja tu TRA pale bandarini kuchukuwa kodi mara moja ili mzigo ukitoka basi watu wasisumbuane? mbona kwenye mafuta wameweza mzigo kwenye meli unakatwa kila kitu basi unaingia sokoni. Kuna nini hii kila siku kukimbizana wakati Tech imekuwa sana kuna njia za kuchukuwa mapato kwa njia ya kisasa tu badala ya haya mambo ya double taxation watu hakuna kuaminiana kwanini lakini? kodi kulipa ni haki basi tuweke mfumo utakaonekana ni wa haki.
Sababu za mgomo ni zipi?
Kama hawaitaki CCM nitajiunga nao mapema kuanzia kesho asubuhi, leo nimechelewa tu kwasababu sikuwa na taarifa mapema.
Kwa Taarifa yako BANDARINI ni mpakani, kwa hiyo huduma zote za kikodi zinazotolewa na TRA mipakani zinatolewa pia BandariniSio kila bidhaa inayouzwa inapitia bandarini, nyingine zinapitia mipakani ambapo Tanzania inazungukwa na nchi nyingi. Nyingine zinazalishwa ndani ya nchi
Hakuna kitu kama hicho. Siasa mbovu ndio zimetufikisha hapa.Ukiingiza siasa tayari uneshaharibu,
otherwise umetumwa kuuvuruga. haya ni madai ya Wafanyabiashara dhidi ya Serikali na pengine kwa chini chini kuna mkono wa watu wa CCM kuhakikisha Serikali inasikiliza madai yao tupunguze ujuaji
Kuua uchumi ili wale mabwanyenye wapate mkate wao wakila siku. Si unaona yalivyonenepeana hadi yanashindwa kupumua kama viboko.Sijawahi na pengine sitakuja kuwahi kuelewa hizi kodi zinavyokatwa
Mzigo ukifika bandarini unatokutana na tra
Mzigo huohuo ukifika dukani unakutana tena na tra
Sasa najiulizaga yule tra wa bandarini ni tofauti na huyu wa dukani????
Na km wote ni TRA, hizi kodi za mara mbilimbili zinalenga nini????
Kwan mipakani ndio hazichajiwi kodi mkuu au ulitaka kusemaje sijakupata vema?!Sio kila bidhaa inayouzwa inapitia bandarini, nyingine zinapitia mipakani ambapo Tanzania inazungukwa na nchi nyingi. Nyingine zinazalishwa ndani ya nchi
Hadi wanamkumbuka yule mzee masikini. Watu wanasema yule mzee alikuwa anachukia wafanyabiashara na matajiri ila hawajui kilichokuwa kinaendelea. Ama kweli wema hawana maisha.Kipindi cha JPM wafanyabiashara halali walikuwa wanasikilizwa vizuri na kero zao zinatatuliwa. Lakin sasa serikali ya KULA KWA UREFU WA KAMBA TRA wanakula kwa urefu wa kamba zao na hakuna anayejali sawa
Kama umeacha gap kwenye taarifa yako ulitegemea nini?!Ukiingiza siasa tayari uneshaharibu,
otherwise umetumwa kuuvuruga. haya ni madai ya Wafanyabiashara dhidi ya Serikali na pengine kwa chini chini kuna mkono wa watu wa CCM kuhakikisha Serikali inasikiliza madai yao tupunguze ujuaji
Ukikutana navyo na tuvitambulisho twao aisee huwa natamani nivikalibishe kahawa nivisute nivisemeeeeee hadi vijisikie aibu kuendelea na kazi. Yaani hivi vimisukule ni vipambe nuksi hadi basi.TRA ni taasisi yenye watu wapumbavu, wivu wivu wivu sumu kubwa iliyotamalaki kwa mioyo yao, tamaa tamaa hawana maadili wapumbavu hao.
Lakini hapa shida ni watunga sheria maana nimepitia haya mambo airport wao wanaingiza thamani ya mzigo system inatoa angalizo la gharama za kodi ambayo kwa kweli Tanzania wana kodi kubwa sana sasa shida hapa ni kwenye makadirio sababu ni maamuzi ya mtu wa TRA japo kuna wakati wanakusaidia maana wanakuuliza tu gharama bila wao kujiridhisha ila pia wanaweza kuweka thamani juu na ukaumia shida kodi nchi hii ni kubwa sana tena sana.TRA ni mamlaka inayokubali kutumika kifisadi kwaajiri ya kuwaridhisha na kuwapa hawa ma'CCM pesa za kirahisi rahisi.
Ukijaribu kutazama mfumo wa kodi umekaa kidalali sana. Kuanzia kutax magari used yanayoingia kutoka Japan, mizigo ya viwandani kutoka China etc.
Unanunua gari milioni 4 kodi milioni 9, na hakuna raia ambaye ameshitaki mahakamani hadi sasa. Hawa nguruwe ndio wanaochochea mfumuko wa bei na kuharibu ukuaji wa SME's halafu ukiyakuta ya kwenye mijadala ya kitaifa yanavyojinasibu kuhusu uzalendo na kujitoa kama taifa unagundua hawa wanaojiita viongozi hakuna kitu ni vishoka wa mataifa ya magharibi hakuna mwenye utimamu wa kusimamia uzalendo hata m'moja kudadadeki zao.
DuuWana bahati wangefanya huo mgomo kipindi cha mwenda zake, sasa hivi tungekua tuna hesabu maiti za viongozi wa hilo soko.
πππππππππMtanikumbuka
Mfumo wa kulipa kodi ni wa kiwendawazimu ila huwezi lipa kodi kwa kutumia bandari na mipaka tu. Kwanza tunazungukwa na nchi nane na mipaka yote ina mianya ya magendo na kupita bila kukaguliwa. Na wakati huo kuna uzalishaji unafanyika ndani na mnyororo wa thamani unaongezekaMimi sijaongelea bandarini tu nimesema TRA kwani unaweza kupita mpakani, bandarini au airport bila uwepo wa TRA? wako kila entry ya nchi waweke mfumo wa kisasa kukusanya kodi sio mambo ya kuviziana madukani mambo ya kishamba sana.
Watu wanakwepa kodi kwa sababu kodi zenyewe zina utata na matumizi yake pia ni mabaya .Sababu za mgomo ni zipi?
Kama hawaitaki CCM nitajiunga nao mapema kuanzia kesho asubuhi, leo nimechelewa tu kwasababu sikuwa na taarifa mapema.
Kuna ubaya gani TRA kuwataka muorodheshe store zenu mnazohifadhia mali, wanataka wazifahamu ili wakazikague, kwasababu huko Kariakoo kuna ukwepaji mkubwa sana wa kodi.
Anyway, niwapongeze hao wafanyabiashara kwa uthubutu, wamejaribu.