Unajua kwa siku TRA wanaingiza kiasi gani kwa biashara ya Kariakoo pekee.
Unajua kwanini Kariakoo ni mkoa wa kikodi?
Unajua kariakoo inahudumia Tanzania kwa ukubwa gani?
Unajua Kariakoo inahudumia nchi ngapi zisizo na bandari?
Umemsikia Mkuu wa mkoa alichokisema? Amesema Tanzania ni kubwa sana. Yale yale niliyoandika mimi. Kariakoo ni ndogo sana ukilinganisha na ukubwa wa Tanzania.

Sasa fungeni maduka yote Kariakoo kwa wiki moja tu, halafu tuone nane atakayepata hasara; serikali au mfanya biashara? Tuone nani atadaiwa kodi ya frame mwisho wa mwezi.

Mambo mengine yanahitaji akili na siyo mihemuko. Mfanyabiashara mwenye akili hafungi duka sababu anajua at the end of the day ni yeye atapata hasara.
 
Katika migomo kama hii lazima kwanza ukae utafakari Kwa kina wewe mwenyewe binafsi kwanza kabla ya kuanza kugoma, tunagoma Kwa kufuata na kuingia kwenye mfumo wetu au tunagoma Kwa kufuata na kuingia kwenye mifumo ya watu, hivyo mgomaji lazima awe na akili ya kutafakari sawasawa.
 
Unakuta ni uvccm na mwalimu huko nanjilinji unaona mfanyabiashara mwenye mtaji wa milioni 500 wengine bilioni wamefunga biashara zao hawana akili.

paragraph ya mwisho imeonyesha either ni chawa, uvccm au mwanafunzi.
 
WAkati muafaka wa kulipa kodi, asiyetaka aachie fremu wamachinga watauza.
 
Soma hayo madai namba 12 hayafanani na ulichoandika.
 
Safi sio kodi zinainiwa tu acha wajue
Afunaliteasisi apewe cheti ya uninja manake hajulikani selikal imepigwa pazito sana
 
Ukwepaji wa kodi ni mkubwa sana. TRA wanachofanya ni kukaza kwenye suala la utoaji wa riskti za EFD na returns ambazo wengi wanafoji na kupeleka mahesabu ya uongo na kukwepa kodi kwa kiwango cha kutisha sana.

TRA wanafanya Kazi yao kwa usahihi sana na kufuatilia receipts zote za wanunuzi wa mizigo madukani kisha wanakwenda kwenye duka husika na ndiko wanakuta uongo na ukwepaji wa kodi na udanganyifu.

Sasa hapo TRA kosa lao ni nini? Yaani waache watu wakwepe kodi? Kwanza haya makosa ni uhujumu uchumi na kwa nini watu hawa wanaachwa?

Serikali ifike mahali anayekataa kufungua duka futeni leseni yake akafanye kazi nyingine lakini hatuwezi kuwa na taifa la wakwepa kodi.

Huu upuuzi hawakuwa wanaweza kuufanya wakati wa Magufuli kwa sababu hakukuwa na mchezo kwenye suala la kulipa kodi. Sasa hivi hawa watu wameleta mazoea sana na serikali na haya ndiyo madhara yake sasa.
 
Kodi si ombi. Kama umechoka biashara achia wengine wafanye hizo biashara. Mazingira Ni wezeshi hapo kariakoo. Acheni kusumbua Viongozi
Njoo nikuachie kama unaona ni vyepesi sana kufanya biashara Kariakoo.

Mnajiongelea tu na visuruali vyenu vya kubana na tie shingoni mnajikuta kila kitu mnakijua.
 
Wewe ndiye ukasome ulichoandika pale juu kama kinaendana na dai #12 kwenye malalamiko ya wafanyabiashara View attachment 3024874
Huo msururu wa kodi mnaotaka ufutwe mnataka kufanya biashara bila kulipa kodi? Kuna kundi kubwa la walipa kodi mfano watumishi wa umma na sekta binafsi kila mwezi wanakatwa PAYE wafanyabisha wao ni nani hadi wapunguziwe kodi zote hizo ? Na bado ukwepaji kodi ni mkubwa tu tunajua risiti hazitolewi na pia kufanyiwa makadirio madogo ya hesabu za biashara mnadhani serikali haijui?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…