Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Mgomo unaoendelea Kariakoo uwe wake up call kwa serikali kuacha kutumia vyombo vya dola kuendesha biashara za raia. Tutumie wataalam watuambie tatizo lilipo na tulipatie ufumbuzi.
Siku dola ikipewa jukumu la kuimarisha usalama biashara zifanyike usiku na mchana nchi itapiga hatua. Lakini tukiendelea kutumia dola kukusanya kodi, kutumia dola kulazimisha wafanya biashara wakalale, kutumia dola kukusanya mapato tutaua uchumi.
Wageni kukimbia Kariakoo ni kutokana na matumizi makubwa ya dola katika kuratibu biashara. Hakuna mfanyabisahara serious atakuja kwenye soko ambalo askari wamejazana kila kona kuanzia dukani hadi barabarani. Zambia wameondoa dola kwenye biashara sasa hivi wanafanya vyema.
Hii ni nchi yenye amani tuachane na matumizi ya dola, tuachane na fikra mgando kwamba watu wote wanatakiwa kulala usiku, tuachane na fikra kwamba tunaibiwa na badala yake tujiulize nini kinasababisha wafanya biashara wasiwe waaminifu?
Pia soma:
- News Alert: - Mgomo mkubwa Soko la Kariakoo: Maduka yamefungwa, Mei 15, 2023