MGOMO: Wafanyabiashara Kariakoo kufunga biashara zao kuanzia 24/6/2024 mpaka changamoto zao zitakapotatuliwa'

Kabisa naungana nao maana kinachofanyika saizi sio kodi tena bali ni ufisadi.

Hadi msajili line aliyeweka bango nje la tigo siku hizi wamekuja na sheria mpya inaitwa kodi ya bango ikimtaka huyo mtu awe analipia hilo bango.

Kuna mtu jana katozwa na Manispaa 80K kwa ajili ya bango la saluni "hair cutting"

Bado hapo hujazungumzia Service Levy, mawakala wa miamala wanalalamika kamisheni zao zinakatwa na mwisho wa mwezi TRA wanachukua 10%

Lakini bado wanalazimika kuwa na lesenj ku run biashara hiyo yani wanakatwa kodi zaidi ya mara mbili kwenye huduma moja.

Huu ni ukandamizaji, nchi imeingia gizani viongozi wanajali matumbo yao mtu wa chini wala hawamuangalii.

Naungana na wafanyabishara wa Kariakoo kwenye hili.
 
Low Bettry, think wisely
 
Wewe ni kunguni...udini umeingaaje hepo fine ya mil 15
wewe ni kunguni..kila saa unawaza udini...fine ya mil 15 ni ndogo...mwigulu must go...ni mpumbavu
 
Mkuu kama hujui kitu ni Bora ukae kimya Tu, nipo kariakoo mwaka wa 11 huu najua mambo mengi Sana ya wafanyabiashara.. kumbuka wafanyabiashara wataowekeza ubungo ndiyo haohao wapo kariakoo, ndiyo maana kariakoo inaitwa mkoa wa kikodi ( eneo ambalo linachangia revenue kubwa serikalini kama hadhi ya mkoa)

Waulize TRA kariakoo ikifungwa Kwa siku moja inakuaje!!!
 
Kwahiyo Wapemba, Wamanyema na Wasomali waliojazana Kariakoo hawawapendi viongozi Waislamu?🐼
 
Changamoto zenu mbona hamjaainisha
 
Tatizo ni mshikamano mkuu. Wabongo tunaweza kuja na azimio moja na kulitekeleza wote kwa wakati huo huo?
 
Wewe mdini ama chawa mkubwa wa mama.

Hauwezi kuongelea logic zako mpaka uambatanishe na hayo matakataka?

Ukristu ama uislam wa kiongozi wa nchi unakuletea sukari mezani wewe?

Kuwa biased na dini ama madhehebu kunatia upofu raia kutokujua haki zetu na kupelekea kunyanyaswa na hizi tawala dhalimu.
 
Wewe hujui usemalo! Wafanya biashara waliokuwa hawafanyi magumashi kipindi ya Magufuli walifanya kazi vizuri sana!
Saizi Chini ya Samia ni TRA kuomba rusha na kufanya gharama za kuendesha biashara kuongezeka!
Samia na serkali yake hawatabiriki leo hiki kesho kile!
 
Kuporwa pesa kwenye akaunti baada ya kusingiziwa kudaiwa kodi miaka mitano iliyopita ndiyo kulikuwa kuzuri! Acha kuongea uongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…