MGOMO: Wafanyabiashara Kariakoo kufunga biashara zao kuanzia 24/6/2024 mpaka changamoto zao zitakapotatuliwa'

MGOMO: Wafanyabiashara Kariakoo kufunga biashara zao kuanzia 24/6/2024 mpaka changamoto zao zitakapotatuliwa'

Wafanyabiashara wote wa viunga vya Kariakoo mnatakiwa kufunga biashara zenu zote ikiwemo maduka yenu, ofisi zetu na chochote unachokifanya kuanzia Jumatatu ya Juni 24, 2024 bila ukomo hadi pale changamoto zetu zote za kibiashara zitakapoweza kutatuliwa.

Mikoa ya Mbeya, Iringa, Mwanza, Arusha, Ruvuma, Kagera na Rukwa mtaanza kufunga biashara zetu kuanzia siku ya Jumanne ya Juni 25, 2024 bila ukomo.

Kuanzia siku ya Jumatano ya Juni 26, 2024 wafanyabiashara wote nchini tutaungana kufunga biashara zetu hadi pale changamoto zetu zote zitakapopata ufumbuzi wa kudumu.

Kutakuwa na kikosi kazi cha kupitia ili kukagua ofisi au biashara ambazo hazijafungwa ili kuhakikisha wote tunaungana kupambana na udhalimu huu wa kodi kandamizi.

----
Pia soma
Tetesi: - Wafanyabiashara Kariakoo kugoma muda wowote kutokana na madai yao kupuuzwa

View attachment 3023083
Kumekucha!
 
Mpaji,

Huwa ninafurahi sana mtu anakuambia hawana ubavu sababu biashara zao ni za mikopo. Na bado kuna mwingine atataka kuifananisha na ubungo.

Hawaelewi kwamba kariakoo ndio soko kubwa, hawataki kuelewa kwamba kariakoo ina athiri mzunguko wa fedha. Haielewi kwamba kariakoo inaweza ikasababisha athari za mikataba ya kimataifa ya kikodi.

Hawataki kusikiliza wanaendekeza siasa
Uzuri viongozi wetu wanajua nguvu ya soko la kariakoo, kariakoo inahudumia masoko ya ndani na nje kama Congo na Malawi
 
Huu ni mkakati mahususi na umekuwa ukifanyika kila wakati kiongozi wa nchi anapokuwa Muislamu ili kuhakikisha utawala huo unakosa utulivu na kuleta chuki baina ya wananchi na utawala uliopo madarakani.
Wakati wa utawala wa Magufuli wafanyabiashara walionewa sana ikiwa ni pamoja kufunguliwa kesi za uhujumu uchumi na kuporwa pesa kwenye akaunti zao benki lakini hatukushuhudia hata kunguni kuandamana au kugoma,
Huu ni unafiki na tukae tukijua kwa unafiki tulionao Watanzania hatutofanikiwa kujinasua kutoka kwenye makucha ya utawala dhalimu wa ccm.
Ili baki kidogo tuu ujiite nguruwe

Sema mwishoni kwel sisi wanafki Sana.
 
Huu ni mkakati mahususi na umekuwa ukifanyika kila wakati kiongozi wa nchi anapokuwa Muislamu ili kuhakikisha utawala huo unakosa utulivu na kuleta chuki baina ya wananchi na utawala uliopo madarakani.
Wakati wa utawala wa Magufuli wafanyabiashara walionewa sana ikiwa ni pamoja kufunguliwa kesi za uhujumu uchumi na kuporwa pesa kwenye akaunti zao benki lakini hatukushuhudia hata kunguni kuandamana au kugoma,
Huu ni unafiki na tukae tukijua kwa unafiki tulionao Watanzania hatutofanikiwa kujinasua kutoka kwenye makucha ya utawala dhalimu wa ccm.
Mawazo ya kijinga haya
 
Wajinga hao, ngoja soko la Ubungo likamilike, mchina analeta mzigo moja kwa moja, wafanyabiashara wanachukua bila udalali. Ni ujinga wa watu wa kariakoo kuwashawishi wafanyabiashara wa kigeni wasichukue risiti, baadae wakitoka nje ya kariakoo wanakamatwa, wakikamatwa hao wafanyabiashara wanawaruka. Pumbafu sana, na ndio inafanya wageni wakimbie

Serikali itengeneze karikoo zaidi ya nne hapo jijini, hii itaondoa hali ya monopoly kama ilivyo kwenye sukari.
Umeongea madudu tu Zambia,Zimbabwe,SA au Botswana tunanunua mizigo hatukamatwi kama wanavyokamatwa kariakoo ni vile hampo kwenye biashara ndio maana unaweza kuongea chochote hapa Jozi unaweza kushusha kontena hautapata usumbufu kama kutuma box tatu Tanzania...maana hakuna kontena au mzigo utafika bila kulipiwa ni vile Watanzania wengi wamedumaa wanakua na maamuzi ya kuua Biashara kwa Nchi iliyo na Bandari ila Watanzania wanafata mizigo Uganda na Kenya kama sio Ujinga huo ni nini?waweke mazingira mazuri kwa Wafanyabiashara na wanunuzi ili watu wapate bidhaa bora na kwa bei nafuu..
 
Huu ni mkakati mahususi na umekuwa ukifanyika kila wakati kiongozi wa nchi anapokuwa Muislamu ili kuhakikisha utawala huo unakosa utulivu na kuleta chuki baina ya wananchi na utawala uliopo madarakani.
Wakati wa utawala wa Magufuli wafanyabiashara walionewa sana ikiwa ni pamoja kufunguliwa kesi za uhujumu uchumi na kuporwa pesa kwenye akaunti zao benki lakini hatukushuhudia hata kunguni kuandamana au kugoma,
Huu ni unafiki na tukae tukijua kwa unafiki tulionao Watanzania hatutofanikiwa kujinasua kutoka kwenye makucha ya utawala dhalimu wa ccm.
lichawa likubwa hili
#kataaChawa
#KataaUozo2025
 
Wewe mdini ama chawa mkubwa wa mama.

Hauwezi kuongelea logic zako mpaka uambatanishe na hayo matakataka?

Ukristu ama uislam wa kiongozi wa nchi unakuletea sukari mezani wewe?

Kuwa biased na dini ama madhehebu kunatia upofu raia kutokujua haki zetu na kupelekea kunyanyaswa na hizi tawala dhalimu.
Hii iwekwe kwenye mlango wa kila nyumba Tanganyika, mjini na vijijini.
 
Wewe kijana acha ujinga! Nitajie nani aliyekuwa na biashara halali aliporwa hela zake?
Waulize wafanyabiashara Kariakoo kama walikuwa wanaasumbuliwa kama wanavyosumbuliqa saizi!
Magufuli wewe kama ni muuza vitu vya michongo hulipi kodi lazima serkali ikuulize hela hiyo umepata wapi na kwa biashara gani na kodi ya sekali ni ipi!,Hilo lipp dunia nzima sio kipindi cha Magufuli tu!
Samia ameshafeli na ataendelea kufeli maana kawaachia TRA kazi ya kukusanya hela kwa rushwa na usumbufu!
Kama ndivyo wananchi wote tunawaza basi wala sio kosa la Rais Samia peke yake, ni letu sote.

Serikali ni Taasisi na utendaji na utimizaji wa wajibu ni jukumu la wahusika wote waliopo serikalini ndani ya hiyo/hizo Taasisi zake.

Ni kipindi cha Hayati Magufuli watu walilalamika pia kuhusu “one man show” iliyokua inaendelea.

Bahati mbaya sana haya yanayoendelea sasa yanathibitisha hulka ya binaadam anapopewa nafasi na Uhuru mpaka wa nafsi.
 
Haya mambo ya migomo haya bna jau sana, sometimes wanapambania kisichokuathiri ila inabidi uunge mkono, maana ukiwa mkaidi hawachelewi kukufanyia zengwe.

Hili ni pigo kwa wenye mikopo.
 
Back
Top Bottom