MGOMO: Wafanyabiashara Kariakoo kufunga biashara zao kuanzia 24/6/2024 mpaka changamoto zao zitakapotatuliwa'

Kuna wakati nilikuwa nanunua mizigo cash and carry na jumbo stores, ukija beitbridge unajaza fomu ya vat refund, na utapata, huku kwetu kariakoo anakatwa mzambia hana ririti ya vat ilhali tra hawana taratibu za kurudisha vat.
Mpaka sasa hivi ukinunua kitu chochote hapa kama unapanda ndege ukionyesha vitu na risiti zako pale Airport unapewa kadi ya Bank baada ya siku kadhaa unakutana na hela Tanzania unatoa bank yeyote ukinunua hivyo vitu unavyosema au gari ni mpaka uje ulipe kodi Tanzania unawatumia copy ya passport yako na malipo ya kitu ulichonunua ukirudi unapewa 15% ya VAT yako yote na inakua ni nyingi Watanzania hakuna kitu tunajua kuhusu VAT waliwahi kuweka VAT kwenye transit goods mpaka jamaa wakawa wanasema ina maana Tanzania hakuna hata vyuo Vikuu wawashauri hao wasiojua kitu Wazambia na na Wakongo wakakimbilia SA mpaka tulipotoa na kuwafata tena kuwaambia waje Ujinga ndio umejaa kwenye vichwa vyao yaani siku wakipata akili hili swala la Risiti wataachana nalo na pesa nyingi sana watapata ni vile Wamekaririshwa..
 
Lipa kodi ndugu ya biashara unayo fanya kwa mujibu wa sheria.

Uwezi jiamkia tu utaki lipa kodi kisa utaki kujiemelisha wala kuelewa elimu unayopewa kila siku.

TRA wana account yao rasmi ya kutoa elimu ya kodi JF amtaki kuitumia kupewa elimu.

Kuhamasisha watu kutolipa kodi ni uhaini unaostahili hatua za kisheria
(binafsi muhusika ningempeleka jela).

Kutotaka kujielimisha kuhusu mambo ya kodi aina maana ubembelezwe sheria ikufuata mkondo wake.

Lipa kodi kwa hiari, acha visingizio.
 
Ila tuongee ukweli.kuna sehemu wanakwepa kodi kushinda kariakoo?unanunua kitu cha million 3 wanakupa rising ya laki 3.aladu bado wanalalamika. Mnawalea sana.
Hivi umekuja ofisin....nakuuzia bidhaa ya laki tatu...nakuambia kabisaa hii bidhaa ya laki tatu utalipia laki tatu na themanini na risiti yako itaandikwa hivyo hivyo...lakin kurahisisha biashara yangu hii bidhaa ya laki tatu nitakuuzia laki tatu tu na risiti itatoka ya laki mbili na themanini...utachagua kipi...ninyi wateja hamjui wafanya biashara wanakumbana na mikiki mikiki mingapi mpaka bidhaa inakufikia wewe final consumer...umewahi waza TRA kabla hata hujaanza operate biashara yako lakin wenyewe washakupigia makadirio ya kodi? Yan hata mlaji wa bidhaa zako humjui lakin wenyewe washakufanyia estimations....ushawah jiuliza kuwa kwa kawaida kodi hukatwa baada ya faida? Sasa ndio unaanza biashara hayo makadirio wanayo weka yanatoka kwenye faida ipi wakati ndio kwanza unaanza biashara?? Tz ndio sehemu ambayo ukianza kukua tu kibiashara utawakuta hawa wehu hawa hapa..,utafikiri mitaji walikutafutia...sipingi kulipa kodi lakin kuna namna kodi zinatumika vibaya pia namna ya utekelezaji wa kukusanya kodi utaratibu wake sio mzuri...unakuta officer wa TRA anataka aonekane boss yani aogopwe...hyo mind set vijana wameiweka sana kichwani...hata hiz service levy ni za kaz gan? Hivi kweli tumeshindwa buni kabisa vyanzo vingine vya mapato?? Kweli mtu anaweka bango la biashara kuchochea mzunguko wake...bado tna wanakuja kutoza ushuru wa bango ni akil au matope..?
 
Huu ni mkakati mahususi na umekuwa ukifanyika kila wakati kiongozi wa nchi anapokuwa Muislamu ili kuhakikisha utawala huo unakosa utulivu na kuleta chuki baina ya wananchi na utawala uliopo madarakani.
Wakati wa utawala wa Magufuli wafanyabiashara walionewa sana ikiwa ni pamoja kufunguliwa kesi za uhujumu uchumi na kuporwa pesa kwenye akaunti zao benki lakini hatukushuhudia hata kunguni kuandamana au kugoma,
Huu ni unafiki na tukae tukijua kwa unafiki tulionao Watanzania hatutofanikiwa kujinasua kutoka kwenye makucha ya utawala dhalimu wa ccm.
Mmeanza kuleta habari za Udini hapa
Nenda kwenye hayo maandamano uone hata masheikh wapo,,,, Mama nchi immemshinda full stop
Magufuli alikuwa chuma mtetezi wa wanyonge mazuri yake ni meengi sanaaaa
 
Sasa hivi wana kitengo cha DRD kodi za ndani wao watu wakiingiza magari wanafungia Tin hasa za kutoka SA eti wanataka kujua hela kapata wapi ya kununua gari mbona hafanyi biashara Tanzania yaani hawataki watu warudi na Mali Tanzania wao muda wote ni kutengeneza vitu vya kupata Rushwa tu Nchi ya watu masikini na fikra na mawazo ya kimasikini tu...
 
Lipa kodi ndugu ya biashara unayo fanya kwa mujibu wa sheria.

Uwezi jiamkia tu utaki lipa kodi kisa utaki kujiemelisha wala kuelewa elimu unayopewa kila siku.

TRA wana account yao rasmi ya kutoa elimu ya kodi JF amtaki kuitumia kupewa elimu.

Kuhamasisha watu kutolipa kodi ni uhaini unaostahili hatua za kisheria
(binafsi muhusika ningempeleka jela).

Kutotaka kujielimisha kuhusu mambo ya kodi aina maana ubembelezwe sheria ikufuata mkondo wake.

Lipa kodi kwa hiari, acha visingizio.
Ndio maana hata umeya walikutoa...hakuna aliye kataa kulipa kodi...ww mwenyewe tukiamua kuanika madudu yako hapa hili jukwaa utalikimbia..
 
Wafanyabiashara wote wa viunga vya Kariakoo mnatakiwa kufunga biashara zenu zote ikiwemo maduka yenu, ofisi zetu na chochote unachokifanya kuanzia Jumatatu ya Juni 24, 2024 bila ukomo hadi pale changamoto zetu zote za kibiashara zitakapoweza kutatuliwa.

Mikoa ya Mbeya, Iringa, Mwanza, Arusha, Ruvuma, Kagera na Rukwa mtaanza kufunga biashara zetu kuanzia siku ya Jumanne ya Juni 25, 2024 bila ukomo.

Kuanzia siku ya Jumatano ya Juni 26, 2024 wafanyabiashara wote nchini tutaungana kufunga biashara zetu hadi pale changamoto zetu zote zitakapopata ufumbuzi wa kudumu.

Kutakuwa na kikosi kazi cha kupitia ili kukagua ofisi au biashara ambazo hazijafungwa ili kuhakikisha wote tunaungana kupambana na udhalimu huu wa kodi kandamizi.

----
Pia soma
Tetesi: - Wafanyabiashara Kariakoo kugoma muda wowote kutokana na madai yao kupuuzwa

View attachment 3023083
Tungemaliza la sukari kwanza.
 
Hivi umekuja ofisin....nakuuzia bidhaa ya laki tatu...nakuambia kabisaa hii bidhaa ya laki tatu utalipia laki tatu na themanini na risiti yako itaandikwa hivyo hivyo...lakin kurahisisha biashara yangu hii bidhaa ya laki tatu nitakuuzia laki tatu tu na risiti itatoka ya laki mbili na themanini...utachagua kipi...ninyi wateja hamjui wafanya biashara wanakumbana na mikiki mikiki mingapi mpaka bidhaa inakufikia wewe final consumer...umewahi waza TRA kabla hata hujaanza operate biashara yako lakin wenyewe washakupigia makadirio ya kodi? Yan hata mlaji wa bidhaa zako humjui lakin wenyewe washakufanyia estimations....ushawah jiuliza kuwa kwa kawaida kodi hukatwa baada ya faida? Sasa ndio unaanza biashara hayo makadirio wanayo weka yanatoka kwenye faida ipi wakati ndio kwanza unaanza biashara?? Tz ndio sehemu ambayo ukianza kukua tu kibiashara utawakuta hawa wehu hawa hapa..,utafikiri mitaji walikutafutia...sipingi kulipa kodi lakin kuna namna kodi zinatumika vibaya pia namna ya utekelezaji wa kukusanya kodi utaratibu wake sio mzuri...unakuta officer wa TRA anataka aonekane boss yani aogopwe...hyo mind set vijana wameiweka sana kichwani...hata hiz service levy ni za kaz gan? Hivi kweli tumeshindwa buni kabisa vyanzo vingine vya mapato?? Kweli mtu anaweka bango la biashara kuchochea mzunguko wake...bado tna wanakuja kutoza ushuru wa bango ni akil au matope..?
Kaka mbona wafanyabiashara wa rangi nyeupe wanatoa risiti halali. Nenda kanda pale kwa msomali. Shida ipo kwa sisis ngozi nyeusi. Tunapenda janja janja. Wenzenu wanatoa risiti nzima nzima kwanini ninyi hamtoi. Haya sawa mnatoa risiti pungufu ba bado mnalalamika kodi kubwa🤣🤣🤣.yaani mtu kanunua kitu cha milioni 3 umempa risiti ya laki 3.lakini bado hapo hapo unaona hyo laki 3 kodi yake kubwa.badilikeni
 
Huu ni mkakati mahususi na umekuwa ukifanyika kila wakati kiongozi wa nchi anapokuwa Muislamu ili kuhakikisha utawala huo unakosa utulivu na kuleta chuki baina ya wananchi na utawala uliopo madarakani.
Wakati wa utawala wa Magufuli wafanyabiashara walionewa sana ikiwa ni pamoja kufunguliwa kesi za uhujumu uchumi na kuporwa pesa kwenye akaunti zao benki lakini hatukushuhudia hata kunguni kuandamana au kugoma,
Huu ni unafiki na tukae tukijua kwa unafiki tulionao Watanzania hatutofanikiwa kujinasua k
Hamna uhusiano na uislamu hapo,

Tusiongee sana hatuna pesa ya mawakili, ila uislamu unataka haki na sio uchawa na wala usizungumze jambo usilolijua
 
Kaka mbona wafanyabiashara wa rangi nyeupe wanatoa risiti halali. Nenda kanda pale kwa msomali. Shida ipo kwa sisis ngozi nyeusi. Tunapenda janja janja. Wenzenu wanatoa risiti nzima nzima kwanini ninyi hamtoi. Haya sawa mnatoa risiti pungufu ba bado mnalalamika kodi kubwa🤣🤣🤣.yaani mtu kanunua kitu cha milioni 3 umempa risiti ya laki 3.lakini bado hapo hapo unaona hyo laki 3 kodi yake kubwa.badilikeni
Tatizo ww una deal na effects..inakubidi utafute chanzo...then ndio uje hapa...kodi zinalipwa haswa...
 
Kaka kwani kile kinachokatwa kwenye risiti si ndicho kinajumuishwa chote.alafu mwisho wa mwaka wa kodi ndo unakwenda kulipa?
sasa ninyi mlikuwa mnataka mkalipe bei gani. mimi yule msomali namsifu sana. Nunua mzigo wa bei yoyote ile risiti yako unaipata vile vile.saaa nenda kwa kitenge au machupa. Uone balaa. Sasa uwa najiuliza yule msomali anapata vipi kodi na hawa wengine wanakosa vipi kodi.
 
Tungemaliza la sukari kwanza.
Mkuu kwa sukari bashe mtamuonea tuu...
Ipo hivi mahitaji ya ndani ya sukari ni Tani 420,000...na uwezo wa viwanda vya ndani uzalishaji wake ni tan 280,000 hapa kuna ombwe la tani 140,000 za sukari ambayo itabidi iagizwe nje ili kukidhi mahitaji...

Mwaka jana kukawa na uhaba wa sukari sababu wazalishaji wa ndan au viwanda vya ndani kudai mashamba yalijaa maji...hii ilipelekea uhaba wa sukari hivyo sukari ikaanza panda bei...baadhi ya maeneo ilifika mpaka kilo sh 7,000...waziri bashe akatoa vibali kwa viwanda vya ndani kuagiza sukari nje ili kuzuia mfumuko wa bei ya sukari.,

Sasa wafanya biashara wa ndani kwa njama zao hawakutii agizo kupelekea sukari kupanda zaidi...Bashe alivyo ona agizo halijafanyika akawafutia vibali hivi viwanda vya ndani .,

Maamuzi aliyo chukua ni kuwapa vibali wafanya biashara wenye uwezo wa kuagiza sukari nje ili tu kuzuia mfumuko wa bei ya sukari na hapa ndio tunaona mpaka makampuni ya simu yalipewa tender ya kuagiza sukar nje na bei tuliona zilirudi mahali pake...ingawa ni nje ya utaratibu lakini ilitibu tatizo...

Kama wewe ungekuwa bashe ungefanyaje??? Binafsi nampa maua yake...sijajua tatizo lake na mpina lakini kwenye hili mnyonge mnyongeni haki yake apewe..
 
Ndio maana hata umeya walikutoa...hakuna aliye kataa kulipa kodi...ww mwenyewe tukiamua kuanika madudu yako hapa hili jukwaa utalikimbia..
Ujasema shida ya kodi hiko wapi.

Hao wahuni wanao waamasisha kutolipa kodi wanavunja sheria (mshukuru huruma wa bi-tozo).

Vinginevyo kwa mamlaka ya TRA kupitia mamlaka ya ‘tax administration’ watu kama nyie msiotaka kujifunza hesabu za biashara zenu, kwa Sasa mshukuru huruma wa raisi.

Lipa kodi hesabu żako za hovyo bila ya kuzingatia finance bills (ya mwaka husika), employment laws na business rates za mahala ulipo hazina uhusiano na sera za nchi. Ni jukumu lako kuzielewa vinginevyo. .

Bila ya maelezo shida yako ni nini? serikari itakuchukulia wewe ni mkwepa kodi. Bahati nzuri hii ni serikali yakulea na kukuza biashara sema unakwazika vipi upewe elimu.

Serikali haipo kunyanyasa wafanya biashara ilal ipo kuwakuza wafanyabiashara hilo ndio lengo lake.

Njia moja wapo ya kukuza biashara ni kuwapa elimu ya kodi na namna ya kupiga hesabu sahihi za kibiashara sio mambo yenu ya kubuni, na kujadiliana based on simple costs. Baada ya hapo mnaanza malalamiko.

Kuhamasisha watu kutokulipa kodi kwa sababu za upumbavu zilizopo kwenye upumbavu wa vichwa vya viongozi weny sio suluhisho, Wakati TRA ipo mpaka ndani ya JF kwa sababu kujibu hoja tu.

Baada ya kukupa ukweli wa kodi kama unamaswali leta ujibiwe.

Sasa nakukaribisha kuuelezea umma jinsi unavyonijua, usiache kitu, Iła mimi sijui utani na wala sipendi mazoea kwa wanaonijua vizuri.

Lipa kodi, uwezi kuwa kila siku unapewa elimu kodi ni sheria ambayo utaki kuelewa halafu unalalamikia ignorance yako.

Kama ujifunzi kwa maneno, utajifunza kwa matendo (yote kwa ni kwa mujibu wa sheria hakuna uonevu).
 
Wajinga hao, ngoja soko la Ubungo likamilike, mchina analeta mzigo moja kwa moja, wafanyabiashara wanachukua bila udalali. Ni ujinga wa watu wa kariakoo kuwashawishi wafanyabiashara wa kigeni wasichukue risiti, baadae wakitoka nje ya kariakoo wanakamatwa, wakikamatwa hao wafanyabiashara wanawaruka. Pumbafu sana, na ndio inafanya wageni wakimbie

Serikali itengeneze karikoo zaidi ya nne hapo jijini, hii itaondoa hali ya monopoly kama ilivyo kwenye sukari.
Ndiyo maana watu wanasema CCM na mashabiki wake ni watu wajinga kupindukia. Wewe na wajinga wenzako wa CCM mnaona solution ni kumleta mchina auze mizigo moja kwa moja. Kweli madaraka yamewapofusha mpaka mnadhani ninyi ndiyo wenye haki ya kuishi Tanzania tu. Kuna siku mtapata mnachokitafuta.
 
Ujasema shida ya kodi hiko wapi.

Hao wahuni wanao waamasisha kutolipa kodi wanavunja sheria (mshukuru huruma wa bi-tozo).

Vinginevyo kwa mamlaka ya TRA kupitia mamlaka ya ‘tax administration’ watu kama nyie msiotaka kujifunza hesabu za biashara zenu, kwa Sasa mshukuru huruma wa raisi.

Lipa kodi hesabu żako za hovyo bila ya kuzingatia finance bills (ya mwaka husika), employment laws na business rates za mahala ulipo hazina uhusiano na sera za nchi. Ni jukumu lako kuzielewa vinginevyo. .

Bila ya maelezo shida yako ni nini? serikari itakuchukulia wewe ni mkwepa kodi. Bahati nzuri hii ni serikali yakulea na kukuza biashara sema unakwazika vipi upewe elimu.

Serikali haipo kunyanyasa wafanya biashara ilal ipo kuwakuza wafanyabiashara hilo ndio lengo lake.

Njia moja wapo ya kukuza biashara ni kuwapa elimu ya kodi na namna ya kupiga hesabu sahihi za kibiashara sio mambo yenu ya kubuni, na kujadiliana based on simple costs. Baada ya hapo mnaanza malalamiko.

Kuhamasisha watu kutokulipa kodi kwa sababu za upumbavu zilizopo kwenye upumbavu wa vichwa vya viongozi weny sio suluhisho, Wakati TRA ipo mpaka ndani ya JF kwa sababu kujibu hoja tu.

Baada ya kukupa ukweli wa kodi kama unamaswali leta ujibiwe.

Sasa nakukaribisha kuuelezea umma jinsi unavyonijua, usiache kitu, Iła mimi sijui utani na wala sipendi mazoea kwa wanaonijua vizuri.

Lipa kodi, uwezi kuwa kila siku unapewa elimu kodi ni sheria ambayo utaki kuelewa halafu unalalamikia ignorance yako.

Kama ujifunzi kwa maneno, utajifunza kwa matendo (yote kwa ni kwa mujibu wa sheria hakuna uonevu).
Wananchi walikupuuza na mimi nakupuuza vile vile...biashara gani ushawah fanya wewe na ukafanikiwa?
 
Huu ni mkakati mahususi na umekuwa ukifanyika kila wakati kiongozi wa nchi anapokuwa Muislamu ili kuhakikisha utawala huo unakosa utulivu na kuleta chuki baina ya wananchi na utawala uliopo madarakani.
Wakati wa utawala wa Magufuli wafanyabiashara walionewa sana ikiwa ni pamoja kufunguliwa kesi za uhujumu uchumi na kuporwa pesa kwenye akaunti zao benki lakini hatukushuhudia hata kunguni kuandamana au kugoma,
Huu ni unafiki na tukae tukijua kwa unafiki tulionao Watanzania hatutofanikiwa kujinasua kutoka kwenye makucha ya utawala dhalimu wa ccm.
Waliogopa viroba na wasiojulikana tu. Walikuwa na kero kibao!
 
Back
Top Bottom