MGOMO: Wafanyabiashara Kariakoo kufunga biashara zao kuanzia 24/6/2024 mpaka changamoto zao zitakapotatuliwa'

MGOMO: Wafanyabiashara Kariakoo kufunga biashara zao kuanzia 24/6/2024 mpaka changamoto zao zitakapotatuliwa'

Wafanyabiashara wote wa viunga vya Kariakoo mnatakiwa kufunga biashara zenu zote ikiwemo maduka yenu, ofisi zetu na chochote unachokifanya kuanzia Jumatatu ya Juni 24, 2024 bila ukomo hadi pale changamoto zetu zote za kibiashara zitakapoweza kutatuliwa.

Mikoa ya Mbeya, Iringa, Mwanza, Arusha, Ruvuma, Kagera na Rukwa mtaanza kufunga biashara zetu kuanzia siku ya Jumanne ya Juni 25, 2024 bila ukomo.

Kuanzia siku ya Jumatano ya Juni 26, 2024 wafanyabiashara wote nchini tutaungana kufunga biashara zetu hadi pale changamoto zetu zote zitakapopata ufumbuzi wa kudumu.

Kutakuwa na kikosi kazi cha kupitia ili kukagua ofisi au biashara ambazo hazijafungwa ili kuhakikisha wote tunaungana kupambana na udhalimu huu wa kodi kandamizi.

----
Pia soma
Tetesi: - Wafanyabiashara Kariakoo kugoma muda wowote kutokana na madai yao kupuuzwa

View attachment 3023083
Watu wnapenda kumbip mama bila sababu..mama vunja miguu hao wote...na watu wanaofunga maduka yao wanahujumu uchumi.. hivyo wachukuliwe hatua stahiki...hatuwezi cheza na mambo ya nchi yaani kila kukicha mtu anaamua tu kuharibu hali ya hewa...hatutakubari hata kidogo..
 
Hapaba ni bongo sio kenya...na aliyetuma huu ujumbe ni mkenya tu
 
Kabisa naungana nao maana kinachofanyika saizi sio kodi tena bali ni ufisadi.

Hadi msajili line aliyeweka bango nje la tigo siku hizi wamekuja na sheria mpya inaitwa kodi ya bango ikimtaka huyo mtu awe analipia hilo bango.

Kuna mtu jana katozwa na Manispaa 80K kwa ajili ya bango la saluni "hair cutting"

Bado hapo hujazungumzia Service Lay, mawakala wa miamala wanalalamika kamisheni zao zinakatwa na mwisho wa mwezi TRA wanachukua 10%

Lakini bado wanalazimika kuwa na lesenj ku run biashara hiyo yani wanakatwa kodi zaidi ya mara mbili kwenye huduma moja.

Huu ni ukandamizaji, nchi imeingia gizani viongozi wanajali matumbo yao mtu wa chini wala hawamuangalii.

Naungana na wafanyabishara wa Kariakoo kwenye hili.
Serikali ijiondoe kwenye matumizi ya anasa yakiwemo ya kununua magari ya kifahari ya viongozi kila mwaka na safari zilizojaa misururu ya viongozi kwenda nje na kuacha mianya mingi ya ufisadi kwenye pesa za umma, haingii akilini kodi zinakamuliwa kwa wafanyabiashara na wananchi maskini kupitia tozo kwenye miamala ya simu na mabenki, bado wanaanzisha tozo kwenye gesi kwa watu wanaotaka kujikwamua kwenye kutumia petroli ambayo bei yake imewekwa juu ambayo siyo himilivu. Hapo hapo mikopo kutoka nje inachukuliwa kama njugu.......wakiambiwa walete katiba mpya kuweka misingi bora na imara ya uongozi na itakayotoa misingi ya uhuru na haki kwa wananchi kuchagua viongozi na mfumo wa uongozi wanaoutaka wanapiga chenga.
Huku mitaani barabara ni mbovu kila mahali, ila kodi na tozo zinakusanywa......nchi ngumu hii.
 
TRA ni wasumbufu sana na ukijaribu kuhoji unaambiwa funga biashara, kodi wanadai mara 2 ukiwaliza wanakwambia leta ushahidi, hivi kweli mtu unatunza risti ya 2018? eti ooh! toka mwaka huo hujawahi kulipa kodi ya mapato au VAT unawauliza mbona kila mwaka mnanipa Tax clearance?? jibu eti wao hawajui wanataka ushahidi, kama kweli computer zenu TRA hazitunzi kumbukumbu mbona tunapolipa hatuambiwi tulete rist wakati huo ili iwekwe kwenye file zenu? TRA ni wezi na kama sikosei inatafutwa hela ya kumiliki timu ya mpira si kwa unyanyasaji huu.Waziri wa fedha hela ya kumiliki timu ya mpira unaitoa wapi kama sio kuwaibia wananchi.

Hatari sana
 
Kikosi kazi alichounda waziri mkuu kikijumuisha wawakilishi wa wafañyabiashara kimefanya kazi gani?

Yule mama Bonge alikuwa anamsifia Samia mpaka anabubujikwa na machozi naye atagoma?

Haya mambo wanayaweza Wakenya tu.
Sasa mama bonge na waziri mkuu...lao moja bussiness patners kabisa..hii nchi kuna muda sijui ufanye nini..
 
Watu wnapenda kumbip mama bila sababu..mama vunja miguu hao wote...na watu wanaofunga maduka yao wanahujumu uchumi.. hivyo wachukuliwe hatua stahiki...hatuwezi cheza na mambo ya nchi yaani kila kukicha mtu anaamua tu kuharibu hali ya hewa...hatutakubari hata kidogo..
Wewe ni makota ya mbwa....
 
Hapaba ni bongo sio kenya...na aliyetuma huu ujumbe ni mkenya tu
Jana mimi nilikipokea hiki kipeperushi pale town so sijui kama muhusika/,mchapaji ni mkenya au siyo mkenya ila hicho Kiswahili kilichotumika hapo ni cha Tanzania
IMG_20240622_150936.jpg
 
Wangaoi wamekufa upto now? Basicaly mswaada bado haujapitishwa na rais. Hivi uanfikiri utapigania haki bila dam kumwagika somehow?
Wewe unasubiri nini ndani toka nje huku uje uandamane damu yako imwagike kwaajili ya wanao au vipi?

Ofcourse nilishaandamana back then, even nilipokuja nchi za nje sikuacha kushiriki maandamano mbali mbali. Why damu haijamwagika mpaka leo, well ukiandamana kistaarabu hupati shida, huo ni uzoefu wa nchi niliyopata hiyo nafasi.

Lakini pia kuandamana si suala la mtu moja bali udhubutu wa jamii, jamii yenyewe ndio ina vijana wa hovyo , chawa, wana ignore masuala ya nchi wako bize na comasava, umbea,mange kimambi. Tell me why niandamane kwenye jamii yenye watu aina yako ambao hawaoni umuhimu?

Unajua kinacho wabeba kenya, ni umoja, jamii imeamka wanajitambua sio yes man.
Hamna umoja means hamna team
 
Huu ni mkakati mahususi na umekuwa ukifanyika kila wakati kiongozi wa nchi anapokuwa Muislamu ili kuhakikisha utawala huo unakosa utulivu na kuleta chuki baina ya wananchi na utawala uliopo madarakani.
Wakati wa utawala wa Magufuli wafanyabiashara walionewa sana ikiwa ni pamoja kufunguliwa kesi za uhujumu uchumi na kuporwa pesa kwenye akaunti zao benki lakini hatukushuhudia hata kunguni kuandamana au kugoma,
Huu ni unafiki na tukae tukijua kwa unafiki tulionao Watanzania hatutofanikiwa kujinasua kutoka kwenye makucha ya utawala dhalimu wa ccm.
Sidhani kama kuna udini hapo. Kuna wafanyabiashara wa Kiislamu pia hapo Kariakok, na wanajielewa. Wasingekubali kutumika kwa maslahi ya dini nyingine.
 
NDO UKWELI NA WEWE UMETHIBITISHA. VERY WEAK. YAANI MAANDAMANO AU MIGOMO YA WATU MNALETA SUALA LA DINI? VERY STUPID KWA KWELI. MNASABABISHA KILA MTU WA IMANI HIYO AANZE KUONEKANA HANA AKILI
Yule wa imani ile aliienda kuua albino nae anawakilisha wa imani yake?
 
Kaka mbona wafanyabiashara wa rangi nyeupe wanatoa risiti halali. Nenda kanda pale kwa msomali. Shida ipo kwa sisis ngozi nyeusi. Tunapenda janja janja. Wenzenu wanatoa risiti nzima nzima kwanini ninyi hamtoi. Haya sawa mnatoa risiti pungufu ba bado mnalalamika kodi kubwa🤣🤣🤣.yaani mtu kanunua kitu cha milioni 3 umempa risiti ya laki 3.lakini bado hapo hapo unaona hyo laki 3 kodi yake kubwa.badilikeni
Hata hao ni wezi unakuta mtu mzima na mkanzu anakupa risiti yenye muda tofauti na muda ule uliofika kununua bidhaa halafu risiti yenyewe katoka nayo chamber
 
Huu ni mkakati mahususi na umekuwa ukifanyika kila wakati kiongozi wa nchi anapokuwa Muislamu ili kuhakikisha utawala huo unakosa utulivu na kuleta chuki baina ya wananchi na utawala uliopo madarakani.
Wakati wa utawala wa Magufuli wafanyabiashara walionewa sana ikiwa ni pamoja kufunguliwa kesi za uhujumu uchumi na kuporwa pesa kwenye akaunti zao benki lakini hatukushuhudia hata kunguni kuandamana au kugoma,
Huu ni unafiki na tukae tukijua kwa unafiki tulionao Watanzania hatutofanikiwa kujinasua kutoka kwenye makucha ya utawala dhalimu wa ccm.
Uislamu au dini imeingiaje hapo mkuu ???
 
Back
Top Bottom