Mgomo Wasambaa Nchi nzima, Wafanyabiashara wa Kyela nao wagoma

Mgomo Wasambaa Nchi nzima, Wafanyabiashara wa Kyela nao wagoma

Maduka yote Mjini Kyela leo 25/06/2024 yamefungwa, ikiwa ni muendelezo wa Mgomo wa wafanyabiasha nchi nzima kupinga dhuluma za serikali kupitia TRA, kuwakamua Wafanyabiashara hadi watoke damu.

Wengi waliofuata mahitaji ya watoto wao hasa kipindi hiki kuelekea kufunguliwa kwa Shule, Wamepigwa na butwaa baada ya kukutana na Makufuli milangoni, haifahamiki hali hii itakuwa hadi lini.

Nachukua nafasi hii kuwapongeza Wafanyanyabiashara wenzangu wa Kyela kwa maamuzi ya kishujaa

View attachment 3025475View attachment 3025476
njaa itawarudisha wafungue wala haina haraka watanyooroka tu wakianza kudaiwa vikoba watafungua hao
 
Ni vyema liwe endelevu na ikiwezekana nchi nzima mpaka vijijini.

Ni vyema wananchi wote tukaungana dhidi ya wanyonya damu, ili kulinda utu wetu na kuwafundisha hawa watu wetu wanaoona hii nchi ni ya kwao na uongozi ni dhamana ambayo sisi tumewapa.
 
hapa mpaka Uchumi Usimame
Syllo
Mtu akisema mpaka uchumi usimame anamaanisha nini? Je ni kuhujumu uchumi? Au kudai haki ya ili yeye anufaike hivyo serikali inufaike pia?
Au huenda ikawa ina maana mwaka huu mpaka uchumi wangu usimame nikimaanisha nipambane kwa nguvu na juhudi mpaka nifanikiwe kiuchumi?

Kauli hiyo ulitafsiri vipi? Na hao waliosema walitafsiri vipi? Maana unaweza kuwa ulitafsiri tofauti na wao na shida ikawa kwako si kwao.
kama huo sio uasi na uchochezi
syllo,

Sheria za nchi yetu Tanzania ukifanya uasi huwezi kupewa polisi wa kukulinda ili uendeleee na maandamano, nifundishe unaposema uasi una maanisha nini?
Haki ya katiba inasema Usimamishe shughuli za Kiuchumi?
syllo

Haki ya katiba inasema ni haki ya raia kufanya maandamano panapoonekana kuna mazingira gandamizi dhidi yao.

Kwani kauli ya Kusimamisha shuguli za kiuchumi ameisema nani?
 
Sawa. Ila usinipangie ni nani anayehusika na uhujumu wa uchumi huu.

Wakati CHADEMA ikiandamana ma hata baadhi za Uzi zenu za WANACHADEMA, mmekuwa mkichochea migomo ifanyike nchi nzima.

Nasema kwa uhakika kabisa, CHADEMA mnahusika, mlisema wenyewe wakati wa maandamano " mpaka uchumi usimame" itoshe, mnasherehekea mgomo huu.

CHADEMA inaingizwa moja kwa moja.

Ndio mitaji mliyonayo.

Hatahivyo, hamna sera wala mbadala wa mapato ya Serikali/Taifa kupitia kodi.
Sihusiki na siasa za nchi hii wala sina chama chochote.
Hili suala halijawa influenced na chadema by any means, wafanya biashara tena kupitia kiongozi wao ambae ni kada mtiifu wa CCM, wameona wanapata changamoto thats how wana address matatizo yao

Lakini pia maandiko yako haya facts, una hisia ambazo hazina uhalisia.
hili suala linahitaji facts na si politics
 
Huu ndio upotoshaji.

Misleading and Dangerous.

Mgomo ufanyike Kyela, waseme "Nchi nzima"

CHADEMA ina mbadala upi wa Kodi? Ina sera gani za Kiuchumi na Biashara?

Utawasikia jibu lao...."Katiba mpya"

CHAGUA kwa Umakini 2025.

Kumbuka CHADEMA haitaleta amani ndani ya nchi hii. Sembuse uchumi(ubora wa maisha na wa kifedha) kwa Wananchi wote.

Kumbukeni wakati wanaandama, walisema wazi kabisa, kwamba "mpaka uchumi usimame" Wananchi wanateseka kwa uchochezi na uharakati wa CHADEMA.
Huo ni upotoshaji wa ukweli uliopo sasa kila kitu anasingiziwa CHADEMA wakati nchi yote kuanzia balozi wa nyumba kumi kumi hadi raisi ni ccm tu .Pumbavu zenu nchi imewashinda.
 
Unaongelea marejesho kama mikopo ya mtasni ndio maana nakupinga
Hapana, naongelea facility kama term loans, overdrafts zilizopo kwenye mabank. Si unajua overdraft zinavyoumiza? Lazima uwaze iwapo hiyo pesa imelala dukani na umefunga biashara. Mpaka mfanyabiashara anagoma ujue kakosa alternative.
 
Back
Top Bottom