Kama unaamini demokrasia basi unaweza kuelewa kwanini nchi inaweza kufanya makosa ya kumweka madarakani rais asiyefaa.Mfano wa karibu kuhusu hilo ni Marekani,taifa tajiri na lililoendelea mara elfu kadhaa zaidi yetu lilipojikuta likiongozwa na kituko George W Bush.
Hivi ni kigezo kipi unachotumia kuihukumu jamii kuwa safi au chafu?Kikwete hakuingiA iKULU kwa vile Watanzania wote ni mafisadi (as you seem to impy) bali alitumia mkakati mwa miaka 10 ambao umefanikiwa katika nchi mbalimbali masikini za dunia ya tatu.Alitengeneza mtandao uliojumuisha maharamia ambao kwao fedha sio tatizo.Hawa walifahamu umasikini wa Watanzania walio wengi.Wakamwaga fedha zao kila kona,wakamchafua kila waliyeona tishio kwao,wakafilisi magazeti walioyaona kuwa kikwazo kwao (eg Rai ya kina Ulimwengu) na mbinu nyingine chafu zaidi ya hizo nilizotaja.
Kuna mambo mengine tunamwonea tu Mungu kwani hakukosea kuwapa watu utashi wa kubuni mikakati yenye manufaa kwa wenzao,lakini wajanjawahuni flani wakairekebisha kukidhi mahitaji yao binafsi.Hizi busara za kidini zisipotumiwa kimakini zinaweza kuishia kumtukana Muumba.Maana kuna usemi kwamba sauti ya wengi ni sauti ya Mungu,na JK alishinda kutokana na kura za watu wengi,na kama watu hao wengi ni mafisadi kama inavyodaiwa hapa ina maana sauti zao ni za kifisadi,meaning kuwa sauti ya Mungu hapo pia ni ya kifisadi.
Tusikimbilie kutoa majibu rahisi kwenye maswali magumu
Vizuri ndugu Mlalahoi
Hiyo mikakati hawakuifanya na mbwa au sungura, walifanya na binadamu wenzetu wenye akili tena wasomi wakubwa! walifanya mikakati makanisani na misikitini mwetu, wachungaji na mashehe walisema chaguo la Mungu.Kuna mtu aliingia mkenge na kuandika kitabu
tumaini lililorejea!
Hayo mabilioni waliwapa watu, watu hawakuwa na akili ya kuuliza ni za nini? zinakuja kipindi cha uchaguzi? au ni haki mtu kupokea fedha haramu kwa kisingizio cha umaskini?
Unaposea mikakati ya miaka 10, unamwelezea Lowassa na Kikwete, ambapo sasa ndiyo haya ya kutaka kuenguana yanatokea? je unafikiri hatuko katika mikakati mingine ya kumweka Kikwete hadharani kwa kuishabikia taarifa hii ya Kubenea?
Jamii kama nilivyosema, kama kuna watu hawakuwa mafisadi wakamchagua Kikwete based on media! tusemeje? walikuwa na base au sababu gani? kuimbiwa nyimbo na Komba?
ndiyo maana nikasema kama jamii siyo fisadi(kama ulivyoproof) basi ni jamii ignorance. Nikasema lazima tuwe na namna ya kuchagua viongozi sio rais tu mpaka ngazi ya kaya!
Tunapoona viongozi wakali tunawaita wanoko, na kwa jinsi hii tunachagua makapi
NA NDIYO YANAKUWA VIONGOZI WAKUBWA. Jamii inayochagua viongozi based on person interest not for society interest ni jamii iliyokwisha, angalia viongozi wa idara, taasisi, makanisani msikitini n.k
Mlalahoi nugu yangu: nadhani tunaeleweshana huwa sitaki ligi, ila niko tayari kukosolewa.just imagine maprofesa wa UDSM walivyoplay role ya Kikwete kuwa Rais , unafikiri babu yangu Kijijini atasemaje.. si ndio zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM?
Umesema Demokrasia , Yes, demokrasia ni kitu cha ajabu I support whaT you say. moja ongeza moja ni sawa na mbili, Demkrasia inaweza ikasema tatu!! eti kwa sababu ya kura! Lakini Demokrasia ikisema tatu haindoi ukweli kuwa 1+1=2!
Ndio maana nikasema swala system. Nchi inatakiwa iwe na misingi yake ya kikatiba, iwe na idara za kudumu za mipango, usalama wa taifa, mahakama, elimu na usalama wa raia.
Labda watu tunachanganya kuhusu serikali, serikali inadumu maana ndio nchi.Hata Rais mpya akija wanaobadilika ni mawaziri, manaibu n.k watu wengi kwenye idara/wizara wanabaki walewale? umeshasikia nchi za wenzetu kubadilisha wizara mara kwa mara? .watu wa chini ndio wanafanya mambo yaendelee, viongozi hao(politician) ni initiators na wanaweza wakaweka mipango mipya ambayo haikuwekwa na viongozi wa zamani.Ndiyo maana wenzetu wanazungumzia mipango ya miaka 100 ijayo! Bush baada ya september 11 alisema
''wamedondosha WTC na kuitikisa misingi yake, lakini hawajaweza kutikisa misingi ya america'' Unapokuwa na taifa ambalo secrety agency wako tayari kumuua Rais kwa sababu ye interest ya Taifa, hapo sawa. Bush unayemlaumu(sitaki kwenda sana huko) ana la kujitetea he was the man in office during 09/11! lakini mbaya au nzuri zaidi maamuzi kule hayatoki kwa washikaji au kwa wake wa marais. kuna wazee wanakaa, wanaamua, wanapanga bajeti.Leo pengine unasikia sana hilo kwa sababu ya upepo wa sasa hivi! maamuzi yale yalifanywa na wengi!
Ninasema haya nataka tujiangalie na sisi pia, lakini Pamoja na hayo yote bado haimpelekei Kikwete kutolaumiwa, he is to be hanged like Sadam
Mlalahoi, nasikitika hata hili jina la mlalahoi umelitoa wapi?
Tanzania hakuna shida!!!! Mali asili za kumwaga, watanzania wapole, wakarimu, watanzania hawtaki fujo, wastaarabu,watanzania wana upendo hata kwa viongozi mafisadi.Hali ilivyo sasa nchi zingine Kikwete angekuwa ameshaondoka siku nyingi, viongozi wa zamani walioifisadi nchi wangekuwa tayari jela, tusingemwona Rostam akihutubia KKT, wala Lowassa akifungua makanisa
Tusidanganyike, hatuna shida kama nchi zingine, ndiyo maana tumelala! ukiwa na taifa ambapo graduate wa chuo kikuu anaridhika , hawezi kuandamana eti yeye anapokea laki 4 kwa mwezi, so yuko relaxed anawaza kuongoza kamati za harusi tu! tumekwisha, tukiwa na tafa ambalo wanawashangilia mafisadi kama tulivyoona kwa Chenge na Lowasa,tumekwisha, tukiwa na tifa ambalo viongozi wa vyama vya upinzani nao ni mafisadi na ya kuwa wengi wao wana personal interest, na ndiyo maana unaona utitiri wa vyama vya upinzani, na vingine tutavijua wiki bili before election tumwekwisha. Ndiyo maana is hardly to find Odinga au Tsavangirai!. Ukiwa na taifa ambalo watu wanaandamana kwa ile HOTUBA YA KIKWETE! tumekwisha.
Ikifikia mali asili zote zimekombwa!, nauli zimepanda kiasi ambacho nusu ya watanzania hawawezi kwenda makazini! nusu ya watanzania wanalala na njaa, nusu ya watanzania wanashindwa kusomesha watoto sekondari, nusu ya watanzania wanashindwa kulipa rent za nyumba, wanashindwa kwenda hospitali kutokana na gharama.
HAPO NDIO UTAONA WATANZANIA WANAAMKA, NA TABIA ZOTE NZURI NILIZOZITAJA HAPO JUU zinabadilika na kuwa negative. ndiyo maana nikasema Kikwete anatesa na tabia ya walio wengi na hali halisi ya nchi.Ufisadi ni ufisadi hata kama ukifanywa na mfagizi, tanzania unaweza ukapata chochote ukiwa na hela hata mitihani!
Tusidanganyike wakati wengine hawalali kwa sababu ya perfomance ya viongozi wa sasa, wengi tena wasomi wako kimya maana wanakula, wanalala, wana magari mazuri, ndiyo maana tunaona shwari.
Hatupaswi tukae kimya kwa sababu wengine wamekaa kimya, hatupaswi kusubiri kila kitu kizuri kichukuliwe ndio tuamke.
SISI TULIOAMKA YATUPASA TUWAAMSHE WENGINE, AU TUPIGE KELELE ZIHARIBU USINGIZI WAO, ILA TUKIWA MACHO WASITUVUTE KWAO. MAANA NAAMINI JAMII YA WATANZANIA WANAOTUMIA WENYE ACCESS YA MITANDAO WENGI WAO, NI WALE WENYE GOOD LIFE, UKICOMPARE NA WENGINE.NDIYO MAANA NAHAMASIKA Nikiona watu wanatoa mawazo yao hapa ya kulenga kulilinda taifa letu zuri
Nadhani nimejitahidi, kindly I remain to be corrected wherever my views are not ,clear acceptable or challenged.
Waberoya