Mgongano: Serikali Vs. Mwanahalisi - Mipaka ya Maoni?

Mgongano: Serikali Vs. Mwanahalisi - Mipaka ya Maoni?

Nimeshindwa kusikiliza mahojiano but based on the words sijaona kama kuna uchochezi kama ambavyo wengi tunafikiri.

My take:

Kubenea anatafutwa sana na wanamtandao kwani kila mbinu wanayotaka kutumia jamaa anawatibulia kwa kuiweka hadharani. Pia haya ni mambo ya kisiasa sidhani yana ubaya wowote hat akina EL kuyajadili this is politics bwana kwa kuwa hata mimi najiandaa kumbwaga mbunge fulani. kosa hapa lipo wapi? ina maana wale wanaolalamikia ninavyotoa misaada kule jimboni kule ndo serikali nayo inalalamikia watu kujipanga kwa 2010? stupid Jacob Tesha! siasa ni pamoja na kuumia opportunities zilizopo man! kama akina EL na RA wameona Benno ni mtaji na pia anauhusiano na kikwete wakaamua kuitumia that fine no p at all, vipi Tesha unataka watu waseme nini sasa?

Hakuna sehemu hata moja ambapo wamekose akina Halisi cha msingi ni kuwa plan na strategy yao imekuwa open cha msingi watafute plan nyingine. Hoja hapa waje wale waliotajwa wampeleke Kubenea kule wanakotaka lakini serikali ikae kimya kabisaaaaa.

Huyu Rwe nae mungu amsaidie tu.....................
 
Huyu Rostam nae? nilidhani angelalamikia kutuhumiwa kuwapo kwenye kundi linalotaka kumwondoa rais madarakani (ndio kisa cha Mwanahalisi kuwa kwenye tishio la kufungiwa sasa), kumbe yeye analilia kuhusishwa kwenye kashfa ya wizi wa bilioni 13? Hizi tuhuma nyingine anazikubali ama?

Hata hivyo bado naona ni fursa kwa Mwanahalisi kumwaga ukweli wote mahakamani, na vyombo vya habari vituripotie ili kila kitu kijulikane, penye ukweli hakuna majungu wala fitna!
 
JUKWAA la Wahariri limesema limehuzunishwa na hatua, jinsi na nguvu iliyotumika na Serikali kushughulikia habari iliyoandikwa na gazeti la MwanaHalisi Jumatano wiki hii.

Laiti ningekuwa mshauri wa JK ningemwambia awazuie 'watu wake' wasithubutu kufanya wanachotaka kufanya (kulifungia mwanahalisi) kwani anguko lake liakuwa ni la aibu.
Hakuna sababu ya msingi ya kufungia gazeti kwa kuweka mambo hazarani badala ya kuwafunga mafisadi wanayageukia magazeti, ovyooo!
 
umefika wakati wa mwanahalisi kuwaeleza wananchi ukweli wa kweli kuhusu viongozi wao kwani huko mahakamani hakuna kuficha kitu, kila kitu kitakuwa wazi kwa wote walioudhuria.

Serikali hatua itayochukua haraka ni kuifungia mwanahalisi lakini haiwezi kwenda mahakamani, hata hivyo akifungia hilo lingine litaanzishwa na kuendeleza kampeni hii kama kawaida.

Walikuwa wanatafuta nafasi sasa wameipata wataitumia vizuri.
 
Binafsi simtaki Lowassa tokea enzi za Nyerere na naamini hana nafasi tena ya kuwa rais au PM wa Tanzania. Anaweza kurudi kwenye baraza la mawaziri lakini sio kuwa rais au PM. Pamoja na hayo, pia sipendi kulishwa sumu na hawa waandishi ambao chuki zao binafsi zinakuwa mbele kuliko ukweli wa habari.

Quote: Gazeti la Mwananchi

"Kwa nini habari hii ilete shida kwa Gazeti la MwanaHalisi pekee wakati tayari iliripotiwa na kuandikwa na Gazeti la Rai kwenye moja ya matoleo yake ya Aprili mwaka huu?" alihoji.

Besides, kwenye kikao cha mwisho cha NEC mjumbe Ole Sendeka,alimkumbusha mjumbe wa kundi la mafisadi Serukamba kwamba haitawezekana wao kugombea urais 2010 kama wanavyopanga kwa sababu muungwana ni lazima aendelee, hapa yaliposemwa rais mwenyewe alikuwepo, mbona haikuwa tatizo?

Mkuu Mtanzania,

Ni haki yako kumuamini Mtikila, lakini mimi ninamuamini Kubenea kwa 100%.
 
...nitawakumbusha wanaJF wenzangu kuwa vitabu vya Mwenzimungu vimesema Yeye(Mungu) atatupa viongozi wanaofanana na watakao waongoza. Ninaheshimu sana maandiko na nina amini kuwa yana ukweli ukweli mtupu.

Tukumbushe Mkuu. Ni vitabu gani hivyo na ni mahala gani imeandikwa hivyo ?
 
(Mungu) atatupa viongozi wanaofanana na watakao waongoza

Mkuu Sokomoko,

Hebu fafanua una maana ipi hasa, yaani ndivyo tulivyo au viongozi wetu ni reflection yetu wananchi tuliowachagua?
 
Nimecheka sana, nadhani hii sentensi inahitaji kitabu kufafanua, anyway let me try using few lines.

Rais wa nchi huwekwa na watu, kama Rais fisadi, ina maana waliomchagua ni mafisadi, kama alikuwa safi akageuka, it means we have poor systems ambazo haziwezi kumfanya lolote Rais aliye madarakani. Na izi sytems huwekwa na watu.

Hamna jamii safi yenye system safi ikamuweka RaiS wa haina hii madarakani.

Kikwete ana wakilisha tamaduni zetu, majumbani, makazini na kila mahali.Kama jamii fisadi Rais atapatikana kifisadi, kwa hiyo na yeye fisadi,Mtu safi hakai kwenye system chafu, akikaa akijua aamekubaliana nao!

Walio wasafi kumchagua kiongozi mchafu kuna mawili aidha jamii mbumbumbu(wajinga)au HAIJAWEKA SYESTEM RAIS WAO HAWEJE. hatujui historia za hawa viongozi, walifanya nini huko nyuma. aidha kama walihusika kusaini mikataba mibovu au la, na ahata kama tulijua walifanya ubaya, Lakini wanakuja wakivaa nguo nyingine, na kuomba cheo kikubwa kuliko kile, tunajiaminisha kuwa siyo yeye!

Wote wamepotea na kupungukiwa utukufu wa uadilifu, kila mahali Tanzania imeoza, makanisani na misikitini jamii imeoza. Kama msafi ni wewe mweyewe ujuaye, lakini usishangae wapiga kelele wengi wa ufisadi wao wenyewe mafisadi, tunajiaminisha kila mtu atakula "ofsini mwake"

I submit

waberoya

Kama unaamini demokrasia basi unaweza kuelewa kwanini nchi inaweza kufanya makosa ya kumweka madarakani rais asiyefaa.Mfano wa karibu kuhusu hilo ni Marekani,taifa tajiri na lililoendelea mara elfu kadhaa zaidi yetu lilipojikuta likiongozwa na kituko George W Bush.

Hivi ni kigezo kipi unachotumia kuihukumu jamii kuwa safi au chafu?Kikwete hakuingiA iKULU kwa vile Watanzania wote ni mafisadi (as you seem to impy) bali alitumia mkakati mwa miaka 10 ambao umefanikiwa katika nchi mbalimbali masikini za dunia ya tatu.Alitengeneza mtandao uliojumuisha maharamia ambao kwao fedha sio tatizo.Hawa walifahamu umasikini wa Watanzania walio wengi.Wakamwaga fedha zao kila kona,wakamchafua kila waliyeona tishio kwao,wakafilisi magazeti walioyaona kuwa kikwazo kwao (eg Rai ya kina Ulimwengu) na mbinu nyingine chafu zaidi ya hizo nilizotaja.

Kuna mambo mengine tunamwonea tu Mungu kwani hakukosea kuwapa watu utashi wa kubuni mikakati yenye manufaa kwa wenzao,lakini wajanjawahuni flani wakairekebisha kukidhi mahitaji yao binafsi.Hizi busara za kidini zisipotumiwa kimakini zinaweza kuishia kumtukana Muumba.Maana kuna usemi kwamba sauti ya wengi ni sauti ya Mungu,na JK alishinda kutokana na kura za watu wengi,na kama watu hao wengi ni mafisadi kama inavyodaiwa hapa ina maana sauti zao ni za kifisadi,meaning kuwa sauti ya Mungu hapo pia ni ya kifisadi.

Tusikimbilie kutoa majibu rahisi kwenye maswali magumu
 
Field Marshall Es,
Mkuu mimi nipo nyuma yako na nakuaminia sana... Hizi habari kama zilivyotoka na jinsi zinavyoendelea zinaonyesha wazi kabisa kwamba kuna jambo linapikwa...

Ni kawaida ya mswahili kuchukia UKWELI unapotoka na mara nyingi huchukua hatua haraka na kukemea kuliko anaposikia Uongo kuhusiana naye... ukiwa uongo hucheka na kupuuza lakini sio ukweli, tunakuwa wakali ajabu atadhani mtu kafumaniwa!..

Tofauti na wenzetu wazungu ambao wakisikia UONGO ndio huchukia na pengine kuchukua hatua kali dhidi ya Uongo.. Unapotokea UKweli wao hujikanyaga na kuachia ngazi ama kuomba msamaha tofauti na Mswahili..

Ushahidi niliokwisha Upata kuhusiana na hatua zinazochukuliwa na vyombo vya serikali hadi sasa hivi, nayakubali maneno yako na nitarudia kusema hivi - 'Kikwete anatumia muda mwingi nje ya nyumba yake hivyo mabingwa wenye fikra chafu ni lazima watakuwepo!'

Inambidi awe macho sana kwa sababu haya maneno yamezungumzwa sana vijiweni kote, lisemwalo lipo kama halipo basi liko njiani...

Lowassa na timu inayoamini ndio walimweka madarakani wamepania kumwondoa..
nakumbuka sana Lowassa alipokuwa waziri mkuu alitawala yeye!.. kumbukumbu ya Lowassa kama waziri mkuu haiwezi kupotea hkwani alionyesha wazi kuwa ni mtu anayependa sana madaraka, mtu anayependa kusujudiwa, Ni mcheshi pale unapoonyesha unyenyekevu kwake - Mungu mtu.

Ni kweli kabisa Kikwete kawatema hawa jamaa kuwaondoa madarakani!.. ni jambo ambalo haliwezi kusameheka hivi hivi tu kwa watu kama Lowassa, Karamagi na hata Rostam ambaye alikuwa mweka fedha wa CCM.

Wanamwona kawageuka hawapo tena katika Ulaji na nguvu ya Utawala.. Ni chuki sawa na ile iliyomkuta Nyerere na kina Kambona na Bibi Titi ambao mbali na kutangazwa Azimio la Arusha waliona mwalimu kawageuka pamoja na kwamba walikuwa bado wana nguvu kubwa serikalini.

Mkuu FMES, nikikumbuka jinsi ulivyotupangia nguvu ya Mtandao kumwingiza Kikwete madarakani....

1. Jinsi sheria na Taratibu za Uchaguzi ndani ya CCM zilivyovunjwa,
2. Jinsi fedha zilivyomwagwa,
3. Jinsi Mkapa alivyozungukwa na hata Malecela kutupwa nje wakati alikuwa na haki sawa na viongozi wengine,
4.Jinsi Salim A Salim alivyodhalilishwa...n.k

Mambo yote haya bila mkono wa Kikwete iweje hili liwe haliwezekani!...wakati list ya Baraza la mawaziri na manaibu wake alioanza nao 2005, asilimia kubwa (ya Mtandao) wako nje!.

Nakukubali mkuu...Siku zote sisi Wadanganyika hugutuka too late hata gonjwa la AIDS tulikuja shituka baada ya kumaliza vijana wengi mijini... na bado tukatunga kinga za kiasili - Nzi kufika kidondani sii haramu.

Kwa hiyo sishangai hata kidogo watu wanapoanza kupinga - NDIVYO TULIVYO..
 
Mkuu Bob,

Heshima ikurudie bro, muungwana is playing smart politics ili a survive na chama kisimeguke under his hands, na amekua akifanya hivyo kwa muda mrefu sana sasa, lakini sasa not anymore jipu linakaribia kupasuka, inatafutwa njia ya kutokea!

Mkapa did the same, yaani siasa za ku-survive tu ili muungano usife na chama kupasuka under his hands, he could not wait kutoka kwenye power kabla mambo hayajaenda mrama, aliyekuwa akimdanganya ni yule mzee wa Mbeya!

Mafisadi wamechacha, na wamekasirishwa sana na jinsi ishu ya Nape ilivyokuwa handled na muungwana, maana amewaabisha na kuwachafua sana mbele ya jamii, sasa kuna picha nyingine inakuja ya uchaguzi wa UWT ambako Mama Mamuya, aliondolewa mapema kwa tuhuma za wizi wa hela za jengo, the dataz ni kumbe alishirikiana na Mama Anna Abdallah, mwenyekiti wake yeye akiwa katibu kuzichota na anaushahidi, aliokuwa ameuweka akisubiri kuutumia kwenye kugombea uenyekiti, juzi Mama Anna kamkata jina na kumpa E kuwa hafai,

The dataz ni kwamba mama mamuya, kapeleka ushaidi wote kwa muungwana na mawaziri wakuu wote na wajumbe wote wa CCC, ndio maana ukasikia Warioba anapiga kelele yaani na huyu ametumia style ile ile ya Nape, huku muafaka umegoma na uchaguzi unakuja, wazungu wakuuu wa dunia wameshampa onyo zito muungwana kua this time watakuwa macho sana na uchaguzi wa huko visiwani, huku mafisadi wamechacha, serikali sasa kama ime-freeze maana kila siku ni scandal kila kona wananchi hawana imani tena na Mtandao,

Sasaa huwezi kusema kwua haya yote ni makosa ya Kubenea, wachawi hapa wanafahamika sio Kubenea, ndio maana tunaojua vizuri tunashangaa kulikoni serikali na kumtisha Kubenea na kuwaacha wenyewe hasa mafisadi?
 
Kama unaamini demokrasia basi unaweza kuelewa kwanini nchi inaweza kufanya makosa ya kumweka madarakani rais asiyefaa.Mfano wa karibu kuhusu hilo ni Marekani,taifa tajiri na lililoendelea mara elfu kadhaa zaidi yetu lilipojikuta likiongozwa na kituko George W Bush.

Hivi ni kigezo kipi unachotumia kuihukumu jamii kuwa safi au chafu?Kikwete hakuingiA iKULU kwa vile Watanzania wote ni mafisadi (as you seem to impy) bali alitumia mkakati mwa miaka 10 ambao umefanikiwa katika nchi mbalimbali masikini za dunia ya tatu.Alitengeneza mtandao uliojumuisha maharamia ambao kwao fedha sio tatizo.Hawa walifahamu umasikini wa Watanzania walio wengi.Wakamwaga fedha zao kila kona,wakamchafua kila waliyeona tishio kwao,wakafilisi magazeti walioyaona kuwa kikwazo kwao (eg Rai ya kina Ulimwengu) na mbinu nyingine chafu zaidi ya hizo nilizotaja.

Kuna mambo mengine tunamwonea tu Mungu kwani hakukosea kuwapa watu utashi wa kubuni mikakati yenye manufaa kwa wenzao,lakini wajanjawahuni flani wakairekebisha kukidhi mahitaji yao binafsi.Hizi busara za kidini zisipotumiwa kimakini zinaweza kuishia kumtukana Muumba.Maana kuna usemi kwamba sauti ya wengi ni sauti ya Mungu,na JK alishinda kutokana na kura za watu wengi,na kama watu hao wengi ni mafisadi kama inavyodaiwa hapa ina maana sauti zao ni za kifisadi,meaning kuwa sauti ya Mungu hapo pia ni ya kifisadi.

Tusikimbilie kutoa majibu rahisi kwenye maswali magumu

Vizuri ndugu Mlalahoi

Hiyo mikakati hawakuifanya na mbwa au sungura, walifanya na binadamu wenzetu wenye akili tena wasomi wakubwa! walifanya mikakati makanisani na misikitini mwetu, wachungaji na mashehe walisema chaguo la Mungu.Kuna mtu aliingia mkenge na kuandika kitabu tumaini lililorejea!

Hayo mabilioni waliwapa watu, watu hawakuwa na akili ya kuuliza ni za nini? zinakuja kipindi cha uchaguzi? au ni haki mtu kupokea fedha haramu kwa kisingizio cha umaskini?

Unaposea mikakati ya miaka 10, unamwelezea Lowassa na Kikwete, ambapo sasa ndiyo haya ya kutaka kuenguana yanatokea? je unafikiri hatuko katika mikakati mingine ya kumweka Kikwete hadharani kwa kuishabikia taarifa hii ya Kubenea?

Jamii kama nilivyosema, kama kuna watu hawakuwa mafisadi wakamchagua Kikwete based on media! tusemeje? walikuwa na base au sababu gani? kuimbiwa nyimbo na Komba? ndiyo maana nikasema kama jamii siyo fisadi(kama ulivyoproof) basi ni jamii ignorance. Nikasema lazima tuwe na namna ya kuchagua viongozi sio rais tu mpaka ngazi ya kaya!

Tunapoona viongozi wakali tunawaita wanoko, na kwa jinsi hii tunachagua makapi NA NDIYO YANAKUWA VIONGOZI WAKUBWA. Jamii inayochagua viongozi based on person interest not for society interest ni jamii iliyokwisha, angalia viongozi wa idara, taasisi, makanisani msikitini n.k

Mlalahoi nugu yangu: nadhani tunaeleweshana huwa sitaki ligi, ila niko tayari kukosolewa.just imagine maprofesa wa UDSM walivyoplay role ya Kikwete kuwa Rais , unafikiri babu yangu Kijijini atasemaje.. si ndio zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM?

Umesema Demokrasia , Yes, demokrasia ni kitu cha ajabu I support whaT you say. moja ongeza moja ni sawa na mbili, Demkrasia inaweza ikasema tatu!! eti kwa sababu ya kura! Lakini Demokrasia ikisema tatu haindoi ukweli kuwa 1+1=2!
Ndio maana nikasema swala system. Nchi inatakiwa iwe na misingi yake ya kikatiba, iwe na idara za kudumu za mipango, usalama wa taifa, mahakama, elimu na usalama wa raia.

Labda watu tunachanganya kuhusu serikali, serikali inadumu maana ndio nchi.Hata Rais mpya akija wanaobadilika ni mawaziri, manaibu n.k watu wengi kwenye idara/wizara wanabaki walewale? umeshasikia nchi za wenzetu kubadilisha wizara mara kwa mara? .watu wa chini ndio wanafanya mambo yaendelee, viongozi hao(politician) ni initiators na wanaweza wakaweka mipango mipya ambayo haikuwekwa na viongozi wa zamani.Ndiyo maana wenzetu wanazungumzia mipango ya miaka 100 ijayo! Bush baada ya september 11 alisema ''wamedondosha WTC na kuitikisa misingi yake, lakini hawajaweza kutikisa misingi ya america'' Unapokuwa na taifa ambalo secrety agency wako tayari kumuua Rais kwa sababu ye interest ya Taifa, hapo sawa. Bush unayemlaumu(sitaki kwenda sana huko) ana la kujitetea he was the man in office during 09/11! lakini mbaya au nzuri zaidi maamuzi kule hayatoki kwa washikaji au kwa wake wa marais. kuna wazee wanakaa, wanaamua, wanapanga bajeti.Leo pengine unasikia sana hilo kwa sababu ya upepo wa sasa hivi! maamuzi yale yalifanywa na wengi!

Ninasema haya nataka tujiangalie na sisi pia, lakini Pamoja na hayo yote bado haimpelekei Kikwete kutolaumiwa, he is to be hanged like Sadam

Mlalahoi, nasikitika hata hili jina la mlalahoi umelitoa wapi?

Tanzania hakuna shida!!!! Mali asili za kumwaga, watanzania wapole, wakarimu, watanzania hawtaki fujo, wastaarabu,watanzania wana upendo hata kwa viongozi mafisadi.Hali ilivyo sasa nchi zingine Kikwete angekuwa ameshaondoka siku nyingi, viongozi wa zamani walioifisadi nchi wangekuwa tayari jela, tusingemwona Rostam akihutubia KKT, wala Lowassa akifungua makanisa
Tusidanganyike, hatuna shida kama nchi zingine, ndiyo maana tumelala! ukiwa na taifa ambapo graduate wa chuo kikuu anaridhika , hawezi kuandamana eti yeye anapokea laki 4 kwa mwezi, so yuko relaxed anawaza kuongoza kamati za harusi tu! tumekwisha, tukiwa na tafa ambalo wanawashangilia mafisadi kama tulivyoona kwa Chenge na Lowasa,tumekwisha, tukiwa na tifa ambalo viongozi wa vyama vya upinzani nao ni mafisadi na ya kuwa wengi wao wana personal interest, na ndiyo maana unaona utitiri wa vyama vya upinzani, na vingine tutavijua wiki bili before election tumwekwisha. Ndiyo maana is hardly to find Odinga au Tsavangirai!. Ukiwa na taifa ambalo watu wanaandamana kwa ile HOTUBA YA KIKWETE! tumekwisha.

Ikifikia mali asili zote zimekombwa!, nauli zimepanda kiasi ambacho nusu ya watanzania hawawezi kwenda makazini! nusu ya watanzania wanalala na njaa, nusu ya watanzania wanashindwa kusomesha watoto sekondari, nusu ya watanzania wanashindwa kulipa rent za nyumba, wanashindwa kwenda hospitali kutokana na gharama.HAPO NDIO UTAONA WATANZANIA WANAAMKA, NA TABIA ZOTE NZURI NILIZOZITAJA HAPO JUU zinabadilika na kuwa negative. ndiyo maana nikasema Kikwete anatesa na tabia ya walio wengi na hali halisi ya nchi.Ufisadi ni ufisadi hata kama ukifanywa na mfagizi, tanzania unaweza ukapata chochote ukiwa na hela hata mitihani!

Tusidanganyike wakati wengine hawalali kwa sababu ya perfomance ya viongozi wa sasa, wengi tena wasomi wako kimya maana wanakula, wanalala, wana magari mazuri, ndiyo maana tunaona shwari.

Hatupaswi tukae kimya kwa sababu wengine wamekaa kimya, hatupaswi kusubiri kila kitu kizuri kichukuliwe ndio tuamke.SISI TULIOAMKA YATUPASA TUWAAMSHE WENGINE, AU TUPIGE KELELE ZIHARIBU USINGIZI WAO, ILA TUKIWA MACHO WASITUVUTE KWAO. MAANA NAAMINI JAMII YA WATANZANIA WANAOTUMIA WENYE ACCESS YA MITANDAO WENGI WAO, NI WALE WENYE GOOD LIFE, UKICOMPARE NA WENGINE.NDIYO MAANA NAHAMASIKA Nikiona watu wanatoa mawazo yao hapa ya kulenga kulilinda taifa letu zuri

Nadhani nimejitahidi, kindly I remain to be corrected wherever my views are not ,clear acceptable or challenged.

Waberoya
 
Mkuu Waberoya,

Mungu akubariki sana,umeongea maneno mazito sana
 
Tukumbushe Mkuu. Ni vitabu gani hivyo na ni mahala gani imeandikwa hivyo ?

Unless hujui maana ya vitabu vya dini zote, or you dont have religion. Kwani wewe mkuu unavijua vitabu vya Dini gani?
 
Mkuu Sokomoko,

Hebu fafanua una maana ipi hasa, yaani ndivyo tulivyo au viongozi wetu ni reflection yetu wananchi tuliowachagua?

viongozi wetu ni reflection yetu wananchi tuliowachagua ndio maana kuwachukulia hatua kama kuandamana mpaka watoke ikulu haiwezekani! wachache watapaza sauti walio wengi hawatakereka!
 
Kama unaamini demokrasia basi unaweza kuelewa kwanini nchi inaweza kufanya makosa ya kumweka madarakani rais asiyefaa.Mfano wa karibu kuhusu hilo ni Marekani,taifa tajiri na lililoendelea mara elfu kadhaa zaidi yetu lilipojikuta likiongozwa na kituko George W Bush.

Hivi ni kigezo kipi unachotumia kuihukumu jamii kuwa safi au chafu?Kikwete hakuingiA iKULU kwa vile Watanzania wote ni mafisadi (as you seem to impy) bali alitumia mkakati mwa miaka 10 ambao umefanikiwa katika nchi mbalimbali masikini za dunia ya tatu.Alitengeneza mtandao uliojumuisha maharamia ambao kwao fedha sio tatizo.Hawa walifahamu umasikini wa Watanzania walio wengi.Wakamwaga fedha zao kila kona,wakamchafua kila waliyeona tishio kwao,wakafilisi magazeti walioyaona kuwa kikwazo kwao (eg Rai ya kina Ulimwengu) na mbinu nyingine chafu zaidi ya hizo nilizotaja.

Kuna mambo mengine tunamwonea tu Mungu kwani hakukosea kuwapa watu utashi wa kubuni mikakati yenye manufaa kwa wenzao,lakini wajanjawahuni flani wakairekebisha kukidhi mahitaji yao binafsi.Hizi busara za kidini zisipotumiwa kimakini zinaweza kuishia kumtukana Muumba.Maana kuna usemi kwamba sauti ya wengi ni sauti ya Mungu,na JK alishinda kutokana na kura za watu wengi,na kama watu hao wengi ni mafisadi kama inavyodaiwa hapa ina maana sauti zao ni za kifisadi,meaning kuwa sauti ya Mungu hapo pia ni ya kifisadi.

Tusikimbilie kutoa majibu rahisi kwenye maswali magumu

Demokrasia gani?ya afrika?unaongelea hii ya kenya na zimbambwe?Mimi siamini demokrasia sijui nyie wakuu! kwanza nafikiria kama nina ulazima wa kupiga kura yangu 2010 maana mafisadi watakuwa kila jimbo kumwaga pesa na kuwapumbaza wapiga kura ili watoe kula!
 
Kama unaamini demokrasia basi unaweza kuelewa kwanini nchi inaweza kufanya makosa ya kumweka madarakani rais asiyefaa.Mfano wa karibu kuhusu hilo ni Marekani,taifa tajiri na lililoendelea mara elfu kadhaa zaidi yetu lilipojikuta likiongozwa na kituko George W Bush.

Hivi ni kigezo kipi unachotumia kuihukumu jamii kuwa safi au chafu?Kikwete hakuingiA iKULU kwa vile Watanzania wote ni mafisadi (as you seem to impy) bali alitumia mkakati mwa miaka 10 ambao umefanikiwa katika nchi mbalimbali masikini za dunia ya tatu.Alitengeneza mtandao uliojumuisha maharamia ambao kwao fedha sio tatizo.Hawa walifahamu umasikini wa Watanzania walio wengi.Wakamwaga fedha zao kila kona,wakamchafua kila waliyeona tishio kwao,wakafilisi magazeti walioyaona kuwa kikwazo kwao (eg Rai ya kina Ulimwengu) na mbinu nyingine chafu zaidi ya hizo nilizotaja.

Kuna mambo mengine tunamwonea tu Mungu kwani hakukosea kuwapa watu utashi wa kubuni mikakati yenye manufaa kwa wenzao,lakini wajanjawahuni flani wakairekebisha kukidhi mahitaji yao binafsi.Hizi busara za kidini zisipotumiwa kimakini zinaweza kuishia kumtukana Muumba.Maana kuna usemi kwamba sauti ya wengi ni sauti ya Mungu,na JK alishinda kutokana na kura za watu wengi,na kama watu hao wengi ni mafisadi kama inavyodaiwa hapa ina maana sauti zao ni za kifisadi,meaning kuwa sauti ya Mungu hapo pia ni ya kifisadi.

Tusikimbilie kutoa majibu rahisi kwenye maswali magumu

Ndio maana I said vitabu vya dini vinasema Viongozi wetu ni mifano ya sisi (tunaoongozwa) kama Bush kituko how do you find hao raia wa Marekani?wengi wao hawajui hata Iraq ipo wapi wanadhani ni among the united states of thei country.
 
Una busara sana kaka!hili libaba linalojiita FMS ni kama vile halina akili!yaani hata mimi lilinidhania ni huyo kuhani!Yaani wewe ukiwa tofauti tu basi!

Any way ndo maisha na ukizingatia watu wanaunganishwa na internet basi mtu anakuwa na hisia tu mbaya zaidi anaamini hisia zake hata kama ni uongo!
Nashukuru na nyie kwa kuona hilo hapo nyuma nimewahi kusema kuwa hili lijukuu la seguyemisi kwanza ni liongo lina majungu ya ajabu lina visasi kama babu yake na pia halikubali kushindwa ata kama unalikamata redhandled...nakumbuka hapo nyuma nilipata kulishauri liwe linakaa jikoni na bibi yake wa kambo mh mlopokaji
 
Huyu Rostam nae? nilidhani angelalamikia kutuhumiwa kuwapo kwenye kundi linalotaka kumwondoa rais madarakani (ndio kisa cha Mwanahalisi kuwa kwenye tishio la kufungiwa sasa), kumbe yeye analilia kuhusishwa kwenye kashfa ya wizi wa bilioni 13? Hizi tuhuma nyingine anazikubali ama?

Hata hivyo bado naona ni fursa kwa Mwanahalisi kumwaga ukweli wote mahakamani, na vyombo vya habari vituripotie ili kila kitu kijulikane, penye ukweli hakuna majungu wala fitna!
kesi hii ilikuwa imefunguliwa muda mrefu uliopita ila wakati hili jipya linatokea ndio muda wa kujibu barua ya siku saba unakuwa umepita tayari....sasa hakuna haja ya kufungua kesi kwa kila anachosema kwa kuwa tayari tumeshamfungulia hio yamtosha kabisa.
 
Unatumia neno 'tu', wewe na nani hasa? Kubenea wananchi tupo nawe sambamba ili mradi utende haki.
 
Back
Top Bottom