Mgonjwa aidai TMJ, Hindu Mandal fidia ya shilingi milioni 500

Dar es Salaam. Mfanyakazi wa Wizara ya Kilimo, Frorence Samwel anadai fidia ya Sh500 milioni Hospitali za TMJ na Hindu Mandal za jijini Dar es Salaam na daktari Moirice Mavura kwa kile anachodai kuwa ni uzembe katika kumtibu.

Pia amedai alipwe Sh53 milioni kwa ajili ya gharama mbalimbali, ikiwemo ya matibabu na usafiri.

Frorence amefungua kesi hiyo dhidi ya Dk Mavura pamoja na hospitali hizo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akidai kuwa hospitali hizo zilifanya uzembe alipokwenda kupata huduma ya matibabu.

Akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ramadhan Rugemalira huku akiongozwa na wakili wake Norbert Mlwale alidai kuwa Juni 27, 2018 alienda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na alifanyiwa uchunguzi wa koo ndipo alielezwa amuone Dk Moirice Mavura.

Alidai baada ya kumuona Dk Mavura alimwelekeza kuwa aende katika hospitali ya Hindu Mandal kwa kuwa ina vifaa vya kisasa kwa ajili ya upasuaji na anafanya kazi katika hospitali hiyo.

Shahidi huyo aliieleza mahakama hiyo kuwa Julai 9, 2018 Dk Mavura alimfanyia upasuaji katika koo lake na alitoa sampuli za tezi la kushoto zikapelekwa katika hospitali ya TMJ kwa ajili ya uchunguzi.

Alidai baada ya kufanyiwa uchunguzi wa sampuli hiyo hospitali ya TMJ ilitoa ripoti yake ikidai kuwa alikuwa na ugonjwa wa Rapillary Carcinoma of Thyoid ambayo alikabidhiwa Dk Mavura.

Baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo Dk Mavura alimfanyia upasuaji wa pili na kuiondoa tezi iliyoambukizwa ugonjwa huo.

Anaeleza kuwa baada ya kufanyiwa upasuaji huo zilichukuliwa sampuli za tezi zenye ugonjwa huo na zilipelekwa katika Hospitali ya TMJ kwa ajili ya uchunguzi mwingine ambapo ripoti ilionyesha kuwa tezi hizo zipo sawa hazina ugonjwa wowote. Mdai huyo alipopewa majibu hayo alienda nayo hadi katika hospitali ya Hindu Mandal na alipofika aliambiwa akamuone daktari aliyetajwa kwa jina moja la Mavunda ambaye alimweleza amekutwa na kansa ya Thyroid hivyo anatakiwa aende katika hospitali ya Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa ajili ya kuanza matibabu ya mionzi.

Anaeleza kuwa alipofika katika hospitali Ocean Road aliomba apimwe tena ili kujua kama ana tatizo hilo, ndipo walimwambia hawapimi upya kwa kuwa huwa wanategemea taarifa za mgonjwa kutoka hospitali husika.

“Nilipewa barua kutoka hospitali ya Hindu Mandal ili niende nayo hadi katika hospitali ya Ocean Road ili nianze matibabu ya mionzi,nilipofuatilia sikufanikiwa nikawa ninazunguushwa huku afya yangu ikiendelea kudhoofika huku ngozi yangu ikisinyaa kama mzee huku nywele zangu zikinyonyoka,” alidai Frorence.

Alidai baada ya kuikosa huduma ya mionzi alichukua uamuzi wa kukopa fedha benki na kuuza kiwanja chake huku ndugu zake wakimchangia fedha ili aweze kwenda hospitali ya Apollo iliyopo nchini India kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Baada ya kupata fedha hizo akaenda katika hospitali ya Hindu Mandal ili apewe barua pamoja na sampuli za tezi hizo aweze kwenda nazo katika hospitali ya Apollo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

“Nilipewa sampuli ambazo zilifungwa kama nilivyokabidhiwa, nilizipeleka moja kwa moja hadi katika hospitali ya Apollo iliyopo nchini India, zilifanyiwa uchunguzi na ilionekana sikuwa na kansa ya Thyoid,” alidai Frolence.

Anasema madaktari wa hospitali ya Apollo walibaini tezi yote ya Thyoid ya kushoto inayosaidia kutengeneza homoni imeondolewa wakati alipofanyiwa upasuaji huo katika hospitali ya Hindu Mandal, jambo ambalo limemsababishia ngozi yake kusinyaa na nywele kunyonyoka.

“Mimi nilikuwa najua nimefanyiwa upasuaji wa goita na sikuwahi kuambiwa na hospitali ya Hindu Mandal kama wamenitoa tezi, nimekuja kujua baada ya kuelezwa na hospitali ya Apollo ya nchini India kuwa kinachonisumbua ni upungufu wa homoni na siyo kansa.

Anadai hospitali ya Apollo ilimuandikia dawa za kuongeza homoni ambapo alielezwa katika maisha yake yote atakuwa anatumia dawa hizo, hatakiwi kuacha na asipofuata masharti hayo ngozi yake itasinyaa na nywele zitanyonyoka.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Rugemarila aliahirisha shauri hilo hadi Septemba 13,,2022 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi wa upande wa mdai.

Source: Mwananchi, July 24

=========

NB:NDO MAANA VIONGOZI NA MATAJIRI HAWATAKI KUTIBIWA NCHINI PIA HIYO FIDIA NAONA NI NDOGO SANA MAANA TEZI YA THYROID INA UMUHIMU MKUBWA MNO KWA MWILI WA BINADAMU NI KAMA WAMEPUNGUZA SIKU ZAKE ZA KUISHI.
Kwahii kesi, daktari hawataweza kumgusa maana hata maelezo yenyewe hayajanyooshwa. Pia mpaka ufikie kumshtaki daktari ni mpaka pathologist wajitetee ndio sasa yeye atafikiwa sasa. Kesi in medical wise bado haijajitosheleza kabisa kimaelezo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tena huku unapewa huduma hata usiyohitaji maadamu pesa iingie.Bora za serikali tafuta pesa yako mshike daktari au nesi mkono atakupa tiba sahahi, private ukienda ukosi ugonjwa utoki bure ni lazima ununue dawa
Unaweza andikiwa operation ya ubongo sababu unapiga chafya sana. Sasa ndugu zako ili kuchukua maiti hiyo bili watafurahi.
 
Napingana na wewe, margin for an error ikiwa kubwa kiasi hicho ina maana kipimo chako hakina calibration sahihi au msomaji/interpreter ni incompetent. Kutoka 2.8kg hadi over 5kg kwa kipimo cha ultrasound sio sawa, basi waking ultrasound imesoma havirleweki wangefanya sophisticated doppler effect. There's always a margin for an error, ikizidi sio error tena, ni mistake.
Sure ni mistake nakubali

Ila kwenye ya nani - hapo bro nasubiri majibu ya tume kama itaundwaga
 
Hili la dr ku-google siyo ukilaza wala jambo geni. Nimeliona mpaka majuu. Anakuwa anatafuta kutaka kujua zaidi na siyo kwamba anategemea google kumtibu mgonjwa. Tusiwe kama watu wasio na shule ukimwambia kuwa umesomea computer anategema ujue kila kitu kwenye computer kichwani mwako. Halfu kuna nchi nyingine matibabu yanaaongozwa na protocal fulani walizojiwekea na ziko kwenye database ambayo dr yoyote anaweza kui-access kwa mwongozo zaidi wakati anatibu. Hata ma-pilot wanatembea na reference zinazoelezea hatua za kutatua changamoto fulani na hawatakiwi wazikariri zote.
Hapo sasa tupo pamoja 👊
 
Uzi mchungu huu sjui kwann nmeusoma seems hamtambui jitihada za matabibu wa kiafrika kujali afya zenu kwenye mazingira duni ya vifaa
 
Kumbe ndo michezo hiyo. Me kabla sijameza dawa naigoogle naisoma weee, source tofauti tofauti na compare details. Nikiona haiendani na ugonjwa wangu simezi.
Safi, hicho ni kitu kizuri kwa asilimia nyingi.

Hapo mwishoni tu kwenye kutomeza ndio ningeshauri wasiliana na daktari wako kabla hujaamua kumeza au kukatisha dawa yoyote.

Na kama uliacha kisirisiri siku nyingine ukirudi kwake mwambie kabisa, ile dawa mimi sikumeza. Inaruhusiwa kabisa kukataa tiba ya aina fulani na kuomba kubadilishiwa matibabu na hata kubadilishiwa mtoa huduma. Haikatai wala.

Na kumbuka nilikuwa naongelea kesi ya mgonjwa kung'angana atibiwe malaria hata kama hana. Ndio nikasema malaria ina kingatiba, hivyo haikatai kuitibu hata kabla haijatokea [mfano SP za wajawazito]
 
Medical Negligence in Tanzania is the norm.

Tatizo amuelewi kipi kizuri kwenu; unakuta mtu hana ata ABC za usimamizi wa huduma za afya lakini anatukana jitihada za wengine.

Nilipowadharau watanzania ni majungu na kuacha Dr Gwajima atolewe hiyo wizara; sidhani wengi wetu tunaelewa how good she was kama angepewa backup ya raisi na serikali kubadili culture ya ufanyaji kazi kwenye hiyo wizara. She was more capable na alikuwa anajua kweli kweli yule ata ulaya anaweza simamia management ya ‘university hospital’.

Mtaalamu wa management ya afya wamempeleka social services kule sasa ndio anaropoka na kufura tu uelewa wa intervention za ile wizara ni mdogo sana.

Matatizo mengine tunajitakia wenyewe.
Gwajima aliyeacha utaalamu na kushabikia kujifukiza?
 
Dar es Salaam. Mfanyakazi wa Wizara ya Kilimo, Frorence Samwel anadai fidia ya Sh500 milioni Hospitali za TMJ na Hindu Mandal za jijini Dar es Salaam na daktari Moirice Mavura kwa kile anachodai kuwa ni uzembe katika kumtibu.

Pia amedai alipwe Sh53 milioni kwa ajili ya gharama mbalimbali, ikiwemo ya matibabu na usafiri.

Frorence amefungua kesi hiyo dhidi ya Dk Mavura pamoja na hospitali hizo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akidai kuwa hospitali hizo zilifanya uzembe alipokwenda kupata huduma ya matibabu.

Akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ramadhan Rugemalira huku akiongozwa na wakili wake Norbert Mlwale alidai kuwa Juni 27, 2018 alienda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na alifanyiwa uchunguzi wa koo ndipo alielezwa amuone Dk Moirice Mavura.

Alidai baada ya kumuona Dk Mavura alimwelekeza kuwa aende katika hospitali ya Hindu Mandal kwa kuwa ina vifaa vya kisasa kwa ajili ya upasuaji na anafanya kazi katika hospitali hiyo.

Shahidi huyo aliieleza mahakama hiyo kuwa Julai 9, 2018 Dk Mavura alimfanyia upasuaji katika koo lake na alitoa sampuli za tezi la kushoto zikapelekwa katika hospitali ya TMJ kwa ajili ya uchunguzi.

Alidai baada ya kufanyiwa uchunguzi wa sampuli hiyo hospitali ya TMJ ilitoa ripoti yake ikidai kuwa alikuwa na ugonjwa wa Rapillary Carcinoma of Thyoid ambayo alikabidhiwa Dk Mavura.

Baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo Dk Mavura alimfanyia upasuaji wa pili na kuiondoa tezi iliyoambukizwa ugonjwa huo.

Anaeleza kuwa baada ya kufanyiwa upasuaji huo zilichukuliwa sampuli za tezi zenye ugonjwa huo na zilipelekwa katika Hospitali ya TMJ kwa ajili ya uchunguzi mwingine ambapo ripoti ilionyesha kuwa tezi hizo zipo sawa hazina ugonjwa wowote. Mdai huyo alipopewa majibu hayo alienda nayo hadi katika hospitali ya Hindu Mandal na alipofika aliambiwa akamuone daktari aliyetajwa kwa jina moja la Mavunda ambaye alimweleza amekutwa na kansa ya Thyroid hivyo anatakiwa aende katika hospitali ya Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa ajili ya kuanza matibabu ya mionzi.

Anaeleza kuwa alipofika katika hospitali Ocean Road aliomba apimwe tena ili kujua kama ana tatizo hilo, ndipo walimwambia hawapimi upya kwa kuwa huwa wanategemea taarifa za mgonjwa kutoka hospitali husika.

“Nilipewa barua kutoka hospitali ya Hindu Mandal ili niende nayo hadi katika hospitali ya Ocean Road ili nianze matibabu ya mionzi,nilipofuatilia sikufanikiwa nikawa ninazunguushwa huku afya yangu ikiendelea kudhoofika huku ngozi yangu ikisinyaa kama mzee huku nywele zangu zikinyonyoka,” alidai Frorence.

Alidai baada ya kuikosa huduma ya mionzi alichukua uamuzi wa kukopa fedha benki na kuuza kiwanja chake huku ndugu zake wakimchangia fedha ili aweze kwenda hospitali ya Apollo iliyopo nchini India kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Baada ya kupata fedha hizo akaenda katika hospitali ya Hindu Mandal ili apewe barua pamoja na sampuli za tezi hizo aweze kwenda nazo katika hospitali ya Apollo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

“Nilipewa sampuli ambazo zilifungwa kama nilivyokabidhiwa, nilizipeleka moja kwa moja hadi katika hospitali ya Apollo iliyopo nchini India, zilifanyiwa uchunguzi na ilionekana sikuwa na kansa ya Thyoid,” alidai Frolence.

Anasema madaktari wa hospitali ya Apollo walibaini tezi yote ya Thyoid ya kushoto inayosaidia kutengeneza homoni imeondolewa wakati alipofanyiwa upasuaji huo katika hospitali ya Hindu Mandal, jambo ambalo limemsababishia ngozi yake kusinyaa na nywele kunyonyoka.

“Mimi nilikuwa najua nimefanyiwa upasuaji wa goita na sikuwahi kuambiwa na hospitali ya Hindu Mandal kama wamenitoa tezi, nimekuja kujua baada ya kuelezwa na hospitali ya Apollo ya nchini India kuwa kinachonisumbua ni upungufu wa homoni na siyo kansa.

Anadai hospitali ya Apollo ilimuandikia dawa za kuongeza homoni ambapo alielezwa katika maisha yake yote atakuwa anatumia dawa hizo, hatakiwi kuacha na asipofuata masharti hayo ngozi yake itasinyaa na nywele zitanyonyoka.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Rugemarila aliahirisha shauri hilo hadi Septemba 13,,2022 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi wa upande wa mdai.

Source: Mwananchi, July 24

=========

NB:NDO MAANA VIONGOZI NA MATAJIRI HAWATAKI KUTIBIWA NCHINI PIA HIYO FIDIA NAONA NI NDOGO SANA MAANA TEZI YA THYROID INA UMUHIMU MKUBWA MNO KWA MWILI WA BINADAMU NI KAMA WAMEPUNGUZA SIKU ZAKE ZA KUISHI.
Mbona 500m kidogo?
 
Pole sana. Mimi nina uvimbe shingoni upande wa kushoto.Nimeenda hospital tatu tofauti, chakushangaza wanachukua kipimo cha aina moja wanapeleka maabara majibu utaambiwa kesho. Majibu ya hospital zote yanatofautiana. The first told me is the goiter , the second Lipoma, the third gland. And their measure is three thousand and four hundred thousand. And all say that medicine is a surgeon .
 
Inaumiza, saa hizi ndugu yangu kabaki na mtoto mmoja kama wa dawa.
Lakini ovary si nzima? Kama ni hivyo, nadhani anawezankupata mtoto kupitia surrogate mother, kwani mayai yanaweza kutoewa kwenye ovary na kupandikizwa nje ya tumbo. Halafu anamkodi mama mwingine anambebea mimba. Maoni yangu mie sio daktari
 
Hapo wamekuingiza gharama ambazo hukutarajia.. Na pesa iwepo haipo je!?
 
Sio ndo

So ndo hapo ujakamilisha ushahidi kwann ummkamate mtu si umpe Dhamana aendelee na maisha yake huku akiendeleea na kesi nje, mfano check wazee wa escrow, wazee wa uhamsho bila makosa wamewaweka ndani miaka, then wanakuja sema hawana nia ya kuendelea na kesi. Kama hawana nia kwann wanawakamata watu mtu kukaa ndani familia yake nani anaitunza, mke wake je si vishawishi kuolewa na mtu mwingine, miaka 10 angekuwa na watoto wangapi amezaa, pangekuwapo na uwajibishwaji wa kulipa fidia kwa kukatwa mishahara yao na pensheni zao hakika Hakuna hakimu, waendesha mashtaka wangechezea maisha ya watu, check mfano mama wa watu zumarid mwaka unaenda sasa bila ushahidi kesi za kutunga tu kisha kawagomea police kwa kutofata utaratibu, then utasikia wamemuachia, mda wake nani ataulipa?
Uzembe wa kutojali ustawi wa watu wengine uko kila mahali kila angle kwenye nchi za afrika. Tazama tu hata vjongozi na watawala wanavyo tu treat
 
Kwakweli vijana wenye taaluma zao ni mzigo saivi
[emoji1787]

Unaenda kwa Dkt unamueleza tatizo yeye anachat kwenye simu.

Nawakubali professional waliokuwepo enzi za mkoloni, japo technology ilikuwa duni lakini walikuwa serious and meticulous na kazi zao.

Hii generation ya siku hizi ni majanga sio madaktari tu, hata wanasheria ( wavivu kusoma) wanagombezwa kila siku court kwa uzembe wao. Hali kadhalika na engineers, accountants etc so unprofessional [emoji706]

Daktari ana 'gugo' symptoms 😂😂😂
 
Ndio kilichobaki, tukianza kushitakiana kidoogo umakini utakuwepo, hatukatai kukosea ndio uwanadamu lakini ni too much.

Wale kenge wa dar group sijui, walifanya uzembe kiasi dada yangu akatolewa kizazi kabisa, ndugu zangu nawaambIa tuwashughulikie, wanasema mradi katoka salama, tuache tu., mtu kakosa mtoto na kizazi wametoa[emoji34]
Kwa namna yoyote inawezekana labda wameuza???
 
Dar es Salaam. Mfanyakazi wa Wizara ya Kilimo, Frorence Samwel anadai fidia ya Sh500 milioni Hospitali za TMJ na Hindu Mandal za jijini Dar es Salaam na daktari Moirice Mavura kwa kile anachodai kuwa ni uzembe katika kumtibu.

Pia amedai alipwe Sh53 milioni kwa ajili ya gharama mbalimbali, ikiwemo ya matibabu na usafiri.

Frorence amefungua kesi hiyo dhidi ya Dk Mavura pamoja na hospitali hizo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akidai kuwa hospitali hizo zilifanya uzembe alipokwenda kupata huduma ya matibabu.

Akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ramadhan Rugemalira huku akiongozwa na wakili wake Norbert Mlwale alidai kuwa Juni 27, 2018 alienda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na alifanyiwa uchunguzi wa koo ndipo alielezwa amuone Dk Moirice Mavura.

Alidai baada ya kumuona Dk Mavura alimwelekeza kuwa aende katika hospitali ya Hindu Mandal kwa kuwa ina vifaa vya kisasa kwa ajili ya upasuaji na anafanya kazi katika hospitali hiyo.

Shahidi huyo aliieleza mahakama hiyo kuwa Julai 9, 2018 Dk Mavura alimfanyia upasuaji katika koo lake na alitoa sampuli za tezi la kushoto zikapelekwa katika hospitali ya TMJ kwa ajili ya uchunguzi.

Alidai baada ya kufanyiwa uchunguzi wa sampuli hiyo hospitali ya TMJ ilitoa ripoti yake ikidai kuwa alikuwa na ugonjwa wa Rapillary Carcinoma of Thyoid ambayo alikabidhiwa Dk Mavura.

Baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo Dk Mavura alimfanyia upasuaji wa pili na kuiondoa tezi iliyoambukizwa ugonjwa huo.

Anaeleza kuwa baada ya kufanyiwa upasuaji huo zilichukuliwa sampuli za tezi zenye ugonjwa huo na zilipelekwa katika Hospitali ya TMJ kwa ajili ya uchunguzi mwingine ambapo ripoti ilionyesha kuwa tezi hizo zipo sawa hazina ugonjwa wowote. Mdai huyo alipopewa majibu hayo alienda nayo hadi katika hospitali ya Hindu Mandal na alipofika aliambiwa akamuone daktari aliyetajwa kwa jina moja la Mavunda ambaye alimweleza amekutwa na kansa ya Thyroid hivyo anatakiwa aende katika hospitali ya Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa ajili ya kuanza matibabu ya mionzi.

Anaeleza kuwa alipofika katika hospitali Ocean Road aliomba apimwe tena ili kujua kama ana tatizo hilo, ndipo walimwambia hawapimi upya kwa kuwa huwa wanategemea taarifa za mgonjwa kutoka hospitali husika.

“Nilipewa barua kutoka hospitali ya Hindu Mandal ili niende nayo hadi katika hospitali ya Ocean Road ili nianze matibabu ya mionzi,nilipofuatilia sikufanikiwa nikawa ninazunguushwa huku afya yangu ikiendelea kudhoofika huku ngozi yangu ikisinyaa kama mzee huku nywele zangu zikinyonyoka,” alidai Frorence.

Alidai baada ya kuikosa huduma ya mionzi alichukua uamuzi wa kukopa fedha benki na kuuza kiwanja chake huku ndugu zake wakimchangia fedha ili aweze kwenda hospitali ya Apollo iliyopo nchini India kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Baada ya kupata fedha hizo akaenda katika hospitali ya Hindu Mandal ili apewe barua pamoja na sampuli za tezi hizo aweze kwenda nazo katika hospitali ya Apollo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

“Nilipewa sampuli ambazo zilifungwa kama nilivyokabidhiwa, nilizipeleka moja kwa moja hadi katika hospitali ya Apollo iliyopo nchini India, zilifanyiwa uchunguzi na ilionekana sikuwa na kansa ya Thyoid,” alidai Frolence.

Anasema madaktari wa hospitali ya Apollo walibaini tezi yote ya Thyoid ya kushoto inayosaidia kutengeneza homoni imeondolewa wakati alipofanyiwa upasuaji huo katika hospitali ya Hindu Mandal, jambo ambalo limemsababishia ngozi yake kusinyaa na nywele kunyonyoka.

“Mimi nilikuwa najua nimefanyiwa upasuaji wa goita na sikuwahi kuambiwa na hospitali ya Hindu Mandal kama wamenitoa tezi, nimekuja kujua baada ya kuelezwa na hospitali ya Apollo ya nchini India kuwa kinachonisumbua ni upungufu wa homoni na siyo kansa.

Anadai hospitali ya Apollo ilimuandikia dawa za kuongeza homoni ambapo alielezwa katika maisha yake yote atakuwa anatumia dawa hizo, hatakiwi kuacha na asipofuata masharti hayo ngozi yake itasinyaa na nywele zitanyonyoka.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Rugemarila aliahirisha shauri hilo hadi Septemba 13,,2022 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi wa upande wa mdai.

Source: Mwananchi, July 24

=========

NB:NDO MAANA VIONGOZI NA MATAJIRI HAWATAKI KUTIBIWA NCHINI PIA HIYO FIDIA NAONA NI NDOGO SANA MAANA TEZI YA THYROID INA UMUHIMU MKUBWA MNO KWA MWILI WA BINADAMU NI KAMA WAMEPUNGUZA SIKU ZAKE ZA KUISHI.
Aseeeee
 
Back
Top Bottom