Mimi kuna Daktari wa kike pale Hurbert Kairuki nilimshinda kwa kutumia google tu kudadadeki, yaani alikuwa ana-force kumpa mwanangu dawa za kifafa wakati kwa ku-google kwa nusu saa tu nikagundua alichonacho mwanangu ni degedege, ila yeye anakomaan kwamba vipimo vya EEGg kitu gani sijui vinaonuesha sijui Hertz ngapi huko kwahiyo anakifafa..., tukapelekeshana hadi kwa madaktari wenzake ikabidi aanze kunikimbia..., na dawa walizompa zilikuwa za mwaka mzima.., sema niliwahi wakati ameshazitumia wiki tu, baada ya kukaa kikao na madaktari wengine wa hospitali hiyo hiyi ikabainika ni ‘febrile seizure’ kama ‘google’ ilivyosema.., na inprinciple huwa hawatoi dawa. Yule Dokta alikimbia hata hakuinekana kwenye kikao.., hakyanani.., kuja kucheki bili ya NHIF wamelamba 2 million!! Sema tu naogopa kuishtaki hospitali, maana nado nawahitaji sana.., huwezi jua lini utawarudia hapo.
Ila niliwaza sana, ni watu wangapi wasio na uwezo wa ku analyse mambo kwa kujiamini kama mimi kiasi wanamuona Daktari kama Mungu asiye na tamaa ya pesa ambao wanaweza kukuandikia dawa au procedure purely out of greed ya kukwapua pesa za bima.., yaani...