Mgonjwa kulipia 'Kumuona Daktari' Hospitali si sahihi

Basi kila sehemu ingekua hivyo tungefika? Mfano ukitaka kusafiri kwenda Morogoro ukiingia tu kwenye abood bus utoe pesa ya kumuona dereva wa basi then ulipie na nauli yako kwa konda
Your browser is not able to display this video.
 

Asante sana mkuu, kumbe nawe umeliona hilo!

Hizi hospital/clinic ni mtihani mkuu. Kufungua file tsh 5000, kumuona daktari 25000 na kwendelea. Ikiwa utakutwa na tatizo basi watakuambia tumia dawa flani, itakubidi dawa hizo uzinunue kwa gharama yako.

Next? Utaambiwa baada ya kumaliza dawa hizo utapaswa uendelee nazo au urejee hospital/clinic uonane tena na daktari, kisha utalipia kumuona daktari kwa mara nyingine, kwa hiyo utaendelea hivyo hivyo mpaka hali itakapokaa sawa. Mheshimiwa rais wa watu, mwenye imani na huruma aliangalie suala hili na alifanyie kazi.
 
Consultation fee unalipa ya nn wakati huyo daktari analipwa mshahara na mwajiri wake??
 
Ni consultation fees, mahali popote kama ni daktari ni lazima ulipe kwani ule ushauri ni sawa na dawa. Sema wapunguze.
 
kwa ivo madaktari wamegeuka kuwa KWA MKAPA!!!
 
Madaktari wamefunzwa kutengeneza pesa mahospitalini, na siku zote madaktari hujiona wao ni special sana ukiuliza oh! sijui wamesoma kwa tabu na miaka mingi. Na ubaya watu huwa na mitazamo ya kudhani madaktari wanajua kila kitu.
We kama unaona daktar hana umuhimu jitibu mkuu
 
Hela inaenda hata kama hujapata huduma yeyote ile..
Elewa kwamba matibabu yanaanzia pale kwenye maongezi ndo anajua shida ni nini achukue vipimo gani aje atoe matibabu gani
 
Huu uzi ndo unathibitisha kwenye watz wanne mmoja anakua ana matatizo ya akili
 
Naona wangepunguza au iwe sawa hospital zote ukitoa kabisa kutatokea usumbufu kila mmoja atataka kumuona daktar mwingine Hana ugonjwa ambao n serious lakin atataka kumuona Dr
 
Daktari Bingwa anasoma miaka zaidi ya kumi tena ukute amesomea hata nje ya nchi alafu wewe uje kumuona bure....
hivi wewe una akili kweli.
hata clinical officer aliyesomea miaka 3 haupaswi kumuona bure.

hebu heshimuni kazi za watu nyie
 
Kitu usichokijua ni kwamba kuonana na Dr ni muhimu Zaid maaana ni yeye atakayekuandikia vipimo kama inabidi, ni yeye utamrudishia vipimo akusomee majibu, ni yeye atakuandikia dawa kulingana na majibu ya vipimo vyako pia hata kama hatokuandikia vipimo Wala dawa atakushauri vizur tu nayo ni matibabu, Sasa kwann umuone bure?

Lakini ukitaka kujiepusha na hiyo consultation fee ya Dr unaruhusiwa pia kwenda hospitali yeyote ( za serikali excluded) na vipimo vyako ukalipia ukapima na majibu ukapewa ukaondoka nayo ukijua utampelekea nani.
 
Kumuona daktari. Humuangalii kama picha. Ile kumueleza tu shida yako naye akasuggest vipimo au dawa ndicho unacholipia. Kama unaona haina maana kumueleza mtaalamu shida zako jiandikie mwenyewe dawa au vipimo.
Na yeye akienda kwa Muhasibu pia alipie pesa kabla ya kumueleza shida zake au umekula maharagwe ya wapi wewe Dr magumashi?
 
Daktari Bingwa anasoma miaka zaidi ya kumi tena ukute amesomea hata nje ya nchi alafu wewe uje kumuona bure....
hivi wewe una akili kweli.
hata clinical officer aliyesomea miaka 3 haupaswi kumuona bure.

hebu heshimuni kazi za watu nyie
Nani kamlazimisha, si aachane na udaktari ajichimbie Sumbawanga akalime maparachichi au mahindi pia ni maisha?
 
Consultation fee unalipa ya nn wakati huyo daktari analipwa mshahara na mwajiri wake??
Kwani hiyo consultation inaenda kwenye mfuko wa Daktari.

Huyo anaemlipa Daktari ndiyo huyo huyo aliyeweka hiyo consultation, kwaajili yake Mwajiri mwenyewe.
 
We kama unaona daktar hana
umuhimu jitibu mkuu
Sijasema madktari sio muhimu bali madktari hujiona wao ndio special kuliko wengine na watu kudhani madaktari wanajua kila kitu kuhusu tiba, mnapenda mtukuzwe muonekane ni watu muhimu kuliko wengine kisa tu
nyie madktari mnajua kila kitu.
Kuna siku nusu tupoteze maisha ya bi mkubwa wangu kama nisingejiongeza na kubaki kutegemea mawazo ya daktari ambaye nilishaona kabisa alikuwa anacheza na uhai wa mtu.
 
Nani kamlazimisha, si aachane
na udaktari ajichimbie Sumbawanga akalime
maparachichi au mahindi pia
ni maisha?
Mimi mwenyewe nashangaa yani mtu alichagua mwenyewe kwenda kusomea udaktari bila kulazimishwa na lengo ni kuja kutibu watu ila ajabu analalamika kama vile amelazimishwa kusoma au kufanya kazi ya udaktari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…