Mguu wa gari kuvuma sana wakati wa mwendo

Mguu wa gari kuvuma sana wakati wa mwendo

Sawa mkuu ni kwamba wanaweka vibaya au ndio wataweka fake hizi mkuu?
Hata kama ni OG,uwekaji una umuhimu wake,
yaani wakati wa kupress wakikosea wakaibonyeza kwenye gololi
wanaiua ikiwa mpya. Ni muhimu sana kudeal na mafundi wanaojielewa.
 
Bearing ikiwekwa vizuri na pressing machine,hata kama ni mchina inadumu.
Kuna kipindi nilitaka kwenda nyumbani mkoani,nikaamua nibadirishe bearings zote kama maandalizi ya safari
nikauziwa bearing wakaniambia ni original na bei ikiwa juu.Wale wawekaji sasa na press machine za kutumia jeki.
wakaibonyeza mojawapo ya mguu wa mbele. Bahati nzuri ilinifikisha
kule wakasema hawana OG wana mchina.Nikaona sina namna waniwekee hiyo hiyo
ikawekwa kwa pressing machine nzuri,mpaka leo natumia sijabadilisha na imepita miaka zaidi ya miwili.
hapo sawa umenipa elimu nyingine kama Hawana press machine sitakubali maana napigaga masafa sana
 
Hata kama ni OG,uwekaji una umuhimu wake,
yaani wakati wa kupress wakikosea wakaibonyeza kwenye gololi
wanaiua ikiwa mpya. Ni muhimu sana kudeal na mafundi wanaojielewa.
ahsante sana mkuu nimeipata elimu nzuri
 
naichukua namba mkuu , naweza kupata wapi plug orginal
20241114_180745.jpg
 
wakuu gari yangu mguu mmoja wa kilia unavuma sana mpaka nakosa raha ya kusikiliza mziki tatizo itakuwa Nini nijue kabla ya kwenda Kwa fundi maiko
Pole sana kwa tatizo hilo! Kuna sababu kadhaa zinazoweza kusababisha mguu wa gari kuvuma sana:

Bearings: Inawezekana bearings za gurudumu zimechoka na zinahitaji kubadilishwa.

Brake Pads: Brake pads zilizochakaa zinaweza kusababisha kelele.

Suspension: Vipuri vya suspension kama vile shock absorbers au bushings vinaweza kuwa vimechoka.

Alignment: Alignment mbaya ya
magurudumu inaweza kusababisha kelele na mtikisiko.
Ni vyema kumpeleka gari kwa fundi ili afanye uchunguzi wa kina na kubaini tatizo halisi. Fundi Maiko atakusaidia kutatua tatizo hili kwa usahihi [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
wakuu gari yangu mguu mmoja wa kilia unavuma sana mpaka nakosa raha ya kusikiliza mziki tatizo itakuwa Nini nijue kabla ya kwenda Kwa fundi maiko
Tatizo ni Wheel bearings kuisha. Nenda kwa fundi ila jibu atakalokupa halitakuwa tofauti na hili.
 
Yes akabadili Bearing sijui za Brevis bei gani ila IST zinaanzia elfu 20.
Ni vizuri kuweka bearings za gharma ili angalau kuokoa pesa na downtimes, hizo beraings 20,000 zitakuwa zinakufa kila mara,
Bearing kuvuma ni moja ya "fail safe" feature za genuine bearings, za kichina hazikupi nafasi ya kuvuma, unastukia tu unalala porini baada ya tairi kuchomoka.
 
Sio aende kwa Salama Bearings kariakoo?
Salama ndo haswa anatakiwa aende , huko kwa authorized toyota dealer ni kutafuta presha zisizo za lazima. Unaweza ambiwa laki kadha kwa kitu cha 90 elfu salama.
 
Salama ndo haswa anatakiwa aende , huko kwa authorized toyota dealer ni kutafuta presha zisizo za lazima. Unaweza ambiwa laki kadha kwa kitu cha 90 elfu salama.
Akisogea Kisangani tu atacheka 😁
 
Ni vizuri kuweka bearings za gharma ili angalau kuokoa pesa na downtimes, hizo beraings 20,000 zitakuwa zinakufa kila mara,
Bearing kuvuma ni moja ya "fail safe" feature za genuine bearings, za kichina hazikupi nafasi ya kuvuma, unastukia tu unalala porini baada ya tairi kuchomoka.
duuh sawa nitazingatia kitafuta original mkuu
 
Salama ndo haswa anatakiwa aende , huko kwa authorized toyota dealer ni kutafuta presha zisizo za lazima. Unaweza ambiwa laki kadha kwa kitu cha 90 elfu salama.
hatari mno
 
wakuu gari yangu mguu mmoja wa kilia unavuma sana mpaka nakosa raha ya kusikiliza mziki tatizo itakuwa Nini nijue kabla ya kwenda Kwa fundi maiko
wheel bearing imechoka. Badilisha za pande zote mbili; baadaye gari litakuwa linayumba sana utashindwa kulicontrol
 
Back
Top Bottom