Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?


Hii thread inaonyesha jinsi ilivyopangwa kumsafisha mtu, ikapanginga. Kwa nini anakazana hivyo kujisafisha? Watu si wataona ukweli? Uadilifu wa mtu haujifichi. Alichowachukulia watz kinatosha
 
Ile njemba hatari bana mie nafikiri baadhi ya pesa ilizaliwa nazo
Ni malipo aliyoyapata na anayoendelae kuyapata toka shamba la marehemu TANZANIA km mmoja aliwahi kusema humu shamba la marehem halinya mwenyewe ni tofauti na shamba la bibi
 
Ni malipo aliyoyapata na anayoendelae kuyapata toka shamba la marehemu TANZANIA km mmoja aliwahi kusema humu shamba la marehem halinya mwenyewe ni tofauti na shamba la bibi

kweli mukubwa kuna baadhi ya watu washaona hii nchi isivyo na mwenyewe wameamua kuila wenyewe kilainiiiiiiii
 
Yapo mambo mengi, fuatilia Mawala advocates, nenda Singita Grumeti (serengeti) nenda vodacom, nenda jengo la south african tz embassy, n.k n.k
 

Mkuu Pasco... taratibu! biashara kubwa halali sawa hatukatai lakini je hela ya kwanza ya kanzisha biashara hizi ilitoka wapi?

historia ya Mheshimiwa wetu huyu siyo ndefu -amekua mbunge na waziri mwaka 90' kabla ya hapo amekaa AICC mwaka 1 tu kama Director na wakati huo tunajua umaskini wa mawaziri wetu wa awamu ile.(ukilinganisha na hawa mawaziri wa utandawazi wanaokua matajiri wakubwa ndani ya mwaka tu). EL 95' anagombania Urais kwa mbwembwe na anasemekana ni tajiri mkubwa. sasa hapa kuna grey areas nyingi sana.

EL hajawahi kua mfanyabiashara kabla ya siasa na hapa hata ameanzisha makampuni kibao makubwa tunakua na wasi wasi na hela ya kwanza ya uwekezaji huu ilitoka wapi na je ni halali? (mfano mkopo kama alivyodai tajiri sumaye) bila ya majibu haya tunajua tu kapata mtaji kwa ufisadi kama akina Yona, Mramba, Ngeleja, Mkulo, etc sema yeye kawazidi hawa kwa kua na "akili" zaidi za kuwekeza.
 
Tangu nianze kusikia lowasa anachangia taasisi mbali mbali na kutoa misaada ni siku nying mno, Kitu ambacho kinanitatiza ni kwamba pesa hizi anazitoa wapi wakati wabunge wanalalamika kila siku pesa hazitoshi.
Maswali yangu ni haya
1. Lowasa anafanya kazi zaidi ya ubunge (MB)?
2. ni mfanyabiashara wa aina gn?
3. Je zaidi ya ule ufisadi wa umeme, naye alijiuzia kiwanda chochote hapa tanzania?

Naomba wenye taarifa kamili tujuzane hapa
 
Anamiliki maduka ya kuosha nguo (dry cleaner), ana kampuni ambayo ni moja ya mawakala wakubwa wa Voidacom, ni mfugaji, anamiliki majumba kadhaa makubwa Dar es Salaam na pesa nyinmgine anaipata kwa kuwachangisha marafiki zake
 
Nami sina uhakika sana Ila huwa nasikia kuwa anamiliki kampuni kadhaa za magazeti hapa nchini, ngoja wajuaji wa mambo watatujuza zaidi
 
Hiyo ya hisa kwenye mojawapo la vodacom nililisikiaga hilo, vp katika umiliki wa magazeti?
 
Anafanya kazi kwa bidii tofauti na waswahili wengi ambao kazi yao ni kupiga umbeya na majungu tu na mwisho wanakufa wakiwa maskini...inaonekana na wewe ni mmoja wao!
 
jiulize kwa nini nchi maskini mnauza madini etc pesa zinaenda wapi jiulize
 
Unauliza mateke polisi
kwani hujui kama hizo pesa alituibia sisi
na vizazi vyetu
au we c mtanzania?
 
Anafanya kazi kwa bidii tofauti na waswahili wengi ambao kazi yao ni kupiga umbeya na majungu tu na mwisho wanakufa wakiwa maskini...inaonekana na wewe ni mmoja wao!
Swala ni kwamba utajiri wake unasababishwa na nn, Nafikiri kujua mtu tajiri anafanyaje mapaka anafanikiwa ni njia sahihi pia ya wewe pia kuanza kuwa tajiri,, changia mda mkuu
 
Ninachojua ni kwamba alichotaga pesa ya kutosha alipokuwa AICC na kuzi-invest ktk miradi mbalimbali kama ilivyotajwa hapo juu na MPITA NJIA. Na ndio sababu mwalimu alikuwa hampendi na aliwahi kumuuliza "kijana mdogo umepata wapi utajiri wote huu ktk kipindi kifupi hiki". Nasikia lile li cultural heritage pale Arusha ni lake, hata Leopard tours pia yake!

Halafu ktk kipindi chake cha uwaziri mkuu napo alikusanya za kutosha! si mnajua alivyo mwizi mchapakazi?

Kifupi ni mtu ambaye yuko strategic na mambo yake. Ndo maana hata ana uwezo wa kuwachangisha marafiki zake pesa. Lakini ujue lengo ni lile lile kwamba akishapata nafasi wanakula pamoja na hao wanaomchangia, whether kihahali au isivyo halali kupitia tender mbalimbali za serikali, plus mikataba isiyo na tija kwa taifa.
 
Anamiliki maduka ya kuosha nguo (dry cleaner), ana kampuni ambayo ni moja ya mawakala wakubwa wa Voidacom, ni mfugaji, anamiliki majumba kadhaa makubwa Dar es Salaam na pesa nyinmgine anaipata kwa kuwachangisha marafiki zake
Anamiliki Kampuni ya Event planning and management ya ENDEPA, Kupitia mwanae Pamela inalipa si kitoto.
 
Sina cha kuchangia, lakini niulize malengo ya huyu bwana kuchangia namna hiyo ni yepi?

Kama ni mema, sawa lakini kama analingine kwa jinsi alivyochafulika kwa kashfa ya richmond hata ajisafishe kwa omoplus ni kazi bure, magogoni kuingia ni vyepesi kwa tembo kupenya tundu la sindano kuliko yeye kukalia kiti cha enzi.
 
Kwani Nyerere ndio kipimo cha kila kitu?Nyerere ni maskini kwa hiyo hawezi kukubaliana na mtu mwenye utajiri.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…