Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?

Lowasa? Akafie mbali na richmond. Tutakutana naye siku ya ufufuo. Mbona mahangaiko ya watanzania hayawatii aibu hawa wanafiki?
 

Pasco, haihitajiki kwa watu kuiona risiti ya shilingi ngapi mmelipwa ili kusafisha kitu ambacho (kama) ni kisafi......! Hakika fedha inaweza kubadili chumvi kuwa sukari.....!

Ombi langu nikuwa tugawieni na wengine....pengine tutanyamaza kama hatutaki kukubaliana na nyie....vinginevyo bora vita ije kila mtu achukue chake.

Kibanga Msese
 
PASCO,Naomba nitofautiane na wewe kidogo kimtazamo.siyo ccm ndio waliwasadikisha watu kuwa kila tajiri ni fisadi.katika Nchi ya masikini wa kipato wengi,kila mwenye nacho huonekana machoni pao kama fisadi vile.wao hudhani pengine hawa walionacho(the haves) wamepata kwa kuwadhurumu wasio nacho (the have nots).usishangae kuona hata mtumishi wa umma ambaye hana hata sehemu ya kuchakachua,akifanya bidii akachuma mali kwa njia halali bado ataonekana ni FISADI.hata wewe kama unamiliki gari na nyumba kuna watu wanakuona ni FISADI.
Kama mtu amekuwa kwenye politics kwa takribani miaka 40 atashindwaje kuwa tajiri kama ana wekeza utajiri na mali zake vizuri? mimi ningeshangaa kama angekuwa masikini. unawezaje kuwa waziri miaka yote hiyo halafu ubaki kuwa masikini?
 
.
Mkuu Jerusalem, umenikumbusha jambo moja la maana sana kuhusu "the haves" na "the have not". Mimi nimefanya kazi ya uandishi wa hanari kwa miaka 15 sasa!, kwa mujibu wa kipato changu, au cha mwandishi, bado huwezi kumiliki nyumba wa gari!, mimi bado naishi nyumba ya kupanga na usafiri ninao miliki ni boda boda!. Kutokana na level ya waandishi kuwa ni "the have not" kwa sana, mimi na hicho ki boda boda changu, naonekana ni fisadi miongoni mwa wanahabari!, na tena kwa vile siku hizi siandiki sana, bali nina visambaza vile vibahasha kwa waandishi wenzangu wa wakati wa baadhi ya matukio ya bahasha kihalali, ni basi mimi naonekana fisadi!.

Huku waandishi wenzangu wakiniona fisadi, humu jf naonekana ni njaa kali eti kwa vile namtetea EL!, wakijiaminisha kwa vile EL ni fisadi, anavitumia vijihela vyake kutulipa watu wenye njaa kama mimi ili tumsafishe humu jf!.

Lazima ni kiri, wengi wa wana jf wa kawaida, they belong to this group la "the have not", matokeo yake wana chuki za ajabu kwa kila mwenye chochote kitu!. Wengi ni hate preachers" na "prophets of the doom"!.
 
pasco una mahaba na lowassa,lowassa alishindwa kumwambia nyerere alivyopata mali zake!na huoni kumiliki hayo makampuni akiwa kiongozi mwandamizi serikalini kuna conflict of interest au undue influence?

huyu jamaa ana vibaraka weli hasa wale wanaoshindwa kupata hata mlo wa siku. Msiwashangae
 
Lowassa kama mwanaume, mkuu wa familia yake akitengeneza hela kwa ajili yake, na familia yake ni mfano wa kuigwa na siwezi kua na chuki nae binafsi. Watz wengi ni maskini, hawana elimu na wamelala, Lowassa peke yake hawezi ibadilisha Tanzania hata kwa miaka 20, sasa kwa nini asipige deal wakati kila mtu anakula kivyake huku sisi wananchi tumelala?

angekua baba yako na asingeiba ungemdharau na kumchukia kwa kupoteza opportunity ya kua tajiri ndani ya mfumo ulioharibika wenye kuweka mbele maslahi binafsi.

abarikiwe zaidi,
 

By the way, who is Lowassa?

Vide: Edward Lowassa - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Lowassa FISADI, MWIZI, JAMBAZI, hawezi nishawishi kwa namna yoyote nimuunge mkono! Hafai kuongoza Watz.
kwa kweli watu ambao wanamuunga mkono lowassa..wanamatatizo kichwani mwao!!!inakuwaje watu ambao ni wasomi munafikia hatua ya kumuunga mkono lowassa ,mtu ambae ni fisadi,tapeli,...kuwa kiongozi mkubwa wa nchi hiii???kama EL ni best ndani ta ccm basi kweli ccm imekufa.Na kama magamba mukimssimamisha huyu AJUZA,basi njia nyeupe kwa cdm kuchukua dola.MUNGU IBARIKI CCM ,KWA KUMSIMAMISHA FISADI ILI CDM TUSIPATE TABU YA KUPIGA KAMPUNI KWA UTUMIA CHOPPER
 
huyu jamaa ana vibaraka weli hasa wale wanaoshindwa kupata hata mlo wa siku. Msiwashangae
Kwakweli jitu kama lowassa kulitetea mbele ya uuma ni tabu sana.Na hta huyu PASCO anakuwa na mahaba na EL kwasababu hatuonani zaidi ya maandishi na majina ya uungo.,kama ingekuwa mbele ya kadamnasi/audience basi huyu jamaa hazingeweza hta kidogo kumtetea,.
 
Pasco, upo sahihi El-nino anatisha njia ni nyepesi, wanaokashifu busara ni hafifu lakini mwisho wa siku El atafika panapostahili Magogoni
 
Ninachojua kuhusu Lowasa:
  1. Baba yake Edward alikuwa karani mtoza ushuru hapo Monduli. Lowasa ni Muarusha, siyo Mmasai.
  2. Lowasa si jina lake halisi. Lowasa ni kimasai maana yake ikiwa ni maringo. Edward alikuwa akijidai sana wakati akiwa mwanafunzi. Ni kutokana na tabia hiyo wamasai wakamwita Maringo, yaani Lowasa.
  3. Katikati ya miaka ya 1970 mara baada ya kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam (akiwa na akina Kinana, Kikwete, Jenerali Ulimwengu, Mkuchika, Bagenda, Chimotto (r.i.p) na wengineo) Nyerere alimwanini Lowasa na kumkabidhi jukumu la kujenga nyumba ya ofisi ya TANU ya mkoa wa Arusha. Badala ya kujenga ofisi ya chama Lowasa alijenga nyumba yake binafsi na kumkasirisha Nyerere. Lowasa alipewa adhabu ya kufukuzwa kwenye chama, lakini baadaye alikuja kuokolewa na Sokoine baada kumshawishi Nyerere amsamehe.
  4. Akiwa waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo mijini, Lowasa alishiriki kuvuja shirika la Msajili wa Majumba na umiliki wake kuhamishiwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Lowasa alitumia udhaifu wa serikali ya Mwinyi kujimilikisha majumba ya msajili, na hata mengine kuyauza, hasa kwa wahindi, na kujirunikia mali. Hadi sasa, Lowasa anamiliki angalao jumba moja katika kila mji wa makao makuu ya mkoa, Tanzania bara.
  5. Kazi ya kuratibu wizi wa majumba na viwanja likuwa ikiratibiwa na Makere (B.Com/UDSM 1991) aliyekuwa anatumia kijumba cha Lowasa kilichopo mbele ya Patel Building (kwenye mbuyu) karibu na show room ya magari ya Conti-Cars.
  6. Wakati wa mafurika ya 2007 yaliyoezua daraja kati ya Msoga na Lugoba, akitumia madaraka ya waziri mkuu, Lowasa aliagiza TACRA kutoa 39bn/- kwa ajili ya kukarabati barabara ya Bagamoyo Msata kwa ajili ya matumizi ya dharura. Barabara hiyo haikujengwa na Lowasa alielekeza pesa hiyo ipelekwe kwingineko (anajua yeye).
  7. Mara tu baada ya kuwa Waziri Mkuu, 2006 Lowasa alibuni mradi wa kutengeneza mvua akishirikiana na WaThailand. Mvua haikutengenezwa na Lowasa alimwagiza Katibu Mkuu, wizara ya Miundombinu kuidhinisha malippo ya 11bn/ kuwalipa wataalam wa kutengeneza mvua kupitia ofisni kwake. Katibu Mkuu alipojaribu kushauri kuwa mradi huo haukuwa katika bajeti ya 2007/2008, Lowasa alimkumbusha kuwa yeye ndiye mtendaji mkuu (mwajiri wa Katibu Mkuu) wa shughuli za Serikali hivyo melekezo yake ni amri. Katibu Mkuu alinywea na kuidhinisha malipo husika kupitia ofisi ya waziri mkuu na kwa maelekezo yake.
  8. Richmond.................... kila Mtanzania mweneyekuelewa anafahamu kilichotokea.
  9. Jengo na kiwanja cha UVCCM.......................... Nnape Nauye na Emmanuel Nchimbi wanafahamu zaidi kilichotokea na Lowasa alipata kiasi gani kutoka kwa Patel.
  10. Kampuni yake ya AlphaTel ni muuzaji wa vodacom scratch vouchers; turnover yake 4bn/- kwa siku.
  11. Taarifa za regular disbursements kutoka Halmashauri za Wilaya/Miji/Manispaa na/au Jiji zilizokuwa zikiratibiwa na Wakurugenzi Watendaji aliowateua na kuwajibika kwake, na pesa hizo kuelekezwa kuwekwa katika account zake tutaziweka baadaye....
 

Nyekundu: Usipende kusema mambo ambayo huwezi kudhibitisha.... maana huwezi kumuita Mungu hapa jukwaani au mahala popote pale hapa dunia atudhibitishie hilo. Vinginevyo huyo mungu unayensema awe yule wa kufungiwa kwenye chupa.

Zambarau: Vibwagizo vingine vinapaswa kusemwa katika saluni za kike ambazo zinapendwa na wadada wanopenda uvivu wa kufikiri.
 
sijamuaona akifanya harambee ya kwa ajili ya ccm ,namuona mara nyingi makanisani ,pesa hizi tujue anatoa mfuko upi wa koti ,wapo viongozi wengi na wa miaka mingi hawajaonesha hadhira kama wana fedha nyingi .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…