Bahati Risiki
JF-Expert Member
- Jun 20, 2012
- 530
- 93
Lowasa? Akafie mbali na richmond. Tutakutana naye siku ya ufufuo. Mbona mahangaiko ya watanzania hayawatii aibu hawa wanafiki?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
PASCO,Naomba nitofautiane na wewe kidogo kimtazamo.siyo ccm ndio waliwasadikisha watu kuwa kila tajiri ni fisadi.katika Nchi ya masikini wa kipato wengi,kila mwenye nacho huonekana machoni pao kama fisadi vile.wao hudhani pengine hawa walionacho(the haves) wamepata kwa kuwadhurumu wasio nacho (the have nots).usishangae kuona hata mtumishi wa umma ambaye hana hata sehemu ya kuchakachua,akifanya bidii akachuma mali kwa njia halali bado ataonekana ni FISADI.hata wewe kama unamiliki gari na nyumba kuna watu wanakuona ni FISADI.Jamii01, fuatilia thread za Lowassa humu utaziona mpaka mali zake zimeorodheshwa!. Lowassa ni tajiri wa ukweli aliyepata mali zake zote kihalali na ndio maana amezisajili zote kwa jina lake na la mkewe Rejina!.
Ila hakuna ubishi CCM imegubikwa na ufisadi hali inayopelekea kila yeyete mwenye chochote kitu kuonekana fisadi.
Lowassa ni miongoni mwa wanaitwa mafisadi wakuu kufuatia kukubali kulibeba lile zigo kubwa la Richmond ili kumnusuru best wake na chama chake na aibu ya mwaka, hivyo yeye kuchafuka kwa kukubali kujitwisha msalaba wa ukombozi na salama ya CCM!.
Anachokifanya huko makanisani na kwenye michango mbalimbali ni kuonyesha uwezo wake kwenye kitu kinachoitwa mass mobilization kwa ajili ya kujiletea maendeleo, kitu ambacho JK ameshindwa kabisa!.
Hilo la kuandikwa magazetini, na kwenye vyombo vya habari, ni kufuatia EL kuwa na mvuto wa ajabu uliotoka kwa Mungu. Kila asemalo linamantik kwa hali ilivyo sasa!. Lowassa ni photo genic!, akipigwa picha anapendezea!, akiongea anavutia kumsikiliza!, na kikubwa zaidi yeye sio mtu wa maneno maneno na vitendo sifuri kama JK, yeye ni mtu wa maneno mafupi na vitendo virefu.
Wakuu wengi waliopo wakisikia JK atatembelea mahali, huandaa taarifa safi, mkuu akifika, akishasomewa taarifa, hupiga makofi na kuendelea na ziara!. Enzi za Lowassa akishasomewa taarifa huipokea na kuelekea physically kuyaangalia hayo yaliyozungumziwa!. Hivyo watu wakisikia JK anakuja, hukaa miguu juu, ila wakisikia ni Lowassa!, kijasho huwa kinawatoka maana jamaa hakubali kabisa longo longo yoyote!.
Ni kufuatia utendaji huu ndio maana mimi na wenzangu wachache humu jukwaani, tumeamua kujitolea kumsafisha Lowassa na ule uchafu wa Richmond, tunamtaka alitue hilo zigo amkabidhi mwenyewe, na yeye ndie ateuliwe kuwa mgombea wa CCM tumpigie debe, aingie Ikulu!.
.PASCO,Naomba nitofautiane na wewe kidogo kimtazamo.siyo ccm ndio waliwasadikisha watu kuwa kila tajiri ni fisadi.katika Nchi ya masikini wa kipato wengi,kila mwenye nacho huonekana machoni pao kama fisadi vile.wao hudhani pengine hawa walionacho(the haves) wamepata kwa kuwadhurumu wasio nacho (the have nots).usishangae kuona hata mtumishi wa umma ambaye hana hata sehemu ya kuchakachua,akifanya bidii akachuma mali kwa njia halali bado ataonekana ni FISADI.hata wewe kama unamiliki gari na nyumba kuna watu wanakuona ni FISADI.
Kama mtu amekuwa kwenye politics kwa takribani miaka 40 atashindwaje kuwa tajiri kama ana wekeza utajiri na mali zake vizuri? mimi ningeshangaa kama angekuwa masikini. unawezaje kuwa waziri miaka yote hiyo halafu ubaki kuwa masikini?
pasco una mahaba na lowassa,lowassa alishindwa kumwambia nyerere alivyopata mali zake!na huoni kumiliki hayo makampuni akiwa kiongozi mwandamizi serikalini kuna conflict of interest au undue influence?
Ni mwizi wa siku nyingi.Hata Nyerere alimwonya aache wizi lakini hakusikia.Sasa anatumia hela ya wizi kutaka Urais.kwa kifupi ni bepari ndio maana ana hela kiasi hicho .
Najiuliza na kukosa majibu Mh.Lowasa si mfanyabiashara,zaidi ya kuwa mbunge,nimejionea siku za hivi karibuni katika vyombo vya habari akichangia mambo mengi hasa katika miradi ya maendeleo na katika taasisi binafsi na zamakanisa.Huyu mweshimiwa pesa anazitoa wapi?
Je alikwisha tangaza mali zake hadharani? na kipato chake kiko vipi?Alipokuwa waziri katika awamu ya tatu kwa nini akufanya hivyo?na alipokuwa waziri mkuu kwa nini alishidwa kufanya hivyo? Na kwa nini safari zake na hotuba zake zinapewa umuhimu mkubwa katika vyombo vyetu vya habari?
kwa kweli watu ambao wanamuunga mkono lowassa..wanamatatizo kichwani mwao!!!inakuwaje watu ambao ni wasomi munafikia hatua ya kumuunga mkono lowassa ,mtu ambae ni fisadi,tapeli,...kuwa kiongozi mkubwa wa nchi hiii???kama EL ni best ndani ta ccm basi kweli ccm imekufa.Na kama magamba mukimssimamisha huyu AJUZA,basi njia nyeupe kwa cdm kuchukua dola.MUNGU IBARIKI CCM ,KWA KUMSIMAMISHA FISADI ILI CDM TUSIPATE TABU YA KUPIGA KAMPUNI KWA UTUMIA CHOPPERLowassa FISADI, MWIZI, JAMBAZI, hawezi nishawishi kwa namna yoyote nimuunge mkono! Hafai kuongoza Watz.
Kwakweli jitu kama lowassa kulitetea mbele ya uuma ni tabu sana.Na hta huyu PASCO anakuwa na mahaba na EL kwasababu hatuonani zaidi ya maandishi na majina ya uungo.,kama ingekuwa mbele ya kadamnasi/audience basi huyu jamaa hazingeweza hta kidogo kumtetea,.huyu jamaa ana vibaraka weli hasa wale wanaoshindwa kupata hata mlo wa siku. Msiwashangae
......
Hilo la kuandikwa magazetini, na kwenye vyombo vya habari, ni kufuatia EL kuwa na mvuto wa ajabu uliotoka kwa Mungu. Kila asemalo linamantik kwa hali ilivyo sasa!. Lowassa ni photo genic!, akipigwa picha anapendezea!, akiongea anavutia kumsikiliza!, na kikubwa zaidi yeye sio mtu wa maneno maneno na vitendo sifuri kama JK, yeye ni mtu wa maneno mafupi na vitendo virefu......