Fursa Pesa
JF-Expert Member
- May 30, 2012
- 4,631
- 3,527
Ni vizuri Lowassa ukawa mkweli. Sema "Nina pesa na watu" Hivi mtu asiyekuwa na pesa anaweza akawa anatoa mamilioni yote hayo katika harambee mbali mbali? Kwa maisha ya kitanzania unahadhi ya kuitwa Milionea. Hivi kama una pesa na ni halali kwanini unakwepa kusema nina pesa na watu wanaoniunga mkono? Be honest EL!
Umempa ukweli wenyewe, ubarikiwe sana.
Wanasiasa kwa uongo wamekubuhu! Kama hana hela hizo milion kumi kapata wapi? Na sio hizo tu sehemu nyingi ikiwemo makanisani huwa anatoa pesa. Hata hao watu wanajua atachangia ndo maana wanamualika mara kwa mara, sjui ndo anatakatisha pesa ya Richmond atajua mwenyewe ila pesa anayo sana asituongopee
Uko nafasi gani kwenye timu yake ya 2015?hakuna ukweli hapo! We mbona umekwisha barikiwa na hauna kitu.Kiukweli pesa hazina maana yoyote kama hakuna watu.Ndio maana hoja yake Ndg.Lowassa imetanguliza watu kwanza fedha baadae.
Teh teh teeeeeh...... Nkuu unashituka leo? Tayari CCM haina chake 2015, kumbe ulikuwa hujui? lakini tena CCM hawawezi kuwakoromea kwa sababu ili kupata nafasi kama hizo kupitia ccm lazima uwe na uwezo wa kuhamasisha watu wanunulike ndo unakuwa MWENZETU, haiwezekani upate bure kwani hapendwi ntu ndani ya ccm. Lakini rushwa na watoe tu, tena waje na kwengu kwa sababu wanawawezesha wasio nacho wapate msimu huu wa mavuno wala usiwaonee mtima nyongo-Siyo siri kwamba wasaka urais wawili wakubwa ndani ya CCM, January Makamba na Edward Lowassa, wamekuwa wakizunguka nchi wakigawa mamillioni ya fedha kwa wananchi ili waungwe mkono katika mbio zao za urais 2015
-Siyo siri kwamba Bw. Makamba Jr. Alikuwa mtumishi wa umma wa kawaida, lakini baada ya muda mfupi, huyu kijana amatokea kuwa na ukwasi mkubwa wa kifedha kiasi kwamba anadhamini vijana, na makundi mengi huku akigawa rushwa za waziwazi. Zanzibar aligawa simu aina za Samsung Galaxy S3 ambazo zinagharimu zaidi ya Tsh 700,000 kwa zaidi ya vijana 200 wa UVCCM. Kwa mahesabu ya juu juu, thamani ya simu 200 ni million 140. Hizi fedha amezitoa wapi January Makamba?
-Naye mzee Lowassa licha ya kwamba jimboni kwake ni masikini wa kutupwa, amekuwa akizunguka nchi nzima akigawa mabillioni makanisani na kwenye misikiti. Hizi fedha naye kazitoa wapi? Hawa watu wanatafuta nini Ikulu? Kwa nini CCM inyamazie tabia za hawa watu? January akumbuke kwamba ubunge wake aliupata kwa hila baada ya babake Mzee Yusuf Makamba kumfanyia hila Mzee. Shelukindo
-Naitahadharisha chama changu CCM kwamba, ikiwa itafanya makosa ya kuwapitisha hawa watu wawili ambao wanazunguka nchi wakigawa rushwa hadharani bila vyombo vya dola kuwahoji, nitafanya maamuzi magumu ya kuongoza uasi ndani ya CCM ili tuwape wananchi njia mbadala ya uongozi, hata kama itamaanisha kuwaunga mkono viongozi safi wa upinzani. Hawa vinara wawili siyo tu wanakiuka miiko na maadili ndani ya CCM, kwa maana kwamba muda wa kampeni bado, kadhalika wanavunja sheria za nchi kwa kugawa rushwa.
-January hajawahi kuchaguliwa kwenye cheo chochote kile hata ubunge, lakini badala ya kufuata njia halali, yeye anaendekeza rushwa huku akimpiga majungu waziri wake pale wizara ya Sayansi na Teknolojia. Natokea jimboni Bumbuli, lakini cha ajabu, Mzee Makamba na Mwanaye wanatangaza jimboni kwamba January Akiwa Rais Tanga itakuwa kama Singapore? Really? Tutafika kweli kwa mwendo huu? Hawa jamaa wanakimbilia ikulu kufata nini?
Haka kadogo kwanza niweke wazi ,mpaka leo sijawahi kumuona Makamba kama mtu anayefaha kuwa katika hiyo nafasi ukiachia kubebwa bebwa na jina la familia,lakini pili huyu dogo ni mzigo uliobaki CCM na atawasumbua kwasababu ana tabia kama za Zitto,wote ni watu wa uchu na wako radhi kufanya lolote na ndo walivyokuwa wakijiimarisha kwa pamoja sema sasa mwenzie CDM wameshtuka na kumshughurikia ..nawapeni pole CCM kwani majanga mnayo mengi na hizi pesa zitawagharimu na siku si nyingi mjiandae kumpokea na Zitto
-Siyo siri kwamba wasaka urais wawili wakubwa ndani ya CCM, January Makamba na Edward Lowassa, wamekuwa wakizunguka nchi wakigawa mamillioni ya fedha kwa wananchi ili waungwe mkono katika mbio zao za urais 2015