Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?

Ni vizuri Lowassa ukawa mkweli. Sema "Nina pesa na watu" Hivi mtu asiyekuwa na pesa anaweza akawa anatoa mamilioni yote hayo katika harambee mbali mbali? Kwa maisha ya kitanzania unahadhi ya kuitwa Milionea. Hivi kama una pesa na ni halali kwanini unakwepa kusema nina pesa na watu wanaoniunga mkono? Be honest EL!

Pesa bila watu ni ubatili mtupu na kujilisha upepo.Kiukweli kauli yake iko sawa kwani watu ndio pesa ishi na watu vizuri upate pesa.
 
Umempa ukweli wenyewe, ubarikiwe sana.

hakuna ukweli hapo! We mbona umekwisha barikiwa na hauna kitu.Kiukweli pesa hazina maana yoyote kama hakuna watu.Ndio maana hoja yake Ndg.Lowassa imetanguliza watu kwanza fedha baadae.
 
Wanasiasa kwa uongo wamekubuhu! Kama hana hela hizo milion kumi kapata wapi? Na sio hizo tu sehemu nyingi ikiwemo makanisani huwa anatoa pesa. Hata hao watu wanajua atachangia ndo maana wanamualika mara kwa mara, sjui ndo anatakatisha pesa ya Richmond atajua mwenyewe ila pesa anayo sana asituongopee

Mwizi ni mwizi hakuna hata siku moja atakiri kuwa ni kibaka.
Huyu Lowassa nani asiyemjua kuwa ni mtu wa michongo. na bahati yake ni kwa kuwa bwana fastjet naye anahangaika na mambo mengine , la sivyo huyu bwana angekuwa ananyea debe kwenye nchi za wenzetu ambazo kwao wizi ni adui nambari wani
Sasa huyu baba akili yote iko kwenye Urais , nani ampe labda atawale visiwa vya mafia.
CCM ntawona hawana akili wakimpendekeza huyu baba mamvi
 
hakuna ukweli hapo! We mbona umekwisha barikiwa na hauna kitu.Kiukweli pesa hazina maana yoyote kama hakuna watu.Ndio maana hoja yake Ndg.Lowassa imetanguliza watu kwanza fedha baadae.
Uko nafasi gani kwenye timu yake ya 2015?
 
-Siyo siri kwamba wasaka urais wawili wakubwa ndani ya CCM, January Makamba na Edward Lowassa, wamekuwa wakizunguka nchi wakigawa mamillioni ya fedha kwa wananchi ili waungwe mkono katika mbio zao za urais 2015

-Siyo siri kwamba Bw. Makamba Jr. Alikuwa mtumishi wa umma wa kawaida, lakini baada ya muda mfupi, huyu kijana amatokea kuwa na ukwasi mkubwa wa kifedha kiasi kwamba anadhamini vijana, na makundi mengi huku akigawa rushwa za waziwazi. Zanzibar aligawa simu aina za Samsung Galaxy S3 ambazo zinagharimu zaidi ya Tsh 700,000 kwa zaidi ya vijana 200 wa UVCCM. Kwa mahesabu ya juu juu, thamani ya simu 200 ni million 140. Hizi fedha amezitoa wapi January Makamba?
attachment.php

-Naye mzee Lowassa licha ya kwamba jimboni kwake ni masikini wa kutupwa, amekuwa akizunguka nchi nzima akigawa mabillioni makanisani na kwenye misikiti. Hizi fedha naye kazitoa wapi? Hawa watu wanatafuta nini Ikulu? Kwa nini CCM inyamazie tabia za hawa watu? January akumbuke kwamba ubunge wake aliupata kwa hila baada ya babake Mzee Yusuf Makamba kumfanyia hila Mzee. Shelukindo

-Naitahadharisha chama changu CCM kwamba, ikiwa itafanya makosa ya kuwapitisha hawa watu wawili ambao wanazunguka nchi wakigawa rushwa hadharani bila vyombo vya dola kuwahoji, nitafanya maamuzi magumu ya kuongoza uasi ndani ya CCM ili tuwape wananchi njia mbadala ya uongozi, hata kama itamaanisha kuwaunga mkono viongozi safi wa upinzani. Hawa vinara wawili siyo tu wanakiuka miiko na maadili ndani ya CCM, kwa maana kwamba muda wa kampeni bado, kadhalika wanavunja sheria za nchi kwa kugawa rushwa.

-January hajawahi kuchaguliwa kwenye cheo chochote kile hata ubunge, lakini badala ya kufuata njia halali, yeye anaendekeza rushwa huku akimpiga majungu waziri wake pale wizara ya Sayansi na Teknolojia. Natokea jimboni Bumbuli, lakini cha ajabu, Mzee Makamba na Mwanaye wanatangaza jimboni kwamba January Akiwa Rais Tanga itakuwa kama Singapore? Really? Tutafika kweli kwa mwendo huu? Hawa jamaa wanakimbilia ikulu kufata nini?
 
Attachments

  • makamba-lowassa.jpg
    makamba-lowassa.jpg
    25.8 KB · Views: 7,788
Hawa wapewe fundisho ili watambue kuwa watanzania wa leo si wale wa 2005

Ndiyo maana kuna shule iliyojengwa kwa miti na kuezekwa kwa majani bagamoyo, huku wakisema serikali haina fedha kumbe wanaziiba kwa malengo ya kununua uongozi.

Hakuna tena nafasi hiyo huko twendako, enough is enough
 
Haka kadogo kwanza niweke wazi ,mpaka leo sijawahi kumuona Makamba kama mtu anayefaha kuwa katika hiyo nafasi ukiachia kubebwa bebwa na jina la familia,lakini pili huyu dogo ni mzigo uliobaki CCM na atawasumbua kwasababu ana tabia kama za Zitto,wote ni watu wa uchu na wako radhi kufanya lolote na ndo walivyokuwa wakijiimarisha kwa pamoja sema sasa mwenzie CDM wameshtuka na kumshughurikia ..nawapeni pole CCM kwani majanga mnayo mengi na hizi pesa zitawagharimu na siku si nyingi mjiandae kumpokea na Zitto
 
-Siyo siri kwamba wasaka urais wawili wakubwa ndani ya CCM, January Makamba na Edward Lowassa, wamekuwa wakizunguka nchi wakigawa mamillioni ya fedha kwa wananchi ili waungwe mkono katika mbio zao za urais 2015

-Siyo siri kwamba Bw. Makamba Jr. Alikuwa mtumishi wa umma wa kawaida, lakini baada ya muda mfupi, huyu kijana amatokea kuwa na ukwasi mkubwa wa kifedha kiasi kwamba anadhamini vijana, na makundi mengi huku akigawa rushwa za waziwazi. Zanzibar aligawa simu aina za Samsung Galaxy S3 ambazo zinagharimu zaidi ya Tsh 700,000 kwa zaidi ya vijana 200 wa UVCCM. Kwa mahesabu ya juu juu, thamani ya simu 200 ni million 140. Hizi fedha amezitoa wapi January Makamba?

-Naye mzee Lowassa licha ya kwamba jimboni kwake ni masikini wa kutupwa, amekuwa akizunguka nchi nzima akigawa mabillioni makanisani na kwenye misikiti. Hizi fedha naye kazitoa wapi? Hawa watu wanatafuta nini Ikulu? Kwa nini CCM inyamazie tabia za hawa watu? January akumbuke kwamba ubunge wake aliupata kwa hila baada ya babake Mzee Yusuf Makamba kumfanyia hila Mzee. Shelukindo

-Naitahadharisha chama changu CCM kwamba, ikiwa itafanya makosa ya kuwapitisha hawa watu wawili ambao wanazunguka nchi wakigawa rushwa hadharani bila vyombo vya dola kuwahoji, nitafanya maamuzi magumu ya kuongoza uasi ndani ya CCM ili tuwape wananchi njia mbadala ya uongozi, hata kama itamaanisha kuwaunga mkono viongozi safi wa upinzani. Hawa vinara wawili siyo tu wanakiuka miiko na maadili ndani ya CCM, kwa maana kwamba muda wa kampeni bado, kadhalika wanavunja sheria za nchi kwa kugawa rushwa.

-January hajawahi kuchaguliwa kwenye cheo chochote kile hata ubunge, lakini badala ya kufuata njia halali, yeye anaendekeza rushwa huku akimpiga majungu waziri wake pale wizara ya Sayansi na Teknolojia. Natokea jimboni Bumbuli, lakini cha ajabu, Mzee Makamba na Mwanaye wanatangaza jimboni kwamba January Akiwa Rais Tanga itakuwa kama Singapore? Really? Tutafika kweli kwa mwendo huu? Hawa jamaa wanakimbilia ikulu kufata nini?
Teh teh teeeeeh...... Nkuu unashituka leo? Tayari CCM haina chake 2015, kumbe ulikuwa hujui? lakini tena CCM hawawezi kuwakoromea kwa sababu ili kupata nafasi kama hizo kupitia ccm lazima uwe na uwezo wa kuhamasisha watu wanunulike ndo unakuwa MWENZETU, haiwezekani upate bure kwani hapendwi ntu ndani ya ccm. Lakini rushwa na watoe tu, tena waje na kwengu kwa sababu wanawawezesha wasio nacho wapate msimu huu wa mavuno wala usiwaonee mtima nyongo
 
Nafikiri chama kita lipatia ufumbuzi ili swala kupitia vikao vya ndani.
CCM sio kama CDM mgogoro kidongo ndani ya chama wao wanapayuka hadi dunia nzima inajua.
 
Haka kadogo kwanza niweke wazi ,mpaka leo sijawahi kumuona Makamba kama mtu anayefaha kuwa katika hiyo nafasi ukiachia kubebwa bebwa na jina la familia,lakini pili huyu dogo ni mzigo uliobaki CCM na atawasumbua kwasababu ana tabia kama za Zitto,wote ni watu wa uchu na wako radhi kufanya lolote na ndo walivyokuwa wakijiimarisha kwa pamoja sema sasa mwenzie CDM wameshtuka na kumshughurikia ..nawapeni pole CCM kwani majanga mnayo mengi na hizi pesa zitawagharimu na siku si nyingi mjiandae kumpokea na Zitto

Dogo acha bange. Kama mbege na gongo vinakuyumbisha mpaka akili yako inakosa mwelekeo kakojoe uende kulala.

Makamba na Zitto wapi na wapi?? Ni matahira kama wewe tu ndio wenye kulinganisha Makamba na Zitto.

Mtu yeyote makini anayepambanua siasa za nchi hii kwa kina na weledi wa kiwango kinachokubalika, anafahamu kabisa kuwa Makamba na ZZK they are incomparable!!!

Ukijidanganya kulinganisha Makamba na Zitto ni sawa kwamba unalinganisha mwendo wa basikeli ya miti na jumbo jet airline. Sasa kams siyo bange, gongo, mbege na viroba vinavyokusumbua kichwani ni nini????

Lakini vilevile ni misukule na vibaraka wa dj baba freelady na mzee slaa pekee, ndio wanaoona kwamba ZZK mwanademokrasia anayedai demokrasia harisi kuanzia ndani ya chama mpaka nje ya chama kuwa ana uchu wa madaraka!

Dogo acha kuwa mvivu wa kufikili, ZZK ndio jembe la mkulima, mtanzani masikini anayepuuzwa na CCm vilevile ZZK ndio jembe la kumkomboa mtanzania anayeendelea kudanganywa na wahafidhina, mafisadi wa cdm,watafuna ruzuku, wahuni wapenda wake za watu, wasiojali jasho la mlipa kodi na kuamua kurudisha wapenzi wao kutoka ktk vikao na ziara za kamati kwenda Dubai kula maisha na hawara yake!!!!!!

Dogo,Una akili timamu kweli!!!! Bado haya yote huyaoni? Dogo acha kubwabwaja ungea vitu vya maaana ueleweke -----!!!!!!
Agrrrrrrrrrrrrr mbafu.
 
Kama sisahau JK alisharuhusu wagombea wa ccm kuanza 'campaign'. Ninachokiona ccm tayari ni mfirisi wa wagombea urais. Izi figure za mwanzo kujitokeza adharani sizo na hazitaweza kuimili nguvu ya upinzani.
 
-Siyo siri kwamba wasaka urais wawili wakubwa ndani ya CCM, January Makamba na Edward Lowassa, wamekuwa wakizunguka nchi wakigawa mamillioni ya fedha kwa wananchi ili waungwe mkono katika mbio zao za urais 2015

-Siyo siri kwamba Bw. Makamba Jr. Alikuwa mtumishi wa umma wa kawaida, lakini baada ya muda mfupi, huyu kijana amatokea kuwa na ukwasi mkubwa wa kifedha kiasi kwamba anadhamini vijana, na makundi mengi huku akigawa rushwa za waziwazi. Zanzibar aligawa simu aina za Samsung Galaxy S3 ambazo zinagharimu zaidi ya Tsh 700,000 kwa zaidi ya vijana 200 wa UVCCM. Kwa mahesabu ya juu juu, thamani ya simu 200 ni million 140. Hizi fedha amezitoa wapi January Makamba?

-Naye mzee Lowassa licha ya kwamba jimboni kwake ni masikini wa kutupwa, amekuwa akizunguka nchi nzima akigawa mabillioni makanisani na kwenye misikiti. Hizi fedha naye kazitoa wapi? Hawa watu wanatafuta nini Ikulu? Kwa nini CCM inyamazie tabia za hawa watu? January akumbuke kwamba ubunge wake aliupata kwa hila baada ya babake Mzee Yusuf Makamba kumfanyia hila Mzee. Shelukindo

-Naitahadharisha chama changu CCM kwamba, ikiwa itafanya makosa ya kuwapitisha hawa watu wawili ambao wanazunguka nchi wakigawa rushwa hadharani bila vyombo vya dola kuwahoji, nitafanya maamuzi magumu ya kuongoza uasi ndani ya CCM ili tuwape wananchi njia mbadala ya uongozi, hata kama itamaanisha kuwaunga mkono viongozi safi wa upinzani. Hawa vinara wawili siyo tu wanakiuka miiko na maadili ndani ya CCM, kwa maana kwamba muda wa kampeni bado, kadhalika wanavunja sheria za nchi kwa kugawa rushwa.

-January hajawahi kuchaguliwa kwenye cheo chochote kile hata ubunge, lakini badala ya kufuata njia halali, yeye anaendekeza rushwa huku akimpiga majungu waziri wake pale wizara ya Sayansi na Teknolojia. Natokea jimboni Bumbuli, lakini cha ajabu, Mzee Makamba na Mwanaye wanatangaza jimboni kwamba January Akiwa Rais Tanga itakuwa kama Singapore? Really? Tutafika kweli kwa mwendo huu? Hawa jamaa wanakimbilia ikulu kufata nini?

Wewe ni CCM na UNAULIZA? Haukusoma HABARI ya kuwa Waziri wa Madini Dr. Muhongo Amekwapua SH. Million 400 Unadhani zinakwenda kwa Wananchi???
 
Mosco nakupongeza umeliona hilo. Kazi ya mwisho unayotakiwa ufanye kwa kumaliza hasira zako ni kupitia sanduku la KURA. Omba Mungu akufikishe 2015.
 
ndugu mwanaccm pole sana ! Ni vizuri ukajua kuanzia leo kwamba ccm ni kichaka cha wahalifu , rejea kauli ya KAPUYA kwamba ' watoto wetu wanauza unga na hakuna wa kuwakamata ' ! Katika wenye ccm wewe haumo bali unajipendekeza tu !
 
Watanzania kama hawataamka basi pesa zao(zitaendelea) kuibwa au kuchukuliwa kihalali na kuishia katika matumizi ambayo hayakukusudiwa kama vile vikao/upembuzi yakinifu/michakato e.tc.
 
Back
Top Bottom