Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?

Nafikiri chama kita lipatia ufumbuzi ili swala kupitia vikao vya ndani.
CCM sio kama CDM mgogoro kidongo ndani ya chama wao wanapayuka hadi dunia nzima inajua.

Tatizo la rushwa na ufisadi linatatuliwa na vikao vya ndani ??? Baada ya zoezi la kuvuana magamba kushindwa au vipi Shame on
 

Weka ushahidi hatutaki umbea umbea hapa
 
Una chuk kama mtoto wa kondoo,ona aibu nan kasema anatafta urais?unaujua umri wa JM? Je kufkia hyo 2015 atakuwa amefikisha umri wa miaka 45?acha chuki za kibwabwa mkuu ukiwa GT pambanua mambo kwa kina,,,,,,,,,afu kama wanagawa rushwa ww kama raia mwema mtaka haki na usawa kawariport takukuru basi ulete uzi hapa na kesi uliowafungulia
 

Mkuu miaka 45 ya nini? Kama hujui miaka siamini kama unajua kwamba hawautaki Urais!!
 
Mkuu Moscow kwa jinsi ya makundi yalivyo kwa hivi sasa ndani ya CCM, CCM isipomeguka mapande mapande kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 basi itadumu daima.

Naona mwanza kuna kura nyingi kwa kuwa wawania Urais wengi ndani ya CCM wamekula xmass jijini Mwanza wakiwa na lundo la wafuasi wao.
 
Last edited by a moderator:
Hii nchi bado ni kichwa cha mwenda wazimu. Hata jambazi lowasa na makamba eti wanataka wawe marais......na tatizo mitanzania mingi bado haina akili wa naweza kuwapigia kura.
Kazi yetu sisi kunyolewa na kila mwenye fedha. Jamani ya kikwete yametutosha sasa tunataka MTU Majibu sio misifamisifa
 

Kaka kama ungalikuwa na akili kidogo tu hata kama ya kuku ungalimfahamu zito na tabia zake. Unangia kwa kuchemka kama mafuta ukidhani unawasilisha uhalisia kumbe you are very negative about who is real Zitto. Zito ana sura zaidi ya kumi na ni kigeugeu, msalili, mnafiki, muongo, mwenye ucho wa madaraka, mwenye hila mpaka kufikia njama za kuuwa huku akisingizia ni yeye anawinda na uchafu mwingi ambao hauelezeki kwa kuwa hapa is too public. Zito ni hatari kuliko anavyokuaminisha, unavyosoma maandiko/ matamshi yake na anavyojipambanua. Anajijua yeye mwenyewe, baadhi ya washirika wake wanaoshirikia kutekeleza uovu na ushirikina wake.
 
Hawa wanaohonga wananchi kwa sasa waachwe waendelee na honga hizi ili angalao fedha zinazokwapuliwa kwa wananchi ziwarudie na at the end in mmoja tu ndo atakayechaguliwa. Tusiwakatisj=he tamaa tena tuwapongeze ili ari ya hongo iendelee na maskini wa kijijini wapate nao haki
 
mpaka sasa ina mapande mengi, hawa jamaa -cccccmmmm kutoka 2015 na kushika ikulu kazi sana, naona ule mchezo wa kheri tukose wote unakuja ktk hiki chama, hapa ni suala la muda tu. Wamefikia pabaya sana, hawaaminiani, wanazungukana, wanaangamizana, utu hakuna, kila mtu ana lake. Angalia hata pale bungeni jinsi wabunge wake wanavyoongea ni aibu tupu. Wamesahau kabisa ilani yao ya uchaguzi badala ya kutekeleza ilani wanalumbana ni aibu tupu kwa watu wazima
 
Mkuu miaka 45 ya nini? Kama hujui miaka siamini kama unajua kwamba hawautaki Urais!!

Miaka 41 najua kwa mujbu wa katka ya JMT swal langu n je atakuwa kafka hapo?jib n hapana hvo basi nkianza na ww shobo kali waambie wenzio waache chuk za kikondoo wafanye yanayowahusu,tukiendekeza chuk hz TZ itakuwa nchi ya mapoyoyo tuuuu
 
hili ni balaa aisee,makamba nae anataka urais?kwa uzoefu upi alionao kisiasa? haya bwana kila la heri bwana makamba jr
 
Mh.Lowassa na January Makamba wote hawa walikuwa kambi moja ndani CCM na walifanikisha kwa njia zozote zile kumweka Jakaya Kikwete Madarakani mpaka wa Leo.


Sasa wote wawili wanapita huku na kule kujitengenezea makundi ndani na nje ya chama.

Makanisani na Misikitini wameingia nakutoka na wameacha ushawishi pamoja na Minoti kibao.

Boda Boda nao tayari wamefikiwa na kila mmoja wao na kuwamwagia ahadi kabambe.

Ila Nitumie nafasi hii kuwaonya madriver Boda Boda wasije wakageuzwa kuwa Double Double badala ya kubakia Boda Boda na wakatuletea Machafuko na Umwagaji wa Damu Usio wa Lazima Ndani Ya Tanzania Yetu.

Nataka kusema wazi January Makamba kuanza mbio za kuusaka Urais mapema hili sio jambo la Bahati mbaya.

Ni mkakati uliosukwa kwa ustadi sana wasio makini wanatoka kavu ukoko bila mchuzi.

Nitawaonyesha kwa kuwabomolea chumba kidogo tu.


Hii ndio kazi ya Makamba Jr :-

1.Kumdhoofisha nguvu Lowassa popote pale alipojijenga ndani na nje ya chama.

2.Kuwagawa wanachama na wapambe wa Eddo ili iwe kazi rahisi kumtengenezea njia Mteule ajaye ndani ya CCM hasa kwenye uchaguzi wao wa kumpata mpeperusha Bendera ya CCM bila ya kutumia Jasho jingi sana.

Kwanini wamefanya hivi.
Wanahofia Lowassa akivuka kuwa mteule wa chama na akafanikiwa kuupata Urais watakuja kushughulikia mmoja baada ya mwingine.

Pia Mahesabu yao yanasimama zaidi kwenye Umri.

Wanaona Makamba bado ana umri mdogo ukimlinganisha na Lowassa,yeye ni Kijana Mwororo hata akikosa kuteuliwa ndani ya chama cha mapinduzi 2014 kwake hakuna madhara kama kwa Mh.Lowassa.

Wanajua wazi Lowassa hana Ujanja wa kwenda na kiu ya kuutaka Urais kwa mwendo wa Miaka Ishirini (20) Ijayo,

Wakifanikiwa kumharibia 2014 ndio basi.

Kama mnazifutilia siasa za jirani zetu Kenya Utagundua Uhuru na Ruto Wamejipanga kuachiana Madaraka umri pia umezingatiwa.

Inavyoonekana Ndani ya CCM mpango ni huu Mh.Lowasaa na J.Makamba Jr 2014 wakose wote atawekwa ambaye hakutarajiwa sanana wengi ili kupambana na CHADEMA.

Endapo atahimili mikiki mikiki ya CHADEMA Mgombea wao na Kushinda Basi akifanikiwa kumaliza miaka kumi (10) Ndiposa J.Makamba Gamba liliokomaa kwa wakati huo naye Ashike Dola.

Huu ni mkakati wao Makamba na wenzake Mwenye kupuuza na apuuze.

Mh.Lowassa kama kweli uko makini hapa ndipo Pakuangalia. Uliwahi Kusikika unasema WAKIMWAGA UGALI WEWE UTAMWAGA MBOGA

Hapo ndipo tutakapojua MBIVU na MBICHI ndani ya CHAMA CHA MAPINDUZI. Na Msisahau wote kuwa, HASIRA YA MKIZI NI FURAHA YA MVUVI.

Nashauri Mh.Lowassa achangamke mapema 2014 kumwaga mboga.

Ukifanikiwa kuingia mwaka mpya wa 2014 Usijivune maana sio kwa nguvu wala kwa uwezo wako,WEWE JIFUNZE KUWA NA SHUKRANI KWA MUNGU.
 
Inawezekana ukawa sahihi kwani sion kama makamba kwss ana sifa/uzoefu za kuwa rais,yawezezekana ikawa nai maandalizi( long term plan )
 
Nafikiri chama kita lipatia ufumbuzi ili swala kupitia vikao vya ndani.
CCM sio kama CDM mgogoro kidongo ndani ya chama wao wanapayuka hadi dunia nzima inajua.
Ccm hamna ujasiri wa kuwajibishana ,acha longolongo yako.Chadema hawaangalii sura ya mtu.Paka shume wewe,nenda Lumumba kachukue buku 4 sasa.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…