-Siyo siri kwamba wasaka urais wawili wakubwa ndani ya CCM, January Makamba na Edward Lowassa, wamekuwa wakizunguka nchi wakigawa mamillioni ya fedha kwa wananchi ili waungwe mkono katika mbio zao za urais 2015
-Siyo siri kwamba Bw. Makamba Jr. Alikuwa mtumishi wa umma wa kawaida, lakini baada ya muda mfupi, huyu kijana amatokea kuwa na ukwasi mkubwa wa kifedha kiasi kwamba anadhamini vijana, na makundi mengi huku akigawa rushwa za waziwazi. Zanzibar aligawa simu aina za Samsung Galaxy S3 ambazo zinagharimu zaidi ya Tsh 700,000 kwa zaidi ya vijana 200 wa UVCCM. Kwa mahesabu ya juu juu, thamani ya simu 200 ni million 140. Hizi fedha amezitoa wapi January Makamba?
-Naye mzee Lowassa licha ya kwamba jimboni kwake ni masikini wa kutupwa, amekuwa akizunguka nchi nzima akigawa mabillioni makanisani na kwenye misikiti. Hizi fedha naye kazitoa wapi? Hawa watu wanatafuta nini Ikulu? Kwa nini CCM inyamazie tabia za hawa watu? January akumbuke kwamba ubunge wake aliupata kwa hila baada ya babake Mzee Yusuf Makamba kumfanyia hila Mzee. Shelukindo
-Naitahadharisha chama changu CCM kwamba, ikiwa itafanya makosa ya kuwapitisha hawa watu wawili ambao wanazunguka nchi wakigawa rushwa hadharani bila vyombo vya dola kuwahoji, nitafanya maamuzi magumu ya kuongoza uasi ndani ya CCM ili tuwape wananchi njia mbadala ya uongozi, hata kama itamaanisha kuwaunga mkono viongozi safi wa upinzani. Hawa vinara wawili siyo tu wanakiuka miiko na maadili ndani ya CCM, kwa maana kwamba muda wa kampeni bado, kadhalika wanavunja sheria za nchi kwa kugawa rushwa.
-January hajawahi kuchaguliwa kwenye cheo chochote kile hata ubunge, lakini badala ya kufuata njia halali, yeye anaendekeza rushwa huku akimpiga majungu waziri wake pale wizara ya Sayansi na Teknolojia. Natokea jimboni Bumbuli, lakini cha ajabu, Mzee Makamba na Mwanaye wanatangaza jimboni kwamba January Akiwa Rais Tanga itakuwa kama Singapore? Really? Tutafika kweli kwa mwendo huu? Hawa jamaa wanakimbilia ikulu kufata nini?
Waacheni mafisadi na vibaraka wao walamba makombo wahangaike kugawa rushwa za kila aina,kiboko yao 2015 pale tutakapowapiga chini pamoja na kula pesa zao! WAKILETA PESA ZAO AU BODABODA ZAO TUNACHUKUA LAKINI KURA TUNAPIGA CDM,Watz wa leo si wale wa 2010!
Waacheni mafisadi na vibaraka wao walamba makombo wahangaike kugawa rushwa za kila aina,kiboko yao 2015 pale tutakapowapiga chini pamoja na kula pesa zao! WAKILETA PESA ZAO AU BODABODA ZAO TUNACHUKUA LAKINI KURA TUNAPIGA CDM,Watz wa leo si wale wa 2010!
Weka ushahidi hatutaki umbea umbea hapa
Tuendelee kuandika sana......RA ni mwendo kimya kimya......myaonayo kwa EL ni mvua za vuli...... subirini ELNINYO.......poor me and you......
Haka kadogo kwanza niweke wazi ,mpaka leo sijawahi kumuona Makamba kama mtu anayefaha kuwa katika hiyo nafasi ukiachia kubebwa bebwa na jina la familia,lakini pili huyu dogo ni mzigo uliobaki CCM na atawasumbua kwasababu ana tabia kama za Zitto,wote ni watu wa uchu na wako radhi kufanya lolote na ndo walivyokuwa wakijiimarisha kwa pamoja sema sasa mwenzie CDM wameshtuka na kumshughurikia ..nawapeni pole CCM kwani majanga mnayo mengi na hizi pesa zitawagharimu na siku si nyingi mjiandae kumpokea na Zitto
Kaka kama ungalikuwa na akili kidogo tu hata kama ya kuku ungalimfahamu zito na tabia zake. Unangia kwa kuchemka kama mafuta ukidhani unawasilisha uhalisia kumbe you are very negative about who is real Zitto. Zito ana sura zaidi ya kumi na ni kigeugeu, msalili, mnafiki, muongo, mwenye ucho wa madaraka, mwenye hila mpaka kufikia njama za kuuwa huku akisingizia ni yeye anawinda na uchafu mwingi ambao hauelezeki kwa kuwa hapa is too public. Zito ni hatari kuliko anavyokuaminisha, unavyosoma maandiko/ matamshi yake na anavyojipambanua. Anajijua yeye mwenyewe, baadhi ya washirika wake wanaoshirikia kutekeleza uovu na ushirikina wake.
Kuna vitu vinashangaza katika taifa hili mojawapo ni hili suala la Watu kugawa Fedha wazi wazi Huku mamlaka zikiangalia tuSumaye kasema watanzania tushaanza kupigwa mnada na mafisadi. Tena ni timu kwa mafisadi kutuonyesha kweli alituibia ndio maana anagawa hela kila mahali , tuwe makini!!
Tofauti na Mwalimu alivyosema, siku hizi Ikulu kuna biashara kubwa sana.Sumaye kasema watanzania tushaanza kupigwa mnada na mafisadi. Tena ni timu kwa mafisadi kutuonyesha kweli alituibia ndio maana anagawa hela kila mahali , tuwe makini!!
Kuwakamata inawezekana ikawa ngumu lakini inawezekana kufuatilia kujua pesa wanapata wapi na kuwadhibiti au kufuatilia kipato chao, Mtu Kama January heal yote hii anapata wapi? Si mfanyabiashara ni waziri tu.Kwa mbinu hizi ningumu kwa takukuru kuwakamata kwani wao wamekuja na mbinu mpya ya kuwawezesha vijana kujipatia kipato ndo maana wanaanza mapema kabla ya kampeni nakampeni zikianza ni maneno huku wakipaza sauti kwanaotumia hongo kutafuta kura kumbe wao walifanya vitendo hivyo kabla!
Ccm hamna ujasiri wa kuwajibishana ,acha longolongo yako.Chadema hawaangalii sura ya mtu.Paka shume wewe,nenda Lumumba kachukue buku 4 sasa.
ushauri wako ni mzuri sana lakini ccm ni sikio la kufaSi siri tena kwamba bwana Lowassa anausaka urais kwa udi na uvumba. Anamwaga millions of money makanisani na misikitini. Ukija kwa Makamba, ukamcheki vizuri unagundua kuwa kijana ana kiu kuu ya urais na mahali alipofikia, yuko tayari kunywa hata mkojo(rushwa) ili afikie malengo. Juzi amemwaga simu za gharama kwa vijana huko Zanzibar wakati Mwanza ameahidi pikipiki za millions of money kwa vijana. Style zao wote wawili hazitofautiani. Ni watu wenye lengo moja hawa na kamwe ccm msijiloge kuamini kwamba E.L na J.M ni mahasimu. Ninachokiona mimi ni formation ya game ambayo imesukwa kiufundi. Lowassa alichofanya ni kumtumia J.M kwakuwa ni kijana makini na ana ushawishi kwa vijana. Kitakachotokea Mwishoni J.M atampisha Lowassa na kama Lowassa upepo hautamwendea vizuri basi awe amempachika Rais wake J.M. Kwa ccm hiyo ni game hatari msipochukua hatua hao jamaa wanawaulieni chama asubuhiasubuhi. Ni ushauri tu nimeutoa bure kwenu!. Mnaweza kuupuuza ama kuufanyia kazi. CCM oyeeeee+peoplesssss poweeeeeeeeer+hakiiiiiiiiiiiiiii!