georgina george
Senior Member
- Dec 19, 2012
- 114
- 30
Nafikiri chama kita lipatia ufumbuzi ili swala kupitia vikao vya ndani.
CCM sio kama CDM mgogoro kidongo ndani ya chama wao wanapayuka hadi dunia nzima inajua.
Si siri tena kwamba bwana Lowassa anausaka urais kwa udi na uvumba. Anamwaga millions of money makanisani na misikitini. Ukija kwa Makamba, ukamcheki vizuri unagundua kuwa kijana ana kiu kuu ya urais na mahali alipofikia, yuko tayari kunywa hata mkojo(rushwa) ili afikie malengo. Juzi amemwaga simu za gharama kwa vijana huko Zanzibar wakati Mwanza ameahidi pikipiki za millions of money kwa vijana. Style zao wote wawili hazitofautiani. Ni watu wenye lengo moja hawa na kamwe ccm msijiloge kuamini kwamba E.L na J.M ni mahasimu. Ninachokiona mimi ni formation ya game ambayo imesukwa kiufundi. Lowassa alichofanya ni kumtumia J.M kwakuwa ni kijana makini na ana ushawishi kwa vijana. Kitakachotokea Mwishoni J.M atampisha Lowassa na kama Lowassa upepo hautamwendea vizuri basi awe amempachika Rais wake J.M. Kwa ccm hiyo ni game hatari msipochukua hatua hao jamaa wanawaulieni chama asubuhiasubuhi. Ni ushauri tu nimeutoa bure kwenu!. Mnaweza kuupuuza ama kuufanyia kazi. CCM oyeeeee+peoplesssss poweeeeeeeeer+hakiiiiiiiiiiiiiii!
Kweli wewe ni mvivu wa kufikiri kama avatar yako inavyoonyesha.
Pole kwa fikra mgando!
Wewe ambaye sio mnafki ebu weka post yako tuione.Post ya kinafiki na aliyepost ni mnafiki, huna jipya ...
mwanza wananchi wame thubutu huko dar ambako mnalala nao mnaishia kuwapisha na ving'ola vyaoNimepata tetesi kwamba January anafadhiliwa na shemeji yake Rostam Azizi?
Kama kweli basi tunalo. Ifike hawa jamaa mafisadi waanze kupigwa mawe
-Siyo siri kwamba wasaka urais wawili wakubwa ndani ya CCM, January Makamba na Edward Lowassa, wamekuwa wakizunguka nchi wakigawa mamillioni ya fedha kwa wananchi ili waungwe mkono katika mbio zao za urais 2015
-Siyo siri kwamba Bw. Makamba Jr. Alikuwa mtumishi wa umma wa kawaida, lakini baada ya muda mfupi, huyu kijana amatokea kuwa na ukwasi mkubwa wa kifedha kiasi kwamba anadhamini vijana, na makundi mengi huku akigawa rushwa za waziwazi. Zanzibar aligawa simu aina za Samsung Galaxy S3 ambazo zinagharimu zaidi ya Tsh 700,000 kwa zaidi ya vijana 200 wa UVCCM. Kwa mahesabu ya juu juu, thamani ya simu 200 ni million 140. Hizi fedha amezitoa wapi January Makamba?
-Naye mzee Lowassa licha ya kwamba jimboni kwake ni masikini wa kutupwa, amekuwa akizunguka nchi nzima akigawa mabillioni makanisani na kwenye misikiti. Hizi fedha naye kazitoa wapi? Hawa watu wanatafuta nini Ikulu? Kwa nini CCM inyamazie tabia za hawa watu? January akumbuke kwamba ubunge wake aliupata kwa hila baada ya babake Mzee Yusuf Makamba kumfanyia hila Mzee. Shelukindo
-Naitahadharisha chama changu CCM kwamba, ikiwa itafanya makosa ya kuwapitisha hawa watu wawili ambao wanazunguka nchi wakigawa rushwa hadharani bila vyombo vya dola kuwahoji, nitafanya maamuzi magumu ya kuongoza uasi ndani ya CCM ili tuwape wananchi njia mbadala ya uongozi, hata kama itamaanisha kuwaunga mkono viongozi safi wa upinzani. Hawa vinara wawili siyo tu wanakiuka miiko na maadili ndani ya CCM, kwa maana kwamba muda wa kampeni bado, kadhalika wanavunja sheria za nchi kwa kugawa rushwa.
-January hajawahi kuchaguliwa kwenye cheo chochote kile hata ubunge, lakini badala ya kufuata njia halali, yeye anaendekeza rushwa huku akimpiga majungu waziri wake pale wizara ya Sayansi na Teknolojia. Natokea jimboni Bumbuli, lakini cha ajabu, Mzee Makamba na Mwanaye wanatangaza jimboni kwamba January Akiwa Rais Tanga itakuwa kama Singapore? Really? Tutafika kweli kwa mwendo huu? Hawa jamaa wanakimbilia ikulu kufata nini?
mwanza wananchi wame thubutu huko dar ambako mnalala nao mnaishia kuwapisha na ving'ola vyao
Kuna mtafaruku mkubwa kati ya EL na JM. JM ameshastuka kwamba ngamia hawezi kuingia kwenye tundu la sindano hivyo basi JM ameamua aende solo kuponya mkate wake. Kosa la JM ni kutumia mbinu za boda boda na kugawa ela, mbinu hizi zitamgharimu.
Haka kadogo kwanza niweke wazi ,mpaka leo sijawahi kumuona Makamba kama mtu anayefaha kuwa katika hiyo nafasi ukiachia kubebwa bebwa na jina la familia,lakini pili huyu dogo ni mzigo uliobaki CCM na atawasumbua kwasababu ana tabia kama za Zitto,wote ni watu wa uchu na wako radhi kufanya lolote na ndo walivyokuwa wakijiimarisha kwa pamoja sema sasa mwenzie CDM wameshtuka na kumshughurikia ..nawapeni pole CCM kwani majanga mnayo mengi na hizi pesa zitawagharimu na siku si nyingi mjiandae kumpokea na Zitto
Lowasa anafaa achana na mawazo mgando jamani mnataka kila m2 awe masikini kama nyinyi? acheni roho za kwa nini ni kambi gani isiyo na mafisadi? msiongee vi2 hakuna data nyinyi mambo ya kusikia si ya kutemea nayo mtaani nyny wanafiki
Aogopwe kama ukoma huyo.