Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?

Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?

PASCO,Naomba nitofautiane na wewe kidogo kimtazamo.siyo ccm ndio waliwasadikisha watu kuwa kila tajiri ni fisadi.katika Nchi ya masikini wa kipato wengi,kila mwenye nacho huonekana machoni pao kama fisadi vile.wao hudhani pengine hawa walionacho(the haves) wamepata kwa kuwadhurumu wasio nacho (the have nots).usishangae kuona hata mtumishi wa umma ambaye hana hata sehemu ya kuchakachua,akifanya bidii akachuma mali kwa njia halali bado ataonekana ni FISADI.hata wewe kama unamiliki gari na nyumba kuna watu wanakuona ni FISADI.
Kama mtu amekuwa kwenye politics kwa takribani miaka 40 atashindwaje kuwa tajiri kama ana wekeza utajiri na mali zake vizuri? mimi ningeshangaa kama angekuwa masikini. unawezaje kuwa waziri miaka yote hiyo halafu ubaki kuwa masikini?
Ata kama anaiba tunyamaze tu
 
pasco una mahaba na lowassa,lowassa alishindwa kumwambia nyerere alivyopata mali zake!na huoni kumiliki hayo makampuni akiwa kiongozi mwandamizi serikalini kuna conflict of interest au undue influence?

Mzee waswahili wanausemi, ukipenda, chongo huliita kengeza! Naziona jitihada za kumsafisha zimekamilika sasa anang'arishwa! Watanzania ndivyo tulivyo ni wepesi kusahau! Naona wote tuko mkao wa kujiandaa kuyaramba matapishi yetu wenyewe!
 
Jamani mie kuna kitu kinanichanganya sana kuna siku moja kwenye gazeti fulani waliandika mawaziri wastaafu mmoja kati ya hao alikuwa lowassa sasa lowasa alistaafu (retirement) au aliacha uwaziri (resign) na pia ata vyombo vya habari pia vinaandika kuwa waziri mstaafu edward lowassa huu ndio ufisadi jamani maana huyu jamaa anatumia ela za uwaziri mstaafu kwa ajili ya tiba na mambo mengine yanayo wafeva mawaziri wastaafu alafu pia unamwona waziri wa afya na naibu wake wana kubali bajeti ya wizara wakati kuna watu hawastaili kuwamo kwenye bajeti shame on them kabisa wanarudisha nchi nyuma
 
Mkuu hivi umejiuliza swali dogo tu kabla hujaingia kwenye maswali makubwa kuwa richmond walikuwa wanalipwa shiling ngapi kwa siku wazalishe au wasizalishe umeme
 
Fisadi chapakazi Lowasa!!!! Property rent kwa DSM kwa mwezi ni over 250 mil. Bado za Arusha na kwingineko!!! Bepari hili linataka Urais 2015 na ule mtandao wake unakazana ukichuana na ule wa Membe!! Patachimbika!!
 
Najiuliza na kukosa majibu Mh.Lowasa si mfanyabiashara,zaidi ya kuwa mbunge,nimejionea siku za hivi karibuni katika vyombo vya habari akichangia mambo mengi hasa katika miradi ya maendeleo na katika taasisi binafsi na zamakanisa.Huyu mweshimiwa pesa anazitoa wapi?

Je alikwisha tangaza mali zake hadharani? na kipato chake kiko vipi?Alipokuwa waziri katika awamu ya tatu kwa nini akufanya hivyo?na alipokuwa waziri mkuu kwa nini alishidwa kufanya hivyo? Na kwa nini safari zake na hotuba zake zinapewa umuhimu mkubwa katika vyombo vyetu vya habari?
Hapo kwenye bold hapo hujafanya utafiti mkuu, jamaa ni mfanya biashara mkubwa anamiliki ranch huko tanga ana hisa kwenye makampuni kama voda nk. Na kama ujuavyo makampuni ya simu za mikononi ni blue chip company.. hivyo jamaa kuwa na uhakika wa kipato kikubwa maisha yake yote.
 
Katika toleo la Nipashe Jumapili, lililochapishwa jana tarehe 21 Oktoba, 2012, mwandishi wa gazeti hilo Mashaka Mgeta amechambua kwa kina na ufasaha kuhusiana na kile kilicho wazi sasa, yaani kuwasi usiomithilika wa Edward Lowassa. Anajiuliza alikozipata fedha hizo katika maisha yake ya utumishi wa umma na hasa wakati huu ambao hayuko katika madaraka ya kiserikali. Amejiuliza pia kwamba kwa nini hilo linatokea sasa na dhamira yake hasa ni nini! Mgeta anseema kwamba Lowassa hajawahi kujipambanua kama mfanyabiashara mahiri kama walivyo akina Sabodo na Bakhresa.

Kwa waliosoma makala hiyo watakubaliana na mimi kwamba mwandishi huyo ameibua hoja nzito na zenye kudai amjibu ya kina katika kipindi hiki ambacho mwanasiasa huyu mkongwe anahusishwa na harakati za kuusaka urais, huku kila ukicha zikitolewa takwimu za watu waje walioingia katika nafasi za uongozi wa chama na jumuiya zake, katika mazingira yaliyojaa matumizi makubwa ya fedha. Tumeshuhudia pia matumizi ya fedha dhidi ya wale wanaoaminika kuwa mahasimu wakubwa wa kisiasa, kama vile Sumaye, Makongoro Nyerere, Anna Kilango na wengine kadhaa. Sasa hivi kuna tetesi kwamba nguvu zimeelekezwa kuhakikisha kwamba Membe hapati kitu kwenye lile kundi la kifo la kugombea kuingia kwenye NEC ya CCM.

Hebu tilijadili hili wana JF.
 
Duh! Jamaa kashuka maana na mie nimemsoma na hakika hoja za Mgeta hazipaswi kupuuzwa. Hivi uongozi unaonunuliwa kwa mabilioni haya ambayo asili yake haifahamiki una malengo gani na kama alivyosema Mwalimu Nyerere zitarudije? Nchi imeingia kwenye janga na Watanzania wanapaswa kuamka kulikataa hili kwa nguvu maana katika siku za mwanzo tu za uongozi wake nchi hii itakuwa imeshauzwa na kutakuwa na machafuko makubwa ambayo hayajawahi kutokea! Mungu ibariki Tanzania.
 
Nadhani iko sababu kwa CCM kuweka hadharani utajiri na mali ya kila kiongozi wa CCM anayefikiria kutupa karata ya urais 2015.
 
Lowassa anasahau kwamba fedha inaweza kununua baadhi ya vitu, kama wajumbe hawa uchwara wanaonunuliwa hivi sasa lakini kamwe Tanzania haina gharama inayoweza kulipwa na yeyote. Lowassa aache kujidanganya.
 
Aangalie huyo Mgeta maana anapambana na adui asiyemjua nguvu zake,watamsambaratisha bila kujielewa!mtandao wake ni mkali sana,tusubiri majibu yake asije akapiga kelele bure
 
Aangalie huyo Mgeta maana anapambana na adui asiyemjua nguvu zake,watamsambaratisha bila kujielewa!mtandao wake ni mkali sana,tusubiri majibu yake asije akapiga kelele bure

Hivi nyinyi watanzania ni wa ajabu sana! Yaani wewe unaona fahari vitendo vya kuhujumu uhuru wa kutoa maoni ambao waliopigania uhuru walimwaga damu hadi tukaupata? Una maanisha nini unaposema kumsambaratisha? Ni kumuua? Shauri yenu mtakapokuwa na kesi ya kujibu mbele ya haki kwa sababu tu watu walijitolea kusema ukweli wa kile wengine mnachokifumbia macho kwa kichocheo cha fedha na kuuza utu! Mungu atamlinda Mgeta na wapigania haki wengine.
 
Nadhani iko sababu kwa CCM kuweka hadharani utajiri na mali ya kila kiongozi wa CCM anayefikiria kutupa karata ya urais 2015.

CCM hawataweza kufanya hivyo. they are driven by the power of money. M4C wakaze buti kuwaelimisha watu vijijini madhara ya watu kununua uongozi. Wajiandikishe na kupiga kura kwa wingi dhidi ya magamba na wajitahidi kulinda kura zao. Otherwise EL atashangaza wengi.
 
Aangalie huyo Mgeta maana anapambana na adui asiyemjua nguvu zake,watamsambaratisha bila kujielewa!mtandao wake ni mkali sana,tusubiri majibu yake asije akapiga kelele bure
mkuu unakuja na hoja dhaifu ya vitisho. jamaa amefikisha ujumbe, so fanyeni mnalo fanya.
 
kuna siku nimemuona kwenye gazeti akifanya harambee kwenye msikiti... fikirieni huyu jamaa anasaidia kujenga makanisa na kuendesha shuhuli mbalimbali za kimaendeleo...akiwa rais itakuaje? tatizo jk anampa mtu kazi alafu anamuachia aifanye bila kumfuatilia...huyu mmasai hata kama amekupa wewe cheo lakini atafuatilia utendaji wako wa kazi...ndio maana enzi zake za uwaziri mkuu mawaziri na makatibu wengi walikua hawampendi maana alikua anawafuatilia...
 
Lowassa FISADI, MWIZI, JAMBAZI, hawezi nishawishi kwa namna yoyote nimuunge mkono! Hafai kuongoza Watz.

Ushahidi wa haya yote ni nini? Mbona kila siku watu wanasema Lowasa fisadi lakini hawajawahi kuthibitisha hili? Hata Nape mwenyewe anasema Lowasa si safi lakini anashindwa kuthibisha basi mtusaidie na sisi wengine tujue huo ujambazi wake,wizi wake na huo ufisadi wake ni upi tufafanulieni hapo basi na sisi wengine tuamini hivyo.
 
Ni ShareHolder kwenye kampuni ya Vodacom ndiyo sababu hailipi kodi stahiki na hawasumbuliwi.
 
Back
Top Bottom