PASCO,Naomba nitofautiane na wewe kidogo kimtazamo.siyo ccm ndio waliwasadikisha watu kuwa kila tajiri ni fisadi.katika Nchi ya masikini wa kipato wengi,kila mwenye nacho huonekana machoni pao kama fisadi vile.wao hudhani pengine hawa walionacho(the haves) wamepata kwa kuwadhurumu wasio nacho (the have nots).usishangae kuona hata mtumishi wa umma ambaye hana hata sehemu ya kuchakachua,akifanya bidii akachuma mali kwa njia halali bado ataonekana ni FISADI.hata wewe kama unamiliki gari na nyumba kuna watu wanakuona ni FISADI.
Kama mtu amekuwa kwenye politics kwa takribani miaka 40 atashindwaje kuwa tajiri kama ana wekeza utajiri na mali zake vizuri? mimi ningeshangaa kama angekuwa masikini. unawezaje kuwa waziri miaka yote hiyo halafu ubaki kuwa masikini?