Mh. Pinda; Mbunge wa CCM atakayetetea kura ya siri atanyang'anywa kadi!

Mh. Pinda; Mbunge wa CCM atakayetetea kura ya siri atanyang'anywa kadi!

sirluta

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2012
Posts
6,325
Reaction score
2,491
Mheshimiwa waziri mkuu, Mizengo Pinda ametangaza kwenye kikao kilichowashirikisha baadh ya wabunge wa CCM kuwa atakayetetea kura ya siri atanyanganywa kadi ya chama! Vigezo na masharti yazingatiwe.
 
kwani yeye ni nani ndani ya chama hadi awe na mamlaka ya kunyang'anya watu kadi

anatishia tu !
 
Sawa tu ; inaakisi mengi tu ambayo hayajulikani na kuhakikisha kuwa chama kwanza nchi baadae sana!!!!!!

Kweli "amani inaisha unabaki utulivu"!!!!!
 
Mheshimiwa waziri mkuu, Mizengo Pinda ametangaza kwenye kikao kilichowashirikisha baadh ya wabunge wa ccm kuwa atakayetetea kura ya siri atanyanganywa kadi ya chama! Vigezo na masharti yazingatiwe.
WITO KWA WABUNGE WA BUNGE MAALUMU WAPENDA MABADILIKO YA KATIBA,CCM WAKIPITISHA KURA YA WAZI BASI MMUONDOKE BUNGENI MUWAACHE CCM WAJITENGENEZEE KATIBA YAO YA CHAMA.full stop ni kupotezeana muda kama niya thabiti ya kuwa na katiba mpya
 
hawa ndio walikuwa wanadai eti wana demokrasia na kuwa hakuna haja ya kuogopa hakuna atakayeonewa. sasa leo wananchi wamewaona kwa rangi zao mtu namba wani wa kulaumiwa ni jakaya kikwete kwakuingilia zoezi zima la kutunga huku akiubiri kutoingiza vyama lakini kwenye vikao vya siri na wana ccm wenzake wanapanga mbinu zote za kutetea katiba ki vyama.
 
Hii ni jeuri ikipitishwa, Watanzania hawataisamehe CCM. Haiwezekani kuwaburuza watu namna hiyo katika jambo kubwa na la msingi kama Katiba. Na hawa wabunge wa CCM nao bana! Mnatishwa na mnatetemeka kama nani hii! Katiba ya nchi ni jambo la kufa na kupona. Simameni muifie nchi yenu hata kama mtafukuzwa CCM. Kwani nini? CCM sio baba wala mama yenu. Tutawashangaa mkithubutu kuisaliti nchi kwa kuogopa CCM!
 
Mheshimiwa waziri mkuu, Mizengo Pinda ametangaza kwenye kikao kilichowashirikisha baadh ya wabunge wa ccm kuwa atakayetetea kura ya siri atanyanganywa kadi ya chama! Vigezo na masharti yazingatiwe.

Hii ina maana kama mbunge ataonekana kupiga kura ya wazi kupinga msimamo wa chama ktk kipengele Chochote cha katiba atashughulikiwa pia!
Kweli tuna safari ndefu ya kufika kwenye demokrasia ya kweli.
 
Hii ina maana kama mbunge ataonekana kupiga kura ya wazi kupinga msimamo wa chama ktk kipengele Chochote cha katiba atashughulikiwa pia!
Kweli tuna safari ndefu ya kufika kwenye demokrasia ya kweli.

Hapa cha msingi ni wale ambao hawataki kura ya siri kuondoka na kuwaachia CCM watengeneze katiba ya chama chao, kimsingi wakipitisha katiba mbovu Tanzania tusahau maendeleo hata siku moja. Hapa CCM wanajisahau na kufikiri siku zote watakuwa watakuwa madarakani, wanasahau kuwa wanaweza kuwa wapinzani siku katiba mbovu wanayopitisha ikawatesa.
 
Pamoja na vurugu za ccm na matisho kwa wabunge wao,naamini Mungu atatenda miujiza na ccm hawatafanikisha mambo yao kwa % 100,unaweza wafanya wenzako wajinga kwa mda ila huwezi kuwafanya wajinga mda wote
 
Ccm hawakujiandaa kisaikolojia katika katiba mpya,yaan wapo wapo tu
 
Wewe unamwamini Kikwete? Kikwete ni ndumilakuwili! Never trust him, that is how he is. Wakati wote huwa haeleweki anasimamia nini, ndiyo maana walio wajanja wanamzungusha kadiri wapendavyo.

hawa ndio walikuwa wanadai eti wana demokrasia na kuwa hakuna haja ya kuogopa hakuna atakayeonewa. sasa leo wananchi wamewaona kwa rangi zao mtu namba wani wa kulaumiwa ni jakaya kikwete kwakuingilia zoezi zima la kutunga huku akiubiri kutoingiza vyama lakini kwenye vikao vya siri na wana ccm wenzake wanapanga mbinu zote za kutetea katiba ki vyama.
 
Tunataka kura ya wazi kila mtu atusikie tunafanya nini kwenye bunge la katiba hakuna cha usiri hapa mambo yote wazi.
 
Wewe unamwamini Kikwete? Kikwete ni ndumilakuwili! Never trust him, that is how he is. Wakati wote huwa haeleweki anasimamia nini, ndiyo maana walio wajanja wanamzungusha kadiri wapendavyo.
Ndiyo maana kaweza kuongoza nchi mpaka hapa alipofika ujanja ni mhimi sana kwenye uongozi jk kathubutu kaweza na sasa anasonga mbele.
 
Back
Top Bottom