Chama cha siasa ni mkusanyiko wa watu wenye nia ya kuongoza taifa (na ambapo wananchi wana matakwa mengi na yanayotofautiana), kwa hivyo vyama vinachaguliwa na wananchi kwa kuelewa misimamo yao na sera zao. Waliopo bungeni wapo pale kwa niaba ya mimi na wewe kupitia chama, inachofanya CCM si kwamba inalinda maslahi ya chama tu bali na wapiga kura wao waliowachagua kwa kukielewa chama.
Kama mpiga kura kwakuwa sikupata kura ya maoni wala kuhojiwa kuhusu katiba, ni vyema chama nilichokipigia kura kilinde kilichonifanya kukipigia kura chaguzi zilizopita na popote maslahi yangu yanapo zungumziwa including kwenye bunge la katiba. Sasa wasitokee wanachama wenye misimamo tofauti ambayo aikuwa kigezo changu cha kumpa kura mwanachama wao hili aende kuniwakilisha, maana kuna vyama vingine vinavyojinada kwa mwendo mwengine ningeweza wapa kura yangu. Kwa maana hiyo kura ya siri ni kunilaghai mpiga kura nataka kujua umechagua nini kwa niaba yangu na kama ni zile sababu zilizonifanya nikipe kura chama chao na mwakilishi wangu. Vilevile chama cha siasa kina haki ya kulazimisha wanachama wake kulinda kanuni na misingi yao inayojinadi nayo kwa wananchi.