Mh. Pinda; Mbunge wa CCM atakayetetea kura ya siri atanyang'anywa kadi!

Mh. Pinda; Mbunge wa CCM atakayetetea kura ya siri atanyang'anywa kadi!

Hapo kura ya siri tu... je atakayeunga serikali tatu?
 
Tunataka kura ya wazi kila mtu atusikie tunafanya nini kwenye bunge la katiba hakuna cha usiri hapa mambo yote wazi.
Hiyo ndiyo demokrasia mliyonayo huko kwenu kutishia kunyanga'nya watu kadi Professor simiyu yetu???
 
Mheshimiwa waziri mkuu, Mizengo Pinda ametangaza kwenye kikao kilichowashirikisha baadh ya wabunge wa ccm kuwa atakayetetea kura ya siri atanyanganywa kadi ya chama! Vigezo na masharti yazingatiwe.
Mungu wangu!! Imefikia hapa!! eti hakuna mawazo huru kwa haya mashetani!! Ukiwa CCM lazima uwe kama mifugo ya viongozi!! Wanaogopa ukweli!! wamekwisha!!
 
Tunataka kura ya wazi kila mtu atusikie tunafanya nini kwenye bunge la katiba hakuna cha usiri hapa mambo yote wazi.

Kama mnataka uwazi, mbona mmepitisha waandishi wasiudhurie na kuripoti kwenye vikao vya kamati? Ndumilakuwili wakubwa nyie na mlaaniwe
 
Mungu wangu!! Imefikia hapa!! eti hakuna mawazo huru kwa haya mashetani!! Ukiwa CCM lazima uwe kama mifugo ya viongozi!! Wanaogopa ukweli!! wamekwisha!!

kama wanachokiamini kipo sahihi na kina manufaa kwa umma kwanini wana hofu na kura ya siri? Kwa wanatumia vitisho kuipisha kura ya wazi?

Demokrasia ni wengi wa pasipo kujali wako wapi hasa kwenye bunge kama hili
 
CCM wapo Dodoma kuhakikisha mchakato mzima wa kupata katiba mpya unaharibika kwa masilahi yao!
 
Finally viongozi wa CCM wameamua kulinda misimamo yao, taasisi zipo kwa sababu ya malengo fulani haiwezekani taasisi ambayo hipo kwa sababu ya kutoa elimu kuhusu uzazi wa mpango, elimu kama hiyo inaendana na vitu kama contraception nakadhilika halafu atokee member ambae kwa imani zake za kidini anapinga mbinu hizo na kutaka wazazi wajiamulie wenyewe. Swali la kujiuliza alienda kujiunga na kundi kufanya nini wakati anaelewa kabisa wapo kwa makusudi ya kuzuia uzazi usio na mpango in the first place na precautions ni njia moja wapo ya kutoa somo.

CCM kama chama cha siasa pia kina misimamo yake haiwezekani wanachama waone misimamo ya chama haifai unajiuliza walijiunga kwa sababu gani kama hawakubali foundation za chama ambacho ni zao la TANU na ASP mpaka leo watake vingine. Watu hawawezi kukurupuka na matatizo yao ya maisha waingie siasa bila ya kuvielewa vyama vya siasa na kutotaka kuheshimu misingi ya chama, na kama CCM wakiendelea kulea wanachama wa design hiyo ujue misuguano na malumbano haitoisha lazima kuwe na discipline within na wanachama kufuata misimamo ya chama navyojua mimi si tu vyama vya siasa bali taasisi zote sheria/kanuni/misimamo lazima zieshimiwe duniaini kote si Tanzania tu.

Wajumbe la bunge la katiba waache akili za kitoto kura ya siri ni akili za mimi nachotaka na kusimamia, wakati wajumbe wanaulamzima wakuwafahamisha wapiga kura wao na wanamakundi wenzao wamechagua nini na si nafsi zao zinataka nini ndio siasa zenyewe ppl have to compromise for the good of many ie political party.
 
Misimamo ya pamoja ni mizuri sana naunga mkono
 
WITO KWA WABUNGE WA BUNGE MAALUMU WAPENDA MABADILIKO YA KATIBA,CCM WAKIPITISHA KURA YA WAZI BASI MMUONDOKE BUNGENI MUWAACHE CCM WAJITENGENEZEE KATIBA YAO YA CHAMA.full stop ni kupotezeana muda kama niya thabiti ya kuwa na katiba mpya

Naunga mkono sana juu ya hili,ila hawawezi fanya hivyo
 
Ndiyo maana kaweza kuongoza nchi mpaka hapa alipofika ujanja ni mhimi sana kwenye uongozi jk kathubutu kaweza na sasa anasonga mbele.

Ujanjaujanja ni muhimu sana kwenye uongozi???? Hebu fafanua mzigo wangu.
 
katika moja ya hotuba za viongozi wakuu ilisomeka 'Mjiandae kisaikolojia kwa yatakayojiri huko Dodoma'
 
Tunataka kura ya wazi kila mtu atusikie tunafanya nini kwenye bunge la katiba hakuna cha usiri hapa mambo yote wazi.

Mnataka ours ya wazi ili kila mtu awasikie mbona mmekataa waandishi wa habari wasiingie kwenye vikao vya kamati ili watu wote wajue kinachoendelea
 
Sikuwahi kuamini, siamini hadi sasa kuwa mwenyekiti wa ssm anaweza kusimamia mabadiliko ya katiba yenye kunufaisha wananchi wote!
 
CCM wapo Dodoma kuhakikisha mchakato mzima wa kupata katiba mpya unaharibika kwa masilahi yao!
Baadhi ya Watanzania mnafurahisha sana.

Toka lini mchakato wa Rasimu ya Katiba ulikuwa mzuri?. Inaonekana neno 'kuharibika' ndiyo silifahamu.
 
Back
Top Bottom