Mh. Rais wetu kwanini shule za maeneo ya mjini Arusha ni wanawake? Mama mpumzishe Mchengerwa

Mh. Rais wetu kwanini shule za maeneo ya mjini Arusha ni wanawake? Mama mpumzishe Mchengerwa

saigilomagema

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2015
Posts
4,683
Reaction score
7,222
Mh. Rais wetu nchi hii ina ubaguzi mkubwa, kwanini mnawanyanyasa wanaume? Kwa mfano shule ya msingi na sekondari Kaloleni iliyoko Arusha mjini walimu wote zaidi ya 50 ni wanawake, kwanini, walimu wa kiume wako wapi. Jibu ni kwamba wale walimu ni wake wa viongozi pale Arusha, Mkurugenzi hana uwezo, mwenyr uwezo ni waziri, Mchengerwa si waziri sahihi TAMISEMI. Tuletee Ummy Mwalimu, watoto wa kiume wana haki ya kuifanya kazi maeneo ya mjini.

Mama chukulia mfano wa mwanao miaka yote ni kufanya kazi porini ungependa mama? Arusha ni eneo lililooza kwa rushwa mama, wasaidie watu wako
 
Iko hivyo Countrywise.

Hao Walimu, waume zao ndio wako huko Halmashauri/Manispaa husika.

Kitu kingine kama wewe ni Mwanaume haifai kugombania nafasi za kukaa mjini na Wanawake
 
Walimu wanawake wazuri wake zetu mabosi lazma wakae mjini kamavp wapewe kazi ofisi za halmashauri asee we vipi??
Navibinti vizuri navyo pia vinakaa kama michepuko yetu mabosi huelewi kituipi hapo??
We tichya kaa hukohuko kijijini lima,fuga na kufundisha
Unatakaje kukaa mjini huku huna gari,huna pesa ya bia,huna hata viwalo mnavaaga masuruali yenu mapaana ya selebresheni sitasita mji utakuwa hauvutii bana kuwa mwelewa!!
 
Usingemtaja Ummy kwenye uzi wako, ushauri wako ungechukuliwa.

Kwa kweli.
Kwanza huyo Ummy anaweza kuwa na msuli mnene wa kuwa Waziri wa wizara mtambuka kama hiyo ?
Usifanye mchezo!

Hata hivyo kama ni kweli hayo madai Basi yafanyiwe kazi, kusiwepo na upendeleo wa kijinsia.
Kuwe na uwiano na huwa na faida zake.
 
Back
Top Bottom