Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
Katika tukio la kipekee ambalo linakipa Kiswahili nafasi iliyopokwa siku nyingi ni tukio la muhadhara wa uprofesa kuendeshwa Kwa lugha ya Kiswahili.
Mchango mkubwa wa Profesa Mkandala katika hili siyo jambo dogo. Ni dhahiri kuwa ana mchango mkubwa yeye binafsi na kupitia historia yake ya kiuongozi.
Mihadhara ya aina hii ni nafasi adhimu ya lugha na kupitia nafasi hii Kiswahili kinaikanusha methali isemayo "nabii hakubaliki kwao" Kwa mara ya kwanza.
Mhadhara huu unatukumbushia pia machungu ya ajali ya kuzama kwa meli ya M.V Bukoba. Huku ukitoa sababu kadhaa ambazo zilitolewa na wataalam juu ya ajali hiyo. Maelezo hayo aliyoyanukuu Profesa Mukandala yanaonesha bila shaka kuwa lipo jambo la kujifunza mpaka leo. Maswali mengi juu ya ajali hiyo ya meli ya M.V Bukoba bado yaliacha maswali mengine.
Miaka 15 baada ya ajali ya M.V Bukoba meli nyingine aina ya MV. Spice one ilizama, Miaka saba baadae meli ya M.V Nyerere ilipata ajali. Swali ni nini tunajifunza?
Taasisi kubwa Duniani ni dola na soko. Dola na soko havipo sawa Kwa sababu mifumo ya masoko inatengenezwa na nguvu za dola hivyo ipo haja ya kutazama dola na soko kwenye ajali ya M.V Bukoba. Soko linafasiriwa kama njia za uzalishaji mali.
M.V Bukoba ilikufa ila taasisi yake haikufa. Mhadhara huu wa kipekee unatukumbusha historia ya kuvunjika kwa jumuia ya Afrika mashariki na hasara tuliyoipata Tanzania.
Michakato ya manunuzi ya meli haikufuata utaratibu wa manunuzi. Hakuna uhakika kuwa michoro ya meli na uwezo wake kama ilipitiwa.
Mikataba: Hakukuwa na upembuzi yakinifu hivyo hatua za kawaida za ununuzi hazikufuatwa.