Mhandisi: Reli ya SGR mpya kuchukua miaka 15 kumalizika

Mhandisi: Reli ya SGR mpya kuchukua miaka 15 kumalizika

February 19, 2020
Dar es Salaam, Tanzania

UJENZI WA DARAJA LA JUU LA SGR RELI KUINGIA STESHENI ULIPOFIKIA JIJINI DSM

Ujenzi wa daraja la juu jipya maalum kwa reli mpya ya SGR la urefu wa kilometa zipatazo 2.6 KM unavyoendelea jijini Dar es Salaam, Tanzania

Source: TRC RELI TV
 
Huu mradi wa SGR mipango ilikuwepo siku nyingi tatizo fedha haikuwepo,huyu Mzee wetu kaingia mzima mzima kutekeleza mradi huu mwisho wa siku taifa linaingia kwenye mikopo mikubwa yenye riba kubwa sijui kama huu mradi utakamilika maana na wapigaji nao wanazitaka hizo fedha zilizikopwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..reli ya Tazara ilijengwa toka mwaka 1970 mpaka 1975.

..reli hiyo ina urefu wa kilomita 1860 na ni ya kiwango cha cape gauge.
 
Unataka sema nini hapa maana hii yetu ni 450KM miaka 5 itapita

Sent using Jamii Forums mobile app

..ni swali ambalo wote tunatakiwa tujiulize.

..na Yapi Merkaz ni contractor mzuri amejenga reli ya kisasa ya Qatar.

..Na mkandarasi aliyejenga Tazara hakuwa na uzoefu na utaalamu alionao Yapi Merkaz.

..natarajia wataalamu wa masuala ya ujenzi, na haswa reli, watueleze changamoto za ujenzi huu.
 
February 16, 2020
Kilosa, Morogoro
Tanzania

Usafiri wa reli kurejea February 21, 2020 reli ya kati kufuatia ukarabati

Reli ya kati iliyoharibika inatazamiwa kuanza kutumika February 21, 2020. Mizigo zaidi ya tani 16,000 yakwama bandarini Dar es Salaam kutokana na kusitishwa kwa usafiri wa MGR Reli ya mkoloni.

Hayo yamesemwa wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, mhandisi Mh. Isack Kamwele alipotembelea maeneo ya mto Mkondoa kuona uharibifu wa reli ya MGR ya mkoloni na pia kwenda kukagua handaki namba mbili la reli mpya ya SGR kuona maendeleo ya ujenzi wa handaki hilo.

Kwa kutumia kiberenge, TRC RELI TV wakaamua kutembelea na kujionea kazi ya kuisogeza reli MGR ya mkoloni kiasi cha mita 10 toka mto Mkondoa. Kufanya hivyo wahandisi walichonga kingo za mlima na miamba iliyo pembeni mwa mto ili kuisogeza mita hizo 10 toka kandokando ya mto Mkondoa.

Source: TRC RELI TV

Toka maktaba / archive January 2019

January 24, 2019

Source: TRC Reli TV

Maoni ya mwananchi mzalendo January 2019 :

A.M
Hamwezi kudhibiti kwa njia hiyo hapo kidete kuna bwawa lililojengwa na mjerumani baada ya kupata kaidhia ya maji akajenga kupunguza kasi ya maji katika MTO mkondoa.

Bwawa lilimegwa 1997-98 kwenye mvua kubwa kuwahi kutokea elnino na kusomba kingo za bwawa toka kipindi hiko hakuja wahi kubaki salama hiyo kazi mnayoifanya inagharama kubwa.

Masikitiko haidumu maji yananguvu kubwa sana na yanahatarisha vijiji na miji kutoweka solution ni kuchimba tena bwawa LA kidete maarufu kama gombo maji yakija na nguvu yatatulizwa hapo na yatakua yanavujia juu ya kingo au lango la kupumulia yatakua yanatiririka kidogo kidogo.

Kinyume cha hapo hakuna njia mbadala kwa reli na usalama wa watu wa kilosa na vijiji vyake unapopita mto huu chukueni ushauri huu fanyieni kazi mtatulia bila hivyo majanga kila uchwao

1 year ago (2019)
...............................................................................

Fast forward mwaka 2020
January 2020

Mafuriko pia yanaathiri barabara inayotumika kwenda ktk ujenzi wa reli ya SGR maeneo ya Kilosa na kuchelewesha kazi kufanyika ndani ya muda uliokadiriwa. Hii ni kufuatia mvua kubwa zisizo za kawaida na uharibifu wa mabwawa ya kupunguza kasi ya maji kuingia mto Mkondoa na maeneo jirani

Ah.....hugo injinia mtanzania? Mzalendo....?

Sent using Jamii Forums mobile app

Hapa angalau tunapata taarifa za kiuhakika za kitaaalamu za reli, changamoto ya eneo kijiografia, masuala ya athari za mabwawa yaliyotelekezwa na pia hali ya hewa ya mvua nyingi kupita kiasi. Hizi habari zilizo wazi zinatupa walipa kodi mwelekeo juu ya ukweli wa changamoto kubwa ktk miradi ya MGR na SGR.

Ila masuala ya fedha kuwezesha mradi kukamilika na mchanganuo wa tegemeo la marejesho ya faida kiuchumi bado hakuna habari za kutosha toka kwa wahusika .
 
Mjinga wa
Inabidi jpm apambane sana kumuweka mtu wake ili aendeleze reli!lakini nikiingia mimi naipiga chini sitakagi ujinga kabisa!!!Stiglers wakati watu hawana maji wala umeme wa uhakika??
Mjinga wa karne hii.
 
February 21, 2020

SGR RELI UJENZI WA KIPANDE MOROGORO MAKUTUPORA WAFIKIA 25%

Source: TRC RELI TV
 
February 16, 2020
Kilosa, Morogoro
Tanzania

Usafiri wa reli kurejea February 21, 2020 reli ya kati kufuatia ukarabati

Reli ya kati iliyoharibika inatazamiwa kuanza kutumika February 21, 2020. Mizigo zaidi ya tani 16,000 yakwama bandarini Dar es Salaam kutokana na kusitishwa kwa usafiri wa MGR Reli ya mkoloni.

Hayo yamesemwa wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, mhandisi Mh. Isack Kamwele alipotembelea maeneo ya mto Mkondoa kuona uharibifu wa reli ya MGR ya mkoloni na pia kwenda kukagua handaki namba mbili la reli mpya ya SGR kuona maendeleo ya ujenzi wa handaki hilo.

Kwa kutumia kiberenge, TRC RELI TV wakaamua kutembelea na kujionea kazi ya kuisogeza reli MGR ya mkoloni kiasi cha mita 10 toka mto Mkondoa. Kufanya hivyo wahandisi walichonga kingo za mlima na miamba iliyo pembeni mwa mto ili kuisogeza mita hizo 10 toka kandokando ya mto Mkondoa.

Source: TRC RELI TV

February 21, 2020

Kazi usiku na mchana kukarabati reli ya kati inaendelea

Source: TRC Reli TV
 
Hapa angalau tunapata taarifa za kiuhakika za kitaaalamu za reli, changamoto ya eneo kijiografia, masuala ya athari za mabwawa yaliyotelekezwa na pia hali ya hewa ya mvua nyingi kupita kiasi. Hizi habari zilizo wazi zinatupa walipa kodi mwelekeo juu ya ukweli wa changamoto kubwa ktk miradi ya MGR na SGR.

Ila masuala ya fedha kuwezesha mradi kukamilika na mchanganuo wa tegemeo la marejesho ya faida kiuchumi bado hakuna habari za kutosha toka kwa wahusika .
basi shida sana......
 
February 23, 2020
Kilosa, Morogoro
Tanzania

Mhandisi wa SGR reli : Kazi ya Handaki namba 2 reli ya SGR kukwepa Mto Mkondoa kukamilika Julai 2020

Katika mazungumzo na mhandisi wa Yapi Merkezi ya Uturuki ambaye ni Project Manager wa kipande hicho cha reli ya SGR, atoa maelezo kuhusu kazi ya kumaliza mahandaki yote manne katika vilima karibu na mto Mkondoa. Ambapo handaki namba 2 lilo refu zaidi likiimarishwa kwa kusukwa kwa nondo maalum kabla ya kumwagiwa zege na linatazamiwa kukamilika mwezi Julai 2020. Daraja litajengwa kuunganisha baadhi ya mahandaki kuondokana kabisa na changamoto ya mto Mkondoa.

Pia bodi ya usajili ya Tanzania ERB imetumia mradi huu kama 'darasa' kwa kufika na wahandisi 30 kujifunza mambo mbalimbali yanayokwenda na mradi huu ili kuwajengea uwezo wa kutenda na kusimamia miradi mikubwa ya namna hii.

Source: TRC RELI TV

Mwaka 2019 kazi katika handaki # 2
Shuhudia video hapa chini wakati Handaki namba 2 lilipomalizika kutobolewa / kuchorongwa hapo December 5, 2019

Source : TRC Reli TV
 
February 23, 2020
Gulwe / Kilosa
Tanzania

Njia ya muda reli ya kati yafunguliwa

Mkurugenzi Mkuu wa TRC amesema njia ya reli ya muda kuwezesha treni reli ya kati / mkoloni kupita imefunguliwa wakati TRC wakiendelea kutafuta suluhisho la ujenzi wa njia ya kudumu.

Leo tarehe 23 February 2020 treni ya mizigo iliweza kupita katika njia hiyo ya muda ya reli iliyotengenezwa kufuatia reli ya kati kuharibiwa vibaya na mafuriko ya mvua nyingi zilizonyesha na kusababisha mto Mkondoa kujaa maji na kuleta uharibifu wa reli. Mhandisi wa TRC alisemea imewalazimu kufungua njia ya reli ya muda ili kuiunganisha nchi kwanza wakati wakitafuta suluhisho la kupata njia ya kudumu.

Source: ITV Tanzania
 
February 26, 2020
Morogoro, Tanzania

TRC yajikita kukarabati vichwa vya treni

Waziri mdogo wa Uchukuzi na mawasiliano atembelea karakana ya Shirika la Reli la Tanzania mjini Morogoro, Tanzania. Karakana hiyo ilifunguliwa mwaka 1982. Pia kuna karakana nyingine jijini Dar es Salaam.

TRC ina mtandao wa reli urefu wa jumla ya kilometa 2,700. Waziri anasisitiza mabehewa 200 yakarabatiwe na karakana za TRC ili hata sekta binafsi ikiingia kuwekeza mabehewa ya ziada basi Tanzania itakuwa na usafiri wa kutosha wa reli kwa kuwa na mabehewa mengi.

Pia karakana ya Morogoro itakarabati na kuvifanyia maintenance vichwa vya treni (locomotive) vya zamani vilivyofanya kazi ktk mtandao wa MGR ya mkoloni ili viweze kuendelea kutoa huduma bila wasiwasi.

Source: TRC RELI TV
 
Wahamishe njia za maji kwa kuyagawa gawa kabla haya jafika kwenye tuta la reli ili maji yaweze kukatiza reli kupitia kwenye vikaravati na madaraja madogo ya bei nafuu.
 
Back
Top Bottom