Mhandisi: Reli ya SGR mpya kuchukua miaka 15 kumalizika

Mhandisi: Reli ya SGR mpya kuchukua miaka 15 kumalizika

The planned railway line will depart from Uvinza district to Kigoma in Tanzania, via Musongati, Gitega Burundi and extends to the east of the Democratic Republic of Congo.

Mh. Rais Samia Hassan - Kipande cha Uvinza Tanzania hadi Gitega Burundi kujengwa bila mkopo, mwekezaji atajenga kwa pesa zake mwenyewe halafu kutakuwepo utaratibu wa kukatiana faida

 
12 January 2023

Tanzania's Standard Gauge Railway (SGR) Broke Record, With 2561 KM is The Longest in Africa



Tanzania Standard Gauge Railway (SGR) Project Timeline and all you need to know. Tanzania awards $2.2bn contract for Standard Gauge Railway project The 2,561 km rail line will connect the Indian Ocean port of Dar es Salaam to Mwanza on Lake Victoria
Source : Inter Vlog
 
23 January 2023

MKANDARASI NA PIA TRC WAHIMIZWA KUHARAKISHA MRADI



Hayo yamesemwa na naibu katibu mkuu wizara ya ujenzi na uchukuzi inayosimamia pia sekta ya reli alipotembelea kipande cha LOT 3 baada ya kusikia maelezo ya meneja mradi / project manager na consultant wa kipande hicho cha tatu yaani LOT 3.
 
16 February 2023

WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI ANA KWA ANA NA Bw. MASANJA KADOGOSA MKURUGENZI MKUU WA TRC

Wapewa taarifa za maendeleo ya mradi wa TRC ili waweze kutoa habari sahihi kuhusu mradi huu mkubwa wa reli ya SGR utakaokuwa na mtandao wa reli wa zaidi ya kilometa 2,000 za reli na kuwa mradi mkubwa kabisa kuweza kujengwa katika bara la Afrika na kuigeuza Tanzania kuwa kitovu na kimbilio la usafiri kwa nchi zaidi ya 7 ukanda huu wa Afrika abainisha mkurugenzi mkuu wa TRC Bw. Masanja Kungu Kadogosa kwa wahariri wa vyombo vya habari.
Source : TRC Reli TV
 
17 February 2023
Dar es Salaam, Tanzania

WAJUMBE WAPYA WA BODI YA TRC WATEMBELEA SGR DAR-MORO, MWENYEKITI ANENA, MAENDELEO NA UJIO WA VIFAA. PIA WATANZANIA WAWE NA SUBIRA NA IMANI JUU YA MRADI



Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Shirika la Reli Tanzania – TRC Prof. John Wajanga Kondoro ametambulisha wajumbe wapya wa bodi ya wakurugenzi TRC na kuwaaga wajumbe waliomaliza muda wao katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano ofisi ya makao makuu TRC jijini Dar es Salaam, Februari 2023.

Wajumbe wapya wa Bodi ya Wakurugenzi TRC waliotambulishwa ni Bw. Benjamini Adam Mbimbi, Bw. Kondo Abdalah Kibugula, Bw. Joseph Elias Salema, Bw. Juma Samhando Kijavara na Bw. Peter Mayunga Noni.

Wajumbe waliomaliza muda wao ni Bw. Wolfgang Ephraim Salia, Bi. Consolata Chrisostom Ngimbwa, Bw. Karim Godfrey Mattaka, Bw. Rogatus Hussein Mativila na Bw. Mahamud Mashaka Mabuyu.

Mwenyekiti wa Bodi Prof. Kondoro kwa niaba ya uongozi wa TRC amewashukuru wajumbe waliomaliza muda wao kwa mchango waliotoa kipindi chote walichokuwa katika nafasi za ujumbe na kuliwezesha Shirika kupiga hatua na kuongeza ufanisi katika utendaji wa Shirika.

“Lengo la kukutana hapa ni kutambuana na kutambua mchango wa wajumbe ambao wamelitumikia Shirika la Reli, waliingia katika kipindi ambacho tulikuwa kwenye sekeseke kuhusu maendeleo ya mradi wa SGR na mpaka tulipofika hapa, kwahiyo ni vyema kutambua mchango wao lakini pia kuwashukuru na kuwakaribisha wajumbe wapya” alisema Prof. Kondoro

Wajumbe wanaoendelea na nafasi zao ni pamoja na Bw. Jabir Bakari na Bi Lilian Ngilangwa. Baadhi ya wajumbe waliomaliza muda wao walipata fursa ya kutoa neno kwa menejimenti ya Shirika na kupongeza jitihada kubwa zilizofanywa kuhakikisha watumishi wanafanya kazi kwa weledi na kuleta tija katika utendaji wa Shirika.

“Nataka niwapongeze sana menejimenti hususani Mkurugenzi Mkuu, tunashukuru kwamba mradi unaendelea na vipande vyote vina wakandarasi, awali niliona menejimenti ni ndogo lakini nikupongeze Mwenyekiti kwa kuboresha muundo wa Shirika” alisema Bi. Consolata

Aidha, wajumbe wapya wamepata fursa ya kutembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa – SGR kuanzia Dar es Salaam hadi Dodoma kwa lengo la kufahamu namna mradi wa SGR unavyotekelezwa na Shirika la Reli Tanzania.

“Lengo la ziara ni kwamba tumepata wajumbe wapya wa bodi, hivyo ni vizuri kuwapitisha wakajua mifumo na miundombinu watakayokuwa wanaisimamia ikiwemo hii SGR, hii ni sehemu ndogo tu lakini wakati mwingine watapata kutembelea maeneo mengine” alisema Prof. Kondoro.
Sources : TRC RELI TV / https://www.trc.co.tz/news/prof-kondoro-atambulisha-wajumbe-wapya-bodi-ya-wakurugenzi-trc
 
17 February 2023

BODI MPYA YA WAKURUGENZI TRC, WATANZANIA WAWE WAVUMILIVU NA MRADI WA SGR

PROF. KONDORO ATAMBULISHA WAJUMBE WAPYA BODI YA WAKURUGENZI TRC

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Shirika la Reli Tanzania Prof. John Wajanga Kondoro akiwa na wajumbe wapya wa Bodi ya Wakurugenzi TRC waliotambulishwa Bw. Benjamini Adam Mbimbi, Bw. Kondo Abdalah Kibugula, Bw. Joseph Elias Salema, Bw. Juma Samhando Kijavara na Bw. Peter Mayunga Noni wakipata maelezo.

 

WADAU SEKTA BINAFSI WAKUTANA NA WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI​


11 APRIL 2023
Dar es Salaam, Tanzania

news title here



Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ameshiriki katika ufunguzi wa kongamano kati ya Sekta ya Uchukuzi na wadau wa sekta Binafsi (Ministerial Public Private Sector Dialogue – MPPD) lililofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC), Aprili 11, 2023.

Kongamano limekusudiwa kujadili shughuli zilizofanyika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja katika sekta ya uchukuzi, changamoto zinazoikumba sekta ya uchukuzi, mafanikio ndani ya mwaka mzima, pia kujadili sera na mikakati ya nchi inayolenga kukuza sekta ya uchukuzi nchini ili kuleta mafanikio.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amezitaka Mamlaka za Serikali kushirikiana na wafanya biashara kuhakikisha changamoto zinazowakabili zinatatuliwa haraka ili kurahisisha mazingira ya ufanyaji biashara Tanzania.

“Nipende kusema kuwa sekta binafsi ni wadau wakubwa sana wa Serikali, pengine kuna kanuni au taratibu ambazo zinawakwaza, sisi tuko maofisini nyinyi mnafahamu kuliko sisi, kupitia mikutano hii tunaamini tunaweza kujua na kuzifanyia kazi“ amesema Mbarawa.

Aidha, Mheshimiwa Mbarawa ameongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya ujenzi na uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) imelenga kujadiliana na sekta binafsi kupitia mikutano na makongamano mbalimbali ili kuzifahamu fursa, maboresho ya Sera, Sheria , kanuni na miongozo mbalimbali ili kujenga mzingira mazuri ya biashara .

“Ndugu washiriki Mheshimiwa Raisi Dk. Samia Suluhu Hassan, ametuagiza kwamba Wizara ikutane na sekta binafsi katika maeneo yetu ili kupokea maoni, changamoto na maboresho ya sera, Sheria na miongozo mbalimbali kwasababu bila kuwa na Sheria nzuri na kanuni nzuri zinazoendana na wakati hatuwezi kufanya biashara na kushindana na wengine” amesema Mbarawa.

Naye Mwenyekiti wa Sekta Binafsi nchini Bi. Angelina Ngalula amesema sekta ya uchukuzi inasaidia katika kupunguza gharama za bidhaa zinazozalishwa hapa nchini haswa katika sekta ya kilimo hivyo kuitaka Serikali iipe sekta ya uchukuzi kipaumbele kwa kuendeleza miundombinu ikiwemo reli na barabara .

"ukuaji wa sekta ya uchukuzi, itasaidia katika kupunguza gharama za bidhaa zinazozalishwa nchini hasa za kilimo, utakuta bidhaa kutoka China inauzwa gharama kuliko inayozalishwa hapa nchini, hii ni kutokana na gharama kubwa katika usafirishaji “ amesema Bi. Ngalula.

“Nchi yetu ni ya kimkakati na ina fursa nyingi sana, katika sekta hii tutambue sisi ni wanachama wa SADC, kwa hiyo tunapojadili Sera, mikakati na mambo madhubuti ya nchi, lazima tutunge Sera zinazoendana na ushindani wa soko, zikiwa ni Sera tofauti sisi ndio tutakaopoteza zaidi” alisema Bi. Angelina
Source : https://www.trc.co.tz/news/wadau-sekta-binafsi-wakutana-na-waziri-wa-ujenzi-na-uchukuzi

WADAU WATAKA TUSIJIWEKE KTK KITANZI CHA SADC, EAC TUTANUE WIGO WA INTELEJENSIA YA KIUCHUMI

Source : mlimani tv UDSM
 
Pia Reli mpya ya SGR itachukua takriban miaka 15 kumalizwa kujengwa
mbona tuliambiwa itaisha si zaidi ya miaka 5, na kile kipande cha Moro tuliambiwa kingekuwa kimeshaanza kufanya kazi kwa muda huu kulikoni tena.
 
TRC inapoteza zaidi ya milioni 100 kwa siku kutokana na kusitisha safari reli ya kati.
Swali tu, hivi Reli ya kati tuliyojengewa na mkononi kwa nini tumeshindwa kuitunza? sasa mnaona barabara mnajenga kwa gharama kubwa miroli usiku na mchana inaziharibu tunarudi kule kule, tungekuwa na mbadala wa mizigo kupitia reli ya Kati hata ajali zingepungua.

Hii nchi aisee !!
 
12 MAY 2023
TUNDU LISU KIBOKO !! AMEANIKA WIZI NA UFISADI MKUBWA ZAIDI MRADI SGR RELI MPYA , AHOJI FEDHA HIZI ZIMEENDA WAPI



Akinukuu ripoti ya CAG
  1. DSM - Moro 300km hivyo imezidi kilometa 100 ya ziada
  2. Moro - Makutupora ni 336 km lakini wajenga reli 422km kuna kilometa 90 za ziada
  3. Tabora Mwanza Kila kilometa moja ya reli bilioni 3.600 hivyo jumla ya trilioni 1.1 zimeenda wapi
  4. Tabora - Kigoma ...
Baada ya kupitia yanayoendelea ktk ujenzi wa reli ya SGR Mpya kama ilivyoripotiwa ktk ripoti ya CAG makamu mwenyekiti taifa wa CHADEMA Mh. Tundu Lissu anasisitiza katiba mpya ndiyo itaweza kukabiliana na masuala kama haya ya wizi wa kuongeza kilometa za reli na kuiba hizo fedha mchana kweupe kama ripoti ya Mkaguzi wa Mahesabu wa Serikali CAG ... na matatizo mengi mengine suluhisho ni katiba mpya ...
 
23 May 2023
Dodoma, Tanzania

MKURUGENZI AWEKA WAZI CHANGAMOTO RELI MPYA SGR



Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa akizungumza na waandishi wa habari nnje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya Bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuwasilishwa

Mkurugenzi wa TRC kuhusu matamanio ya kuanza kazi vipande vya reli mpya ya SGR ..
 
23 May 2023
Dodoma, Tanzania

NAIBU WAZIRI UCHUKUZI: MABEHEWA YA SGR YA GHOROFA KUINGIA MAPEMA MWEZI JUNI / JULAI

1685539755507.png
 
31 May 2023

MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AFAFANUA KUCHELEWA MAJARIBIO YA TRENI SGR DAR - MORO, MABEHEWA NA TRENI



Sababu za msingi za ucheleweshaji ni kuvunjwa mkataba na Eurowagon kampuni ya Uturuki iliyopewa tenda ya kukarabati treni na mabehewa.

Kampuni ya Ujerumani iliyochukua tenda ya kazi ya Eurowagon kampuni ya Uturuki ya kukarabati vichwa na mabehewa imepata changamoto ya vipuri.

Vipuri hivyo vinapatikana nchini Canada, hivyo kampuni ya Ujerumani imepata changamoto ya kutopata vipuri hivyo kwa wakati kwa ajili ya kumaliza kazi ya ukarabati ..

Canada imepata changamoto zinazoendelea ulimwengu ikiwemo Covid-19 pia masuala mengine yanayoikumba dunia hivyo kampuni ya Canada haijeweza kwenda na ratiba waliyoitazania Shirika la Reli Tanzania TRC ya matamanio kuwa kipande cha Dar-Moro reli mpya ya SGR treni ingekuwa imeshaanza kazi ..
 
05 May 2023
Kigoma, Tanzania

TRC YATUPIWA LAWAMA KUBWA KWA KUKOSA UWEZO WA KUSAFIRISHA MIZIGO KWA WAKATI

video courtesy of Millard Ayo

Hayo yamebainika kutokana na meli kukaa gatini katika bandari ya Kigoma kusubiri mizigo toka Dar es Salaam.

Stesheni master (meneja) wa kituo cha mwisho wa reli hapa Kigoma amesema ili tatizo hilo limalizike serikali inakusanya nguvu kukarabati mabehewa 600 ili iweze kukidhi mahitaji ya wateja wake wenye mizigo ya kuelekea Kigoma, Tabora na nchi jirani.

Ucheweleweshaji wa mizigo kufika ktk bandari ya Kigoma zinazigharimu meli kulipia tozo ya kupaki meli bandarini hivyo kusababisha gharama kubwa zaidi tofauti kama mizigo ingefika kwa muda ukioahidiwa na TRC.

Inabidi mawakala wa mizigo kuhangaika kuwasiliana na mamlaka ya bandari kuomba kusamehewa au kupata punguza la gharama za meli kusubiria mzigo bandarini.

Mawakala wana hofu kuwa watapoteza wateja na pia bandari bila kusahau TRC kukosa mapato maana wateja watatafuta aina nyingine ya usafiri usiohusisha reli na bandari ya Kigoma ili mizigo yao ifike nchi jirani kwa muda muafaka na kwa gharama nafuu.

Mawakala wanasema labda ipo haja ya TRC Shirika la Reli Tanzania na TPA Mamlaka ya Bandari Tanzania ziunganishwe kuwa shirika moja ili ufanisi wa kazi ya kusafirisha mizigo kwa njia ya bandari na reli uongezeke na kutoa ushindani kwa bandari na reli ya nchi jirani.
1685956689738.png

Photo : Kigoma port Tanzania. Courtesy of Millard Ayo@

Njia ya reli ya kati ya mkoloni bado ndiyo tegemeo kubwa kwa usafirishaji wa mizigo huku mradi wa reli mpya ya SGR ukiendelea kujengwa ambao utachukua zaidi ya miaka 10 (muongo mmoja / a decade) moja kukamilika hivyo reli ya MGR ya mkoloni ndiyo inayoibeba TRC, TPA na wateja wao hadi pale reli mpya SGR itapoanza safari za DSM-TBR- KGM

Picha chini Kipande cha reli mpya SGR toka DAR - MORO asilimia 98.14 kimekamilika
1685957200552.png

Photo: Courtesy of TRC RELI TV
 
Kampala, Uganda

Uganda kujenga reli ya SGR Mpya Kampala hadi Malaba

Habari za uhakika ni kuwa sasa Uganda ina nia ya kuongeza matumizi ya usafirishaji wa mizigo kwa reli kati ya Uganda na bandari ya Mombasa ili kupunguza gharama za usafirishaji mizigo baina ya bandari ya Mombasa Kenya hadi Uganda, Rwanda, DR Congo na South Sudan.

Mradi huo wa kilometa 273 wa reli mpya ya SGR Reli ya Uganda utaiunganisha na ule wa Kenya kupitia Malaba hadi Kisumu, Naivasha hadi bandari ya Mombasa Kenya.


Habari za ziada:
14 January 2023

Kampala, Uganda

Uganda has signed a memorandum of understanding with Turkish firm, Yapi Merkezi, to construct a standard gauge rail line from Malaba at the Uganda - Kenya border to the capital, Kampala. The 273-kilometer railway line will cost 2.2 billion U.S. dollars and it is expected to bolster rail services and lower transportation costs in the region.
Mratibu wa mradi SGR Uganda, Injinia Perez Wamburu amesema, Kampala imesaini makubaliano (MOU) na kampuni ya Kituruki ya Yapi Merkezi. Kampuni hiyo inatarajiwa kuwasilisha majibu ya mapendekezo ya serikali kuhusiana na ujenzi huo ndani ya wiki chache zijazo, ikifungua njia kwa ununuzi.

Kampala imesema ufadhili wa mradi huo pia utabadilika , Yapi Merkezi, ambayo inajenga reli ya Tanzania, inatarajiwa kushirikiana na mashirika yake ya utoaji wa mikopo (ECA) ili kufufua mradi huo.

Gazeti la The East Africa limeona mapendekezo kati ya serikali ya Uganda na wafadhili wanaotarajiwa kuufadhili mradi huo ikiwemo UK Export Fund, (UKEF) ambao Septemba mwaka jana ilihusishwa katika mjadala wa ufadhili wa ujenzi wa reli hiyo kwa gharama kati ya paundi 1.5 billion au $1.72 billion.

Kushindwa kwa benki ya Exim ya China kuendeleza mradi huo, Rais Yoweri Museveni mwaka jana aliwaelekeza maafisa wake watafute wafadhili kutoka taasisi nyingine za fedha duniani, London na UKEF zilikuwa taasisi za mwanzo kuwasiliana nao Septemba mwaka jana, Chanzo cha habari kilicho karibu na mradi huo kimeeleza.

Wambura amesema, Mwanasheria mkuu wa Uganda Kiryowa Kiwanuka kwa haraka aliupitia mkataba wa CHEC mara baada ya kuonekana kuwa Exim ya China --- Mfadhili wa mradi mkubwa wa miundo mbinu wa Kampala, kwa muda wa miaka kumi – imeshindwa kutoa ufadhili wa mradi huo
 
06 June 2023
Dar es Salaam, Tanzania

Mabehewa sita yaliyo karabatiwa na kampuni ya Lueckemeier Transport and Logistics GMBH ya nchini Germany yawasili bandari Dar es Salaam



LUECKEMEIER TRANSPORT AND LOGISTICS GMBH ya nchini Ujerumani ilipewa mkataba wa ukarabati wa behewa thelathini (30) na vichwa viwili (2) vya treni kufuatia kupewa tender na Shirika la Reli TanzaniaTRC baada ya kampuni ya Euro Wagon ya Turkey kushindwa kazi hiyo ya kukarabati, hivyo TRC mnamo tarehe 25 Februari 2022 kuuvunja mkataba baada ya kampuni ya EuroWagon ya Turkey kushindwa kukidhi matakwa ya mkataba.

Hatua iliyopelekea TRC kutafuta mkandarasi mwingine kampuni ya LUECKEMEIER TRANSPORT AND LOGISTICS GMBH ya Germany na kazi inaendelea vema.


Pia TRC ina mkataba wa behewa za SGR zilizotengenezwa na kampuni Sung Shin Rolling Stock Technology Limited (SSRST) kutoka Korea ya Kusini.

Kwa sasa TRC inasimamia mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa – SGR awamu ya kwanza Dar es Salaam – Mwanza , pia SGR kwenda Tabora hadi Kigoma na kazi za ujenzi zinaendelea vema.
 
UMUHIMU WA MAMLAKA YA BANDARI TANZANIA TPA NA SHIRIKA LA RELI TANZANIA KUFANYA KAZI KWA PAMOJA

Hili suala halina ubishi kwani ufanisi wa mizigo kuwafikia wateja wa ndani ya nchi na nchi jirani za Burundi, Rwanda, DR Congo unategemea sana muunganiko wa ufanisi katika mashirika ya mawili muhimu katika uchukuzi na kujenga imani wateja kutumia miundo mbinu ya Bandari na Reli inayofanyiwa uwekezaji mkubwa .

Tumkumbuke kuwa washindani wa bandari ya Dar es Salaam na SGR reli mpya ya Tanzania yaani bandari ya Mombasa Kenya pamoja na SGR reli ya Kenya hawalali kuhakikisha wanaongeza ufanisi na kuvutia wateja kutumia bandari na reli ya nchi hiyo jirani.

TOKA MAKTABA:
01 October 2021

SGR KENYA Kuelekea Malaba NA Uganda Itapiga Jeki Biashara​


Na CHARLES WASONGA

TANGAZO la Shirika la Reli nchini (KRC) kwamba huduma za treni kati ya Mombasa na miji ya Kisumu na Malaba zitaaza tena Novemba mwaka huu ni habari njema kwa wafanyabiashara wa humu nchini.


Vilevile, kurejeshwa kwa huduma hizo za uchukuzi wa bidhaa na abiria kutachochea ukuaji wa uchumi ambao umeathiriwa pakubwa na makali ya Covid-19, miongoni mwa changamoto nyinginezo.

Mkurugenzi Mtendaji wa KRC, Philip Mainga wiki jana alisema kuwa huduma hiyo itafanikishwa baada ya kukamilika kwa ujenzi wa reli inayounganisha reli ya kisasa (SGR) katika eneo la Mai Mahiu na reli ya zamani katika eneo la Longonot karibu na mji wa Naivasha.

Afisa huyo aliambia wabunge wanachama wa Kamati ya Fedha kwamba ujenzi wa reli hiyo mpya uligharimu Sh3.5 bilioni.

Mradi wa ukarabati wa reli ya zamani kutoka Naivasha hadi mji wa Malaba ulioko katika mpaka wa Kenya na Uganda na laini ya kutoka Nakuru hadi Kisumu uligharimu jumla ya Sh3.8 bilioni.

Kwa hivyo, kwa kutumia Sh7.3 bilioni pekee, shirika la KRC litawezesha uchukuzi wa bidhaa na abiria kutoka Mombasa hadi taifa jirani la Uganda, kupitia mji wa Malaba, kwa gharama nafuu.

Aidha, mizigo kutoka Mombasa itasafirishwa hadi Kisumu kisha ipakiwe kwa meli katika bandari mpya ya Kisumu na kusafirishwa hadi Uganda.

Ukarabati wa bandari hiyo uligharimu Sh3.2 bilioni.Hii itaimarisha biashara kati ya Kenya na mataifa jirani ya Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Rwanda ambayo hayajapakana na bahari.

Kwa mfano, kulingana na takwimu za hivi punde zilizotolewa na Shirika la Kitaifa la Takwimu (KNBS) Kenya iliuza bidhaa za Sh24.04 bilioni kati ya Mei na Juni mwaka huu.

Hii ni mbali na mapato kutoka kwa bidhaa zilizouzwa Uganda, ikiwemo mafuta, ambayo hutua katika bandari ya Mombasa na kusafirishwa kwa barabara hadi Uganda.

Hivi majuzi, Rais wa DRC, Felix Tshisekedi alizuru nchini na kutia saini mkataba wa kibiashara wa thamani ya Sh92 bilioni kwa mwaka kati ya nchi yake na Kenya.

Kwa hivyo, sasa ni wajibu wa Kenya kupalilia uhusiano mzuri wa kidiplomasia na mataifa haya jirani ili iweze kufaidika kibiashara.

Kunawiri kwa biashara kati ya Kenya na mataifa haya bila shaka kutaliletea taifa hili mapato yatakayoliwezesha kupunguza zigo la madeni linayodaiwa na mataifa ya nje hasa China.

Kufufuliwa kwa shughuli za uchukuzi kwa reli kati ya Mombasa na miji ya Kisumu na Malaba pia kutawezesha mradi wa SGR kuvuna faida kubwa, hususan, kupitia usafiirishaji wa mizigo hadi maeneo ya bara na mataifa jirani.

Tangu kuzinduliwa kwa huduma za uchukuzi wa bidhaa kupitia reli hiyo mpya, mapato kutokana na uchukuzi wa mizigo imekuwa finyu zaidi hali iliyotilia shaka faida ya mradi huo wa SGR uliogharimu Sh347 bilioni.Aidha, laini kutoka Nairobi hadi Mai Mahiu iligharimu Sh150 bilioni, pesa ambazo zilikopwa kutoka serikali ya China.I

sitoshe, kurejelewa kwa safari za treni kutoka Nakuru hadi Kisumu na hatimaye Butere kutaimarisha biashara katika miji ya Molo, Elburgon, Londiani, Koru, Muhoroni na Chemelil ambayo ilififia baada ya kusitishwa kwa huduma hizo miaka 15 iliyopita.Changamoto sasa ni kwa serikali na shirika la KRC kuhakikisha inatoa huduma bora na za kutegemewa na wateja.
Source : CHARLES WASONGA: SGR kuelekea Malaba itapiga jeki biashara – Taifa Leo
 
9 Jun2023

Gerson Msigwa - Watanzania msikubali kupotoshwa



Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa ametoa wito kwa Watanzania kutokubali watu wachache kuwatoa kwenye reli, na badala yake wasimame na Serikali ambayo imeamua kufunga mkanda kuhakikisha kuwa Reli ya Kisasa (SGR) inakamilika.
 
Back
Top Bottom