Mhariri: Diamond Platinumz aangukia pua tuzo za BET

Mhariri: Diamond Platinumz aangukia pua tuzo za BET

Burna Boy Ametangazwa ndio MSHINDI wa Bet Award katika Mashindano Ambayo Msanii Diamond Platnum alikuwa Anashiriki na Kuangukia Pua

====
Hatimaye mshindi wa tuzo za BET katika kipengele cha Best International Act’, atajwa kuwa ni Burna Boy.

Burna Boy ametajwa kushinda tuzo hiyo usiku wa kuamkia leo Juni 28, 2021 ambapo kilele cha utoaji tuzo hizo umefanyika, nchini Marekani.

Ushindi wa msanii huyo kutoka Nigeria, unamfanya awabwage washindani wake waliokuwa wakichuna katika kipengele hicho akiwemo Diamond Platnumz kutoka Tanzania na Wizkid kutoka nchini Nigeria.

Wengine waliokuwa katika kipengele hicho ni Aya Nakamura (Ufaransa),Emicida (Brazili), Headie One (Marekani) Young T & Bugsey (Marekani) na Youssoupha (Ufaransa)

Vilevile hii inakuwa mara ya tatu kwa Burna Boy kushinda kipengele hicho kwani alishachukua tuzo tena mwaka 2019 na 2020.

Tuzo za BET zilianza kutolewa mwaka 2001, zinazoandaliwa mahususi kwa ajili ya kusherehekea mafanikio ya kazi za Wamarekani weusi katika sanaa ya muziki, uigizaji, michezo, zinatolewa usiku wa leo huko nchini Marekani.

1624859909917.png


Pia soma:
 
Watu walishamuwekea gundu mapema hivyo kukosa kwake kulitarajiwa.

Ila jambo jema ni kwamba amewawakilisha vyema watu wa Jamii ya Kimasai wa kutokea kule Kenya na Tanzania.

Hongera kwake walau kwa kushika nafasi ya Tatu.
 
Unajiita Eng hata kuandika hujui?

Anyway, lengo lao halikua asisinde, lilikua aondolewe kwenye kinyang'anyiro.

Kushinda ama kushindwa ni matokeo tu ya mchezo.
”….halikuwa asishinde, lilikuwa…”

Halafu eti unajiita Hakimu na unabeza wenzako!

Wewe ni Guruguja aliyechangamka.🤏[emoji2535][emoji276]
 
Wizi wa kura, maboksi yalikuwa yamejaa kura hata kabla ya kura kupigwa!. Lissu ni shahidi.
 
  • Thanks
Reactions: _ly
Hongera sana Diamond kwa kushiriki,ulishindanishwa na wasanii wakali wenzako,na ameshinda aliyeshinda,jipange wakati mwingine unaweza kushinda wewe,big up sana mtoto wa Tandale

Karibu tena Bongo
 
Watu walishamuwekea gundu mapema hivyo kukosa kwake kulitarajiwa.

Ila jambo jema ni kwamba amewawakilisha vyema watu wa Jamii ya Kimasai wa kutokea kule Kenya na Tanzania.

Hongera kwake walau kwa kushika nafasi ya Tatu.
gundu! almasi anawezaje kumshinda burna boy ambaye anatoa ngoma kali na albam bora duniani?
almasi ana albam ngapi na burna ana albam ngapi?
burna boy ni next level nyinyi.
 
Back
Top Bottom