Mhasibu, Afisa TEHAMA wa Kanisa la SDA wapandishwa kizimbani kwa Wizi wa Tsh. Milioni 717

Watu watatu wakiwemo Mhasibu na Ofisa Tehama wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (SDA), wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashitaka manane, likiwamo la kutakatisha fedha na wizi wa Sh717 milioni mali ya kanisa hilo.

Washitakiwa hao ni ofisa Tehema, Wilson Mapande (35) mhasibu, Winnie Owino (33) na mfanyabiashara, Nicolaus Owino (29).

Watatu hao wamefikishwa mahakamani hapo jana Septemba 25, 2024 na kusomewa mashitaka na Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga akishirikiana na Wakili wa Serikali, Aaron Titus.

Kabla ya kuwasomea mashitaka, hakimu Malewo alisema washitakiwa hawatakiwi kujibu chochote kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.

Amesema mashitaka ya kutakatisha fedha yanayowakabili washitakiwa hayana dhamana kwa mujibu wa sheria, hivyo wanatakiwa kusikiliza mashitaka na hawatatakiwa kujibu chochote.

Akiwasomea mashitaka, wakili Katuga amedai wanakabiliwa na mashitaka manane, la kwanza likiwa ni kuongoza genge la uhalifu, la pili wizi na la tatu hadi la nane ni utakatishaji fedha.

Katika shitaka la kwanza linalowakabili washitakiwa wote, amedai kati ya Mei 2021 na Januari 2023, waliongoza genge la uhalifu kisha kujipatia Sh717.126 milioni kutoka kwenye akaunti ya benki ya CRDB mali ya kanisa hilo.

Shitaka la pili la wizi linamkabili Mapande pekee, anayedaiwa kati ya Mei 2021 na Januari 2023 akiwa mtumishi wa kanisa hilo aliiba Sh717 milioni.

Katika shitaka la tatu la utakatishaji fedha, inadaiwa kwa kipindi hicho Mapande alifungua akaunti benki ya CRDB yenye jina lake akaingiza Sh396.629 milioni.

Shitaka la nne linawakabili Mapande na Winnie wanaodaiwa katika kipindi hicho walifungua akaunti benki ya CRDB yenye jina la Winnie wakaingiza Sh208.468 milioni.

Mbali na hilo, Mapande na Owino wanadaiwa katika shitaka la tano walifungua akaunti benki hiyo na kuingiza Sh112.029 milioni kwa jina la Owino.

Shitaka la sita hadi la nane, linamkabili Mapande na Winnie wanaodaiwa katika kipindi hicho walitumia fedha hizo kununua magari mawili aina ya Toyota Harrier na Toyota Crown. Pia wanadaiwa kununua nyumba eneo ambalo halijapimwa katika Mtaa wa Mtambani, Mapinga, Bagamoyo.

Upande wa mashitaka umedai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika, hivyo umeiomba Mahakama kuipangia kesi hiyo tarehe kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Malewo ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 9, 2024 kwa ajili ya kutajwa. Washitakiwa wote wamepelekwa rumande.

MWANANCHI
 
Attachments

  • FB_IMG_1727368868627.jpg
    FB_IMG_1727368868627.jpg
    57.3 KB · Views: 6
Sasa kuna haja gani ya kwenda kanisani si tuwe tu tunaabudia nyumbani katika roho na kweli badala ya kwenda kanisani kukamuliwa sadaka halafu zinaibiwa na wajanja wachache?

Waebrania 10.25

"wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia"

wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine 👉 kukusanyika ni desturi ya watu wa MUNGU Mkuu Also ni muhimu kwaajili ya kufahamiana na watu mbalimbali na kwenda KUSIKIA kanuni na maelekezo yanayotuongoza kumuabudu MUNGU

Naludia tena MUNGU haabudiwi Mahali fulani Mfano nyumbani au Mahali popote bali anaabudiwa katika Roho na katika kweli

Neno "katika" kwa kiswahili chepesi ni 👉 " Ndani ya"

Kweli ni NENO la MUNGU Ndio hutupa kanuni na taratibu na maelekezo ya kumuabudu MUNGU kwa kila sekunde ipitayo Kwaiyo hatuwezi kumuabudu MUNGU nje ya NENO lake never
 
Watu watatu wakiwemo Mhasibu na Ofisa Tehama wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (SDA), wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashitaka manane, likiwamo la kutakatisha fedha na wizi wa Sh717 milioni mali ya kanisa hilo.

Washitakiwa hao ni ofisa Tehema, Wilson Mapande (35) mhasibu, Winnie Owino (33) na mfanyabiashara, Nicolaus Owino (29).

Watatu hao wamefikishwa mahakamani hapo jana Septemba 25, 2024 na kusomewa mashitaka na Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga akishirikiana na Wakili wa Serikali, Aaron Titus.

Kabla ya kuwasomea mashitaka, hakimu Malewo alisema washitakiwa hawatakiwi kujibu chochote kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.

Amesema mashitaka ya kutakatisha fedha yanayowakabili washitakiwa hayana dhamana kwa mujibu wa sheria, hivyo wanatakiwa kusikiliza mashitaka na hawatatakiwa kujibu chochote.

Akiwasomea mashitaka, wakili Katuga amedai wanakabiliwa na mashitaka manane, la kwanza likiwa ni kuongoza genge la uhalifu, la pili wizi na la tatu hadi la nane ni utakatishaji fedha.

Katika shitaka la kwanza linalowakabili washitakiwa wote, amedai kati ya Mei 2021 na Januari 2023, waliongoza genge la uhalifu kisha kujipatia Sh717.126 milioni kutoka kwenye akaunti ya benki ya CRDB mali ya kanisa hilo.

Shitaka la pili la wizi linamkabili Mapande pekee, anayedaiwa kati ya Mei 2021 na Januari 2023 akiwa mtumishi wa kanisa hilo aliiba Sh717 milioni.

Katika shitaka la tatu la utakatishaji fedha, inadaiwa kwa kipindi hicho Mapande alifungua akaunti benki ya CRDB yenye jina lake akaingiza Sh396.629 milioni.

Shitaka la nne linawakabili Mapande na Winnie wanaodaiwa katika kipindi hicho walifungua akaunti benki ya CRDB yenye jina la Winnie wakaingiza Sh208.468 milioni.

Mbali na hilo, Mapande na Owino wanadaiwa katika shitaka la tano walifungua akaunti benki hiyo na kuingiza Sh112.029 milioni kwa jina la Owino.

Shitaka la sita hadi la nane, linamkabili Mapande na Winnie wanaodaiwa katika kipindi hicho walitumia fedha hizo kununua magari mawili aina ya Toyota Harrier na Toyota Crown. Pia wanadaiwa kununua nyumba eneo ambalo halijapimwa katika Mtaa wa Mtambani, Mapinga, Bagamoyo.

Upande wa mashitaka umedai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika, hivyo umeiomba Mahakama kuipangia kesi hiyo tarehe kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Malewo ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 9, 2024 kwa ajili ya kutajwa. Washitakiwa wote wamepelekwa rumande.

MWANANCHI
Mmh wasabato wanapenda kesi sana hao jamaa nawaonea huruma ingekuwa madhehebu mengine wangefungafunga yaishe ila hapo watatafute wanasheria wanzuri tu angalau issue iwe ndogo mahakamani..
 
Hizi HeLa ni mfumo wa digital ulichezewa na insiders.
Tuliaminishwa tuhamie digital ndo juu kwa juu wakapiga. Ndo maana kuna afisa tehama na wahazini hapo. Na bado chain ni ndefu basi tu waliokutwa na hatia moja kwa moja ni hao
CRDB
 
Walishafutwa
Tuhuma hizi kwakuwa fedha ziliwekwa kwa account zao zinatosha kabisa kuwatoa
Imagine pesa inawekwa kwa akaunti ya mtu binafsi as if Kanisa haina Bank account..kuaminiana sana kunatugharimu wakati Pesa hiyo hiyo ilimsaliti Yesu..Ifike pahala makanisa yatengeneza mifumo ya kuthibiti utakatishaji fedha kuwafuta ushirika tu haitoshi na zitungwe sheria za kuwawajibisha hawa wezi hakuna kuchuachia Mungu tena
 
Hizi zilihamishwa kwa wizi wa kidigitali sio kwa hiyari ya kanisa
 
Kesho sadaka zitapungua Sanaa
Unasali wapi cacutee kesho nije kanisani kwenu. Nilishaacha kutoa sadaka mda sana. Natoa for a purpose only, makambi, majengo..hivyo yani.
 
Nasali mbezi juu
Ila zaka usiachee
 
kwa hiyo lengo la kuzihamisha katika account zao binafsi lengo nini hasa? mbona pesa mingi sana au walikuwa wanahamishia kidogo kidogo kwa account zao binafsi kwa kipindi kirefu hadi account zao zikavimba wakashtukiwa ? Hii ni cheni kubwa ufanyike uchunguzi.
 
Wajinga wakileta PESA ni kuzipiga tu,,,, sasa kwanini wapelekwe Kizimbani,, si mfanye MAOMBI na MAOMBEZI na Mungu atatenda? 🤣 🤣
Dini ni UTAPELI...
 
Mwasomola ameomba raisi samia ashughulike na Hawa wezi wa hizi pesa
 
Back
Top Bottom