Mhasibu, Afisa TEHAMA wa Kanisa la SDA wapandishwa kizimbani kwa Wizi wa Tsh. Milioni 717

Mhasibu, Afisa TEHAMA wa Kanisa la SDA wapandishwa kizimbani kwa Wizi wa Tsh. Milioni 717

IMG-20240926-WA0003.jpg


Matumizi ya hizi pesa sasa utachokaaaa
 
Hivi mashtaka ya wizi wa fedha za kanisa yanawahusu nini mawakili wa serikali? Au SDA inamilikiwa na serikali?
Hapo kwenye utakatishaji.Huwa wana Bibilia na kanuni ya kanisa kama katiba yao, hivyo huenda kama Kanisa wametumia njia zote za kanisa hao mafisadi wamekaidi na kushupaza shingo zao ,sasa kama sikosei kanuni yao inasema washughulikwe kama watu wa mataifa kufuatana pia na Mathayo 18:15-17 japo ni hatua ya mwisho kabisa
 
Wadau hamjamboni nyote?

#Repost @mwananchi_official
——
Watu watatu wakiwemo Mhasibu na Ofisa Tehama wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (SDA), wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashitaka manane, likiwamo la kutakatisha fedha na wizi wa Sh717 milioni mali ya kanisa hilo.

Washitakiwa hao ni ofisa Tehema, Wilson Mapande (35) mhasibu, Winnie Owino (33) na mfanyabiashara, Nicolaus Owino (29).

Watatu hao wamefikishwa mahakamani hapo jana Septemba 25, 2024 na kusomewa mashitaka na Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga akishirikiana na Wakili wa Serikali, Aaron Titus.

Kabla ya kuwasomea mashitaka, hakimu Malewo alisema washitakiwa hawatakiwi kujibu chochote kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.

Amesema mashitaka ya kutakatisha fedha yanayowakabili washitakiwa hayana dhamana kwa mujibu wa sheria, hivyo wanatakiwa kusikiliza mashitaka na hawatatakiwa kujibu chochote.

Akiwasomea mashitaka, wakili Katuga amedai wanakabiliwa na mashitaka manane, la kwanza likiwa ni kuongoza genge la uhalifu, la pili wizi na la tatu hadi la nane ni utakatishaji fedha.

Katika shitaka la kwanza linalowakabili washitakiwa wote, amedai kati ya Mei 2021 na Januari 2023, waliongoza genge la uhalifu kisha kujipatia Sh717.126 milioni kutoka kwenye akaunti ya benki ya CRDB mali ya kanisa hilo.

Soma zaidi katika tovuti ya Mwananchi

(Imeandikwa na Hadija Jumanne)

#mwananchiupdates
#tunaliwezeshataifa
 
Hii nchi ngumu sana. Hata kule KKKT usione akina Malasusa wanapang'ang'ania. Sio bure. Wanatumia hadi ndumba kuingia madarakani ili tu wapige hela. Hakuna cha kutumikia Mungu wala nini Watu wanatumikia matumbo yao.
Mambo ni mengi hata kule katoliki wanaua ma albino.
 
Mwingine kapiga million 200 hapo makanisa ya Kati mikocheni (sitataja kanisa). Amepiga kwenye lipa namba. Ashajenga mjengo mbweni amehama na kanisa. Mhazini Yule alikuwa mlevi kupindukia na mzee ww bata sanaaa.
Analipa kwa mwez sijui laki 4 zile kila mwezii
Na hapo wazee wa kanisa bado wamemtetea eti kanisa haliendi mahakamani.
 
Mwingine kapiga million 200 hapo makanisa ya Kati mikocheni (sitataja kanisa). Amepiga kwenye lipa namba. Ashajenga mjengo mbweni amehama na kanisa. Mhazini Yule alikuwa mlevi kupindukia na mzee ww bata sanaaa.
Analipa kwa mwez sijui laki 4 zile kila mwezii
Na hapo wazee wa kanisa bado wamemtetea eti kanisa haliendi mahakamani.

Watu wanaotumia mazoea ya namna hiyo NI wabaya sana
 
Ikibainika kama ni kweli hawa wafutwe ushirika haraka sana
Pesa azile Mwoposa peke yake si ndio oya hapo machinjioni na nyinyi pigeni tukio IT umelala lala tu wenzio wanapiga pesa huku we kazi kurekebisha majukwaa ya mwoposa tu na kutengeneza graphics za matangazo yake piga hela hizo hapo
 
Back
Top Bottom