Mhasibu afungwa miaka 76 kwa kufoji risiti na kujipatia tsh. mil. 97

Mhasibu afungwa miaka 76 kwa kufoji risiti na kujipatia tsh. mil. 97

is Mungai still alive? lakini najiuliza kitu kimoja: Hivi huyu mary alikuwa hafanyi ukaguzi wa fedha zake kama zinaingia benki? It is simple maana unajua kuwa ni muhula wa kulipa ada, inabidi uone hela inatuna kwenye akaunti zako za benki. Mama Mzembe!
Mungai kafa muda sana...i think 2015
 
Bernard Mnyilenda (51) amehukumiwa kifungo cha miaka 76 jela baada ya kukutwa na hatia kwa makosa 22 ya kugushi kitabu cha risiti na kukitumia kupokea malipo ya ada katika Shule ya Southern Highland Mkoani Iringa.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa imeeleza kuwa Mnyilenda ambaye alikuwa mhasibu wa shule hiyo mwaka 2018-2022, aliwashawishi wazazi kulipa malipo taslim badala ya kufanya malipo kupitia benki na jumla.

Alipopewa nafasi ya kujitetea mtuhumiwa alisema anaomba Mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa wazazi wake wanamtegemea yeye.

Aidha, pamoja na adhabu hizo, Mahakama imemtaka Mnyilenda kurejesha fedha Tsh, Milioni 116.3.

Source: Azam TV
 
Huyo jamaa mjinga vihela vya shule vidogo sana ni rahisi kujulikana. Sasa mtu kalipa na mwanaye yuko hapo.Mkuu wa Shule hela hazioni ila wewe unadai wamelipa. Ni alilo hizo au matope.

Alijaribu kamba yake sasa imekatika.
Inaonekana hiyo aliipiga kwa mda mrefu kidogo kidogo
 
Huyo jamaa mjinga vihela vya shule vidogo sana ni rahisi kujulikana. Sasa mtu kalipa na mwanaye yuko hapo.Mkuu wa Shule hela hazioni ila wewe unadai wamelipa. Ni alilo hizo au matope.

Alijaribu kamba yake sasa imekatika.
Wazazi walikuwa wakilipa cash kwa huyo mhasibu au wakiingiza kwenye akaunti ya shule moja kwa moja?
 
is Mungai still alive? lakini najiuliza kitu kimoja: Hivi huyu mary alikuwa hafanyi ukaguzi wa fedha zake kama zinaingia benki? It is simple maana unajua kuwa ni muhula wa kulipa ada, inabidi uone hela inatuna kwenye akaunti zako za benki. Mama Mzembe!
Wana hela nyingi sana hawa na vyanzo vingi pia.
 
Bernald Mnyilenda aliyekuwa Mhasibu wa Shule ya Southern Highlands amehukumiwa kifungo hicho baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa kumkuta na hatia ya kutumia kitabu ghushi cha Risiti na kupokea ada kiasi cha Tsh. milioni 97.

Mahakama hiyo imemkuta na makosa 22 baada ya kusikiliza Mashahidi 7 wakiwemo wakaguzi wawili, mmiliki wa shule hiyo, Marry Joseph Mungai na baadhi ya wazazi waliothibitisha kulipa ada na kupewa risiti zilizokwisha muda wa matumizi.

Hakimu Mkazi Mkuu Said Ally Mkasiwa, alikataa utetezi wa Mtuhumiwa aliyeomba kupunguziwa adhabu na kusema hajaona ushawishi, hivyo anastahili hukumu ya miaka 76 na kutakiwa kurejesha Tsh. Milioni 116.3.
Ana umri gani? Kila la kheri na maisha marefu kwake! Alipe atakapotoka.
 
IMG_20220831_055125.jpg
 
is Mungai still alive? lakini najiuliza kitu kimoja: Hivi huyu mary alikuwa hafanyi ukaguzi wa fedha zake kama zinaingia benki? It is simple maana unajua kuwa ni muhula wa kulipa ada, inabidi uone hela inatuna kwenye akaunti zako za benki. Mama Mzembe!
Mungai alikufa kifo cha kutatanisha baada ya kunywa kinywaji kilichodhaniwa kuwa na sumu enzi za utawala wa JPM huko Jijini Darisalama.

Na kuhusu kutogundua mapema; kama walivyojibu baadhi ya wadau hapo juu! Hiyo familia ni ya kibepari, hivyo fedha ipo. Ingekuwa hiyo shule ni ya mlala hoi kama mimi, huo wizi ungegundulika mapema sana.
 
mh ! asiporejesha hizo hela nini kinatokea ?

wanasheria mna la kutuambia ?
 
Back
Top Bottom