Mhe. Tundu Lissu, Please Acha Kumsulubu Spika Wetu! Unammaliza Kabisa Hadi Ameshindwa Kazi!

Mhe. Tundu Lissu, Please Acha Kumsulubu Spika Wetu! Unammaliza Kabisa Hadi Ameshindwa Kazi!

Mkuu Pasco huyu TL analifaamu ilo kabisa na nahisi huwa anafanya maksudi kabisa...hata angekua mtoto maadamu anasimamia CCM tundu lisu huruma hiyo hana.. Ni anti state kitambo sana.
 
Last edited by a moderator:
Pasco napenda sana style yako ya uandishi na ku present hoja (unauma na kupuliza). Ila wacha akipate huyo mama huwa anajibu kijeuri sana.
 
Last edited by a moderator:
Wanabodi,

Leo nimepata fursa ya kuliangalia bunge live asubuhi hii kupitia TBC-1,
Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda ameshindwa kabisa kuliendesha bunge!, amepwaya sana na ameendesha kika bila confidence kabisa na mwisho wa maelezo yake, akamtaja Mhe. Tundu Lissu kama ndiye mbunge anayeongoza kwa kuleta vurugu bungeni, na Lissu aliponyanyuka kuomba muongozo wa Spika, akamvurumishia tena Spika Makombora mazito, na kama angeendela kidogo tuu!, Spika Makinda ange break down kwa machozi!. (Naamini akifika ofisini kwake, atajifungia kidogo na kuimalizia hasira yake the same way wanawake wote wanamalizaga hasira zao!.

Kwa kuzingatia sifa kuu iliyomfanya Mhe. Mama Makinda kuchaguliwa kuwa spika, huku Mhe. Tundu Lissu akiujua fika uwezo wa Madam Spika, kwanini anaendelea kumsulubisha kila apatapo fursa?!. This is not fair!.

Kwa vile Mama Makinda amepewa uspika because she is a lady, kwa uzi huu, namuomba Mhe. Tundu Lissu na wabunge wengine wa Kambi ya Upinzani, wanapokuwa na hoja za msingi, wamuaddress Madam Spika with courtesy of addressing a lady, ili ku restore confidence yake kuliendesha bunge ambapo kwa sasa, ameshindwa kabisa, amezuia hoja zote binafsi, hivyo leo bunge limekutana asubuhi tuu kwa kipindi cha maswali na majibu na kuahirishwa, natumaini kesho na keshokutwa itakuwa vivyo hivyo!, huu ni ufujaji bure wa rasilimali za Taifa!.

Nawauliza wajameni, hivi hiki anachofanya Mhe. Lissu na wabunge wengine wa upinzani, kumsubulu Madam Spika ambaye ni mwanamke bila huruma, ni sawa kweli?!.

Kiafrika, wanawanake ni ni watu wa kubembelezwa na kuonewa huruma!, hivi hawa wabunge wa upinzani ni watu wa aina gani wasio hata na huruma kwa wanawake?!, leo ilibakia kidogo tuu madam spika angelia!, jee hiki wanachofanya ni sawa kweli?!. Ni haki?!.

Nawaombeni tumtendee haki Spika wetu aendesha bunge kwa haki na kujiamini!.

Pasco.

statements zenye red zahusika mkuu! kam una huruma na mama Makinda basi mfikishie ushauri wako kuwa ajiuzulu! uspika ni kazi na hauna cha mwanamke wala mwanaume! kama amevaa viatu unavyohisi wewe kuwa ni over size basi aachie nafasi hiyo kwa wengine wenye uwezo na kujiamini! hatuwezi kuvumilia spika na naibu spika wanaobaka demokrasia Bungeni. hivyo nakushauri usilete uzi ndani yake ukaweka weak statements!
 
So chama cha mafisadi(CCM) walimweka mtu asie na uwezo mbali na jinsia yake Ili tuwaonee huruma?,hali ya kuwa wao hawana huruma na wanachi na wana waibia bila huruma,manyang'au wakubwa hawa hakuna haja ya kuwaonea HURUMA AIBU wala kucheka nao kwani hao ni kama nyani,UKICHEKA NA NYANI.............Umeona eeeeeh utavuana mashimo nchi nzima kama MWADUI.bKIROBOTO maji yako shingoni Bt mchapeni tu mpaka alowane.
 
Kwa nini anaongea gender inequality kwenye siasa. Only gender equality pertain in politics.

Hutaki kukubali kama wanawake wanataka wawe kama wanaume pamoja na kuwa hawataki wanaume wawe kama wanawake.

Mh. Makinda yuko kwenye hicho kiti kwa 'MERIT' kama wachapuzi wake wanavyotaka kutuaminisha, basi nasi tunatumaini atafanya kazi yake kwa kiwango cha "MERIT" tunayoaminishwa.

Mbona bunge la UK lilikuwa na mwanamke ambaye aliendesha bunge kwa kiwango cha hali ya juu kwa miaka mingi na kumudu vizuri ukilinganisha na aliyepo sasa pamoja na kupata makombora ya hapa na pale, ukizingatia bunge la waingereza kiwango chake ni cha juu.

Uanawake siyo sababu ya msingi kisiasa kama atakuwa fair and firm.
 
Makinda anaharabiwa na INFERIORITY COMPLEX. Anajua Tundu Lissu anamzidi kwa mbali kwenye SHERIA (read Mlima na kichuguu). Na Tundu Lissu anajua fika mama Makinda ni mweupe wa SHERIA. Hivyo Tundu Lissu anatumia huo UDHAIFU wa Spika kumvuruga mama Makinda. Na Mama Makinda anataka kuficha INFERIORITY COMPLEX yake kwa KUVUNJA KANUNI.

Naungana na Sitta(?)/Msekwa(?) aliyeshauri kwamba SPIKA wa Bunge la JMT lazima awe na taaluma SHERIA. Huu UKIHIYO wa SHERIA wa Mama Anne Makinda ndiyo unaomtafuna na wala SIO jinsia yake ya KE. Katiba mpya iweke kigezo cha taaluma ya SHERIA ili kuwa SPIKA wa JMT. (BTW, mimi sio mwanasheria)
 
acha ujinga taifa linaitaji wanawake shupavu na wenye uwezo kama Magreth Thacha na wengine. In shot Anna Makinda amebebwa na majibu wanayaona walio mbeba. Mbona enzi za Mh Sita bunge lilikuwa imara? Tafakari uchukue hatua sio kuandika ujinga ujianga tu.
 
Sijaona sense ya kuwa mwanamke wa ngazi ya juu ndo abembelezwa pale yuko kazini anapoendesha mambo kihuni asitegemee kubembelezwa hata ndani ya nyumba mama anapoleta ujuha habembelezwi tena,kuwa spika wa bunge alihisi anafaa kwa mantiki hiyo acha watu wa wafanye yawapasayo kufanya,kulisukuma gurudumu la maendeleo coz wakimuchekea watavuna mabua.Well well well done wabunge wote wanaojenga hoja makini
 
pasco, ikifika wakati wa kutimiza majukumu hatuangalii kwamba wewe ni mwanaume au mwanamke, as far as amekalia kiti kama spika basi lazima atimize wajibu wake likiwamo like la kutenda haki bila shinikizo toka serikalini.

Mi nafikiri tatizo si Lissu, tatizo ni serikali inapokuwa haija majibu ya hoja za wapinzani bungeni basi spika huombwa kufifisha au kuua kabisa hizo hoja ili kuinusuru serikali, sasa on doing that mama makinda sisi tunamuona kama hawezi kazi ya kuliongoza bunge.
 
Ccm kulia ni kawaida yao hata pinda alipobanwa mwaka ule alianza kulia ili aonewe huruma na huyo mama km alitakakulia aliamua kumwiga bosi wake, tundu lisu endelea hivyohivyo mpaka na jk siku moja adondoshe chozi
 
Pasco,

Kumbuka unapoandika katika jukwaa huru na public kuna wengi wanaokusoma. Inakuwa ni vizuri sana bandiko lako liwe ni for public interest. Na kwa jinsi hiyo madam speaker Makinda yamemkuta si kwa sababu kwa sababu ya jinsia yake au hitikadi yake bali kwa sababu anashindwa kufanya kazi kwa kufuata standards and quality za mabunge wa Jumuia ya Madola au mabunge mengine popote yalipo.

Pili anashindwa kuoanisha (matching) standards and principles na matakwa ya wananchi. Hataki kusikia sauti ya wanyonge kupitia kwa wabunge wanaowasemea.

Tatu ameshindwa kujua ni kwanini amekalia kiti hicho kama kada wa chama au mfuasi wa chama kisichokuwa na hitikadi.Ndio maana hoja yoyote inayotoka nje ya upinzani lazima aipinge, aiwekee vikwazo, aruhusu miongozo katikati ya hotuba ya mtoa hoja.

Nne, mama hana communication skills kabisa maana anatumia lugha mpaka unashindwa kujua kama kweli inatoka katika kinywa cha spika.

Tano jaziba zimemzidi-mtu ukiamua kuwa na cheo kama cha spika unapaswa kuwa na capacitiki ya ku-control immotions na kinyume chake ni kuhisi fulani kaongea hivi kwa sababu ni mpinzani bila kuangalia mantiki ya mtoa hoja. Si kila hoja ya mpinzani haina maslahi kwa Taifa.

Inawezekana iswe na maslahi na CCM na lazima iswe na maslahi na CCM lakini ina maslahi kwa Taifa. Mfano CCM wanajivunia vtyumba vingi vya madarasa lakini visivyokuwa na walimu. Kilimo kwanza isiyokuwa kilimo, mikataba tata isiyo na maslahi kwa taifa hata mtoto mdogo asiyejua contract management analijua hilo. Kambi ya upinzani itakuja na kitu tofauti lakini kwa maslahi ya taifa. Kwa mtu anayeongozwa na jaziba atakataa.

Kwa hiyo Tindu Lisu sio kwamba anamsulubu Makinda kwa sababu ya jinsia yake kinachomsulubu mama wa watu ni facts. Kuliko na facts na wewe hutaki kuzikubali na kuzifanyia kazi lazima sababu za jinsia, upinzani, fujo na mengine yataletwa as defence mechanism geared at justifying the weakness
 
Makinda anaharabiwa na INFERIORITY COMPLEX. Anajua Tundu Lissu anamzidi kwa mbali kwenye SHERIA (read Mlima na kichuguu). Na Tundu Lissu anajua fika mama Makinda ni mweupe wa SHERIA. Hivyo Tundu Lissu anatumia huo UDHAIFU wa Spika kumvuruga mama Makinda. Na Mama Makinda anataka kuficha INFERIORITY COMPLEX yake kwa KUVUNJA KANUNI.

Naungana na Sitta(?)/Msekwa(?) aliyeshauri kwamba SPIKA wa Bunge la JMT lazima awe na taaluma SHERIA. Huu UKIHIYO wa SHERIA wa Mama Anne Makinda ndiyo unaomtafuna na wala SIO jinsia yake ya KE. Katiba mpya iweke kigezo cha taaluma ya SHERIA ili kuwa SPIKA wa JMT. (BTW, mimi sio mwanasheria)[/QUOTEt]

Mkuu huyu Jobless Ndugai anataaluma ya SHERIA?
 
Back
Top Bottom