Elections 2010 Mheshimiwa John Pombe Magufuli awe Rais wetu

Kwa muono wangu huyu bwana ndio anafaa kumrithi Kikwete, kwa Nchi yetu ilipofikia tunahitaji Rais mwenye msimamo na mbabe kama huyu jamaa, hatuhitaji tena mtu soft!!!!!

Nakuunga mkono. Tulipofika, hatujui kesho kuna nini!!
 
kwa muono wangu huyu bwana ndio anafaa kumrithi kikwete, kwa nchi yetu ilipofikia tunahitaji rais mwenye msimamo na mbabe kama huyu jamaa, hatuhitaji tena mtu soft!!!!!
kufokafoka hovyo hakumaanishi kwamba yeye ni kiongozi bora na mara nyingi mtu mkali na mfokaji sana nyuma yake kuna kitu anaficha.
 
Acheni ushabiki wa mavyama yenu,semeni kwanini anafaa na kwanini hafai,ili hata wasiomjua wafahamu kiundani uzuri wake na udhaifu wake kiutendaji.
 
Rasmi Magufuli umeingia kwenye Mitandao.........Sooon tutakumbusha zile Series za Rai wakati ule wakina Gen. Ulimwengu:A S 39:
 
Yalikuwa ni maamuzi ya serikali nzima JK kipindi hicho akiwemo iweje umuhukumu yeye binafsi, yeye alitekeleza kama waziri mwenye dhamana! Au nawe ndo wale wanawahukumu kwa kuwaandika majina watendaji wa serikali badala ya kuishitaki serikali?

mkuu usipokubaliana na uamauzi au ukiona uamuzi ni mbaya unajiuzulu,huyu ni mwizi tu hakuna jina jingine
 
Si kila waziri anaweza kuwa raisi wa nchi. Mhe. Magufuli ana uthubuti wa kupewa majukumu na kuyasimamia na si vinginevyo. Kwa misimamo yake bora abaki kuwa waziri kwani zaidi ya hapo anaweza kuongoza nchi kidikteta.

Na tulipofikia tunahitaji kiongozi wa namna hii, vyakula vyote vitashuka bei, mafuta n.k
 
Dr. John Joseph Pombe Magufuli akisimamishwa na CCM basi uchaguzi utakuwa umeisha in favour of CCM. Iwe hafai au anafaa lakini wananchi wana imani naye kiasi cha kutosha kwa hiyo anafaa.
 


Kwenye RED; that is precisely kinachosemwa na watu tunaomfahamu Magufuli kwa kufanyakaz nae. Usichokijua wewe (na wenye mtazamo wako kuhusu Magufuli) ni kuwa huyu bwana huwa anafanya mambo bila kufikiri kitakachotokea baadae. Kwa taarifa yako, Mwakajinga alikopeshwa hilo gari (kuna kipindi serikali iliwakopesha maofisa stahili magari ambayo yalikuwa yanamilikiwa na serikali na mkopaji hakurushusiwa kubadilisha namba hadi amalize kulipa). Udhalilishwaji huo kwa Mwakajinga na wengine kuliigharimu serikali maana wote waliochukua hatua walilipwa fidia. Waziri makini angejua hayo kabla hajayatangaza hadharani.

Umem-credit Magufuli na ujenzi wa km 11000 za barabara, ila usichokijua ni kuwa barabara hizo zote zimejengwa kwa fedha za wafadhili au mikopo ya benki ya dunia (na usimamizi wake hufanywa na donors wenyewe). Na process ya kupata fedha za kujenga hizo barabara zilianza na kujadiliwa kwa proposals za serikali ya awamu ya kwanza na ya pili. Unamsifia aliekabidhiwa barabara iliyokamilika wakati aliefanya kazi ya kujenga si yeye!

Kwa kifupi; huo "uchapakazi" wa Magufuli ni wa media tu!
 

Hivi wewe ulielewa nilichokiandika au ulipokuwa unasoma ulikuwa umelewa???? Unajua hesabu wewe?? Hivi miradi 29 kati ya 68 ndio 70%, what have you been drinking sir??

Hebu nionyeshe nilipoandika ulichodai kuwa nimeandika hapo kwenye RED. Uwe unasoma na kuelewa, au na wewe ni "educated illiterate"???
 
Slaa hata akihamia CCM hatakuja kuwa rais wa Tanzania

Hv wewe nani kakudanganya CCM wanaweza kuwa madarakani 2015 mpaka udiriki kusema Slaa hata akihamia CCM hawezi kuwa Rais. CCM imeshakufa.

Kwa upande wa Magufuli ni mtendaji mzuri, sitaki kumbeza kazi anayofanya wote tumeiona, ila kwa nafasi ya Urais bado sana. Jamaa ni mtendaji mzuri ila sioni sifa za urais kwake hasa kwa jinsi ya alivyo na Jazba na kukurupuka sana katika mambo mengi. Namkubali sana tu kama ana mtu juu yake wa ku control decisions zake.


Nisaidien wanajamvi hivi huyu Emmanuel Nchimbi mbona naona Kama CCM wanamkuza sana, ana lipi la kumsafisha hivyo?
 
hebu endeleeni kumchambua maana sie wengine huwa tunamsikia tu kwenye ufunguzi wa ujenzi wa mabarabara.
ni mbabbe asiye na huruma ......huwezi chekelea kuwabomolea maskini katika nchi ambayo hakuna sera /haitekezwi .....asiliamia 90 ya makazi hayajapimwa ni kosa la wamiliki wa nyumba au serikali
 
Kuna kakipande ka barabara fulani kako mwanza palipoishia barabara ya Green Acre. Kila mwezi Nyanza toad wako aple wanajenga toka mwaka 2005. Unajua ni project ya nani? Mi mwenye nisingempa kura yangu bora nipigie jiwe.
Dodoma yote pale mjini ni nyanza, haka kakampuni kana mlio wa mbu, anaekajua atumwagie
 
Watu bana wakiamua kumpaka mtu matope, eti "BUTA BABA GETE MTALEOBONE LAMI"
 

Nikibishana na wewe nitaonekana pia sina akili, wewe ni wa kukuacha mwenye kuelewa atafuatilia na tajua ukweli upo wapi!
 



Una agenda yako ya Siri, Magufuli jembe japo hajastahili kuwa Rais. Au na wewe (Jamaa yako) ni mmoja wa waliokuwa wameregister magari ya umma kwa jina binafsi.
 
Una agenda yako ya Siri, Magufuli jembe japo hajastahili kuwa Rais. Au na wewe (Jamaa yako) ni mmoja wa waliokuwa wameregister magari ya umma kwa jina binafsi.

Maybe una umri mdogo sana (kiasi kwamba yalipokuwa yanafanyika niliyoyasema hapa hukuwa na uwezo wa kuyafuatilia) au uelewa wako wa jinsi serikali inavyofanya kazi ni practically zero. Maana kama miaka ya 90 ulikuwa na angalau miaka 18 ungeshasikia programs nilizozisema hapa, na kama ulikuwa mkubwa na hukuzisikia hilo si kosa langu. It is your loss not mine being ignorant of things that are common and open to the members of the public (who care to know them that is).

As far as Magufuli is concerned, sina ajenda nae, iwe ya siri au isiyo ya siri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…